JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA.
Mnamo
tarehe 27.04.2016 majira ya saa 20:00 usiku huko katika Kijiji na Kata
ya Matundasi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, watu
watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi waliuawa katika majibizano ya risasi
na askari polisi wakiwa katika harakati za kufanya uhalifu kwenye duka
bia la jumla mali ya bwana HAMIS mkazi wa Matundasi.
Inadaiwa
kuwa majambazi hao wapatao watano walikuwa wakitumia pikipiki mbili
huku pikipiki moja ikibeba majambazi watatu na nyingine majambazi wawili
huku wakiwa na silaha aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 na risasi
26 kwenye magazine walitaka kufanya uhalifu kwenye duka la jumla la
kuuza bia mali ya HAMISI.
Kutokana
na taarifa za siri/intelejensia, Jeshi la Polisi lilijipanga
kukabiliana na majambazi hao na katika majibizano ya risasi, jambazi
mmoja ambaye alikuwa na silaha aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120,
risasi 26 kwenye magazine aliuawa baada ya kujeruhiwa kwa kupigwa risasi
tumboni na mguuni na aliweza kufahamika kwa jina moja BARAKA,
anayekadiliwa kuwa na umri kati ya 35 hadi 38, fundi ujenzi mkazi wa
Makongolosi.
Aidha
majambazi wengine wanne walifanikiwa kukimbia kuelekea kijiji cha
Matondo na ndipo askari polisi waliendesha msako mkali kuelekea kijiji
hicho na majambazi hao baada ya kuwaona Polisi waliwasha pikipiki zao
kwa nia ya kukimbia huku wakirusha risasi ovyo ndipo Polisi walijibu
mapigo na kufanikiwa kuwaua majambazi wengine wawili na kukamata
Pikipiki moja yenye namba ya usajili MC 761 AFS aina ya Sanlg iliyokuwa
ikitumiwa na majambazi hao.
Majambazi
wengine wawili walikimbia na msako mkali unaendelea ili kuwakamata.
Miili ya marehemu imehifadhi katika Hospitali ya Wilaya Chunya.
Wito:
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Butusyo A.
Mwambelo anatoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la
Polisi kwa kutoa taarifa za siri ili kuzuia vitendo vya kihalifu mapema
kabla ya kutokea.
Imesainiwa na:
[BUTUSYO A. MWAMBELO – SSP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
No comments:
Post a Comment