Deni la Taifa limeongezeka Kwa 27% Na Misamaha ya kodi Trilioni 1.6
Na Chrispino Mpinge
Ripoti hiyo inaonesha kati ya Halmashauri 164 Zilizokaguliwa, 47 pekee ndizo Zimepata hati Safi,
nyingine Zilizobakia zina hati zenye mashaka, zisizoridhisha na chafu.
Kwa upande wa Mashirika ambayo Ripoti hiyo imeyagusa, Shirika la Usafiri
Dar es Salaam (UDA) limebainika Mauzo ya hisa zake yalikuwa Batili,
hivyo CAG ameshauri lirudi chini ya Usimamizi wa Serikali hadi hapo
mgogoro wa mgawanyo wa hisa utakapotatuliwa.
Kuhusu Wakala wa Usafiri wa Mwendo wa
Haraka Dar es Salaam (DART), ripoti ya CAG imebaini kuwa kwa Mwaka wa
fedha 2014/15 wakala huyo aliingia Mkataba na UDA-RT wa kutoa Huduma ya Usafiri wa mpito wa kuendesha Mabasi 76 kulingana na Vigezo Vilivyoainishwa kwenye Mkataba.
Lakini, Sheria ya Manunuzi ya Umma,
mkataba huo ulitoa ongezeko la ununuzi wa mabasi na kufikia 84 ili
kulingana na matakwa ya DART. Hata hivyo kwenye ukaguzi wa hesabu zao,
CAG alibaini kuwepo na Ununuzi wa mabasi 140 ambayo ni sawa na ongezeko
la mabasi 56 Yasiyo ndani ya mkataba.
Aidha, ripoti hiyo imepigilia Msumari
kwenye suala la watumishi hewa na kusema tatizo hilo limekuwa sugu na
serikali za mitaa zinaongoza kwa kulipa mishahara watumishi waliofariki
na Waliotoroka huku Sh bilioni 2.7 zikiwa zimetumika mwaka wa fedha
2014/15 kwa malipo hayo.
Jambo lingine ambalo limejitokeza
kwenye ripoti ya CAG, ni utoaji wa misamaha ya kodi kwa kiwango cha juu
huku ikionesha Sh trilioni 1.6 sawa na asilimia mbili ya pato la ndani
la taifa, Zilisamehewa katika kipindi kilichoishia Juni 30, 2015.
Alisema kwa mwaka unaoishia Juni 30
,2015, jumla ya hati za ukaguzi 465 zilitolewa kwa Serikali Kuu,
Serikali za Mitaa na mashirika ya umma. Ripoti imeonesha kuwa mashirika
ya Umma na Serikali Kuu yamefanya vizuri kwa kupata hati nyingi safi,
huku zile za mashaka Zikiwa chache.
Aidha Hakuna Hati Mbaya wala
isiyoridhisha. Akifafanua alisema katika Ukaguzi huo, Halmashauri ndizo
zinaongoza kwa kufanya vibaya . Kati ya halmashauri 164 zilizokaguliwa,
47 pekee ndizo zimepata hati safi, nyingine zilizobakia ni zenye
mashaka, zisizoridhisha na Chafu.
Wakati huo huo, akizungumzia misamaha
ya kodi kwa kipindi kilichoishia Juni 30, 2015, Profesa Assad alisema
ripoti yao inaonesha kuwa kiasi cha misamaha kilichotolewa ni Sh Trilioni 1.6 sawa na asilimia mbili ya pato la ndani la taifa.
Kiwango hicho kwa Mujibu wa Profesa
Asaad, ni cha juu ikilinganishwa na lengo la serikali la kupunguza
misamaha hiyo isizidi asilimia moja ya pato la Taifa.
Katika Misamaha hiyo, pia kuna utata
kwenye mafuta yenye Dhamana ya kodi ya Sh bilioni Tano ambayo
yalionekana kwenye mfumo wa forodha wa (TANCIS) kuwa yamesafirishwa nje
kupitia nchini lakini hakuna ushahidi wa hilo.
Akizungumzia deni la taifa, Profesa
Asaad alisema hadi kufikia Juni 30, mwaka 2015, deni la Taifa lilikuwa
Sh trilioni 33.54. Deni la ndani lilikuwa Sh trilioni 7.99 na deni la
nje likiwa Sh Trilioni 25.5 hivyo jumla ya deni lote likiongezeka kwa
asilimia 27 ikilinganishwa na deni lililoishia Juni 30, mwaka 2014,hivyo
ameishauri Serikali kuongeza jitihada za kukusanya kodi ili kulipa
madeni.
No comments:
Post a Comment