Viongozi
wa Chama cha UDP wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha
Kijamii (CCK), kwa madai kinaongozwa kibabe, hakuna Mikutano wala vikao
vinavyofanyika ili kukijenga.
Viongozi
hao ni aliyekuwa mkurugenzi wa uchaguzi wa UDP na Mwenyekiti Wa chama
hicho Mkoa wa Mtwara, Salum Makunganya na Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es
Salaam na mjumbe wa kamati kuu, Joachim Mwakitiga.
Wakizungumza
baada ya kukabidhiwa kadi za chama chao kipya , Viongozi Hao
walisema UDP imegeuzwa mali ya mtu mmoja ambaye Huamua Mustakabali wa
chama kwa matakwa yake.
Mwakitiga alisema uhai wa chama ni mikutano ambayo inawapa fursa Viongozi kujadili na kupanga mikakati ya kukijenga.
Alisema
jambo la kushangaza kwenye chama hicho mwenyekiti wa Taifa wa Chama
hicho, John Cheyo haitishi mikutano wala vikao vya ndani.
Makunganya alidai kwa miaka mitano chama hicho hakijaitisha mikutano wala vikao vya kamati kuu na halmashauri kuu ya chama.
Makunganya alidai kwa miaka mitano chama hicho hakijaitisha mikutano wala vikao vya kamati kuu na halmashauri kuu ya chama.
Alisema
chama ni taasisi na taasisi ni watu, hivyo, viongozi waanzilishi Wanatakiwa kufahamu kwamba chama siyo mali yao bali ni ya wanachama Wote.
Makunganya alisema amejiondoa katika chama hicho ili kutafuta Demokrasia ya kweli sehemu nyingine.
Makunganya alisema amejiondoa katika chama hicho ili kutafuta Demokrasia ya kweli sehemu nyingine.
Katibu
Mkuu wa CCK, Renatus Muabhi alisema wameanza operesheni ya kukijenga
chama chao na viongozi wataanza kuzunguka nchi nzima kufungua matawi na
kuchagua viongozi.
Mwenyekiti
wa Wanawake CCK Taifa, Salama Juma (kulia), akizungumza Wakati wa
kuwapokea viongozi hao. Kushoto Salum Makunganya aliyekuwa Mwenyekiti wa
UDP Mkoa wa Mtwara aliye hamia CCK.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (kulia), Akimkabidhi
kadi ya chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam,
Joachim Mwakitiga aliyejiunga na chama hicho na aliyekuwa Mwenyekiti wa
chama hicho Mkoa wa Mtwara, Salum Makunganya Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (kulia), Akimkabidhi
kadi ya chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara, Salum
Makunganya aliyehamia chama hicho.
No comments:
Post a Comment