Na Chrispino Mpinge
Kiti
cha Spika wa Bunge kimesema ipo Haja ya kufanya Marekebisho ya Sheria
pamoja na Kanuni ili kila mbunge apate posho kulingana na kazi Aliyofanya Bungeni, Badala ya Utaratibu wa sasa wa kuangalia mahudhurio Pekee.
Aidha, kimewataka wabunge kubadilika na kuacha tabia ya kuchukua Posho Za vikao vya Bunge Bila kuzitolea Jasho.
Kauli
hiyo imekuja kutokana na Mwongozo ulioombwa Aprili 25, mwaka huu Na
Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) ambaye alikitaka kiti cha
Spika kutoa Mwongozo kuhusu Usahihi wa wabunge wa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni kulipwa Posho na Mishahara wakati hawashiriki na
kutimiza wajibu wao wa kuchangia kwenye Mjadala wa Bunge la Bajeti
linaloendelea katika Mkutano wa Tatu wa Bunge la 11.
Bashe
alisema mbunge huyo alitumia Kanuni ya 68(7) ya Kanuni za Kudumu Za
Bunge akiomba Mwongozo wa Spika kutokana na Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni, kuamua kutoshiriki mjadala unaoendelea Bungeni, lakini Wabunge
hao wanasaini na kulipwa Mishahara na posho.
Hivyo akaomba Mwongozo endapo ni haki kwa wabunge hao kupokea Posho wakati hawashiriki wala kutimiza wajibu wao wa kisheria.
Katika kujenga hoja hiyo, Bashe alitumia Ibara ya 63(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania isemayo, “Kwa
madhumuni ya Utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza kujadili
utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa
bajeti.”
Aidha,
Bashe alitumia Ibara ya 73 ya Katiba ya Tanzania kufafanua kuhusu Malipo ya Mshahara, Posho na Malipo Mengine kwa Wabunge.
Akitoa
Mwongozo wa Spika, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson Alisema kwa
mujibu wa Katiba ya Tanzania, Ibara ya 73 imeainisha Masharti ya kazi ya
wabunge.
Alisema Mbunge anastahili kulipwa mshahara kwa kila mwezi, na kufafanua kuwa
mbunge anapohudhuria vikao Bungeni na kamati atalipwa posho ya vikao kwa
kiwango kitakachowekwa na Serikali na Kanuni za Bunge.
Alisema Malipo ya Mshahara ni suala la Kikatiba na Sheria hulipwa kwa Mbunge kutokana na kazi yake ya Ubunge.
Hivyo Malipo ya posho kwa Wabunge Yanatokana na Mahudhurio yao Bungeni na
siyo kwa kuchangia kama ambavyo wengi wao Wanapenda iwHivyo.
“Kimsingi
kuhudhuria Bungeni pekee siyo njia inayopendeza kwa kuwa Mbunge
anapofika Bungeni anatarajiwa atekeleze Majukumu yake Yalivyoainishwa
katika Ibara ya 63.
“…Tabia
hii ya kutochangia mijadala na kuzunguka Zunguka Bungeni Haikubaliki na
haitakiwi kuendelea, kila mbunge atekeleze wajibu wake na Sio
anahudhuria ili alipwe posho,” alisema Dk Ackson.
Wakati
huo huo, Spika wa Bunge, Job Ndugai amefanya mabadiliko katika Kamati
mbalimbali za Bunge, kwa kubadilisha wabunge 16 wa Kamati za Awali
kwenda nyingine.
Aidha,
Spika amewapangia Kamati wabunge wapya wanne, walioapishwa Mwanzoni mwa
Mkutano huu wa Bunge, ambao ni Shamsi Vuai Nahodha, Rita Kabati, Oliver
Semuguruka na Lucy Owenya.
No comments:
Post a Comment