Aliyekuwa Mkurugenzi wa TIC Julieth Kairuki Hakuchukua Mshahara Miezi 36
Na Kalonga Kasati
Hali ya Utumbuaji wa Majipu ikiendelea kwa Wakurugenzi wa Taasisi za Serikali ikitofautina Mitazamo ya Watu wengi Hali hii Wanaipenda na Wengi Hawakubaliana na Hali hii ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kuwatumbua na akiacha Majipu Mengine kuyatumbua akiwemo Waziri wa Ujenzi wa Awamu ya nne na Marais Wastaafu akiwaacha na lingine Nikupata katiba Mpya Na Bunge kuonyeshwa live haya ni Baadhi ya Mambo yakiwakera Watanzania Walio Wengi
Licha ya kupingwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania
(TUCTA) Baada ya kutangaza kupunguza Mishahara ya Watumishi wa Umma toka Milioni 40 hadi 15, leo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.
John Pombe Magufuli ametengua Uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Uwekezaji (TIC), Juliet Kairuki.
Dk. Magufuli amefikia Maamuzi hayo baada
ya kubaini Mkurugenzi huyo kutochukua Mshahara wa Serikali katika
kipindi Miezi (36) tangu alipoajiriwa Aprili 2013 kwa Madai kuwa Mshahara huo ni mdogo.
Machi 29 mwaka huu Rais Magufuli akiwa
mjini Chato wakati wa mapumziko ya wiki moja Alitangaza kupunguza
mishahara ya juu kutoka Sh40 milioni hadi Sh15 milioni kwa mwezi na
kusema “wapo watumishi wa umma
wanalipwa masilahi manono na kuishi kama wako peponi, Huku wanaolipwa
Sh300,000 wakiishi kama wako jehanamu”.
Aidha taarifa hiyo inasema Rais Magufuli
amemteua Clifford Katondo Tandari kukaimu Nafasi hiyo, huku mchakato wa
kumpata Mkurugenzi mpya Ukianza Mara moja.
No comments:
Post a Comment