Mahakamani
ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imesita kutoa Uamuzi wa
kesi inayowakabili Harry Kitillya, Shose Sinare na Sioi Solomoni kwa
madai, jalada lake limeitishwa Mahakama Kuu.
Kitillya,
alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA); Sinare, Mkuu
wa Idara ya Ushirikiano na Uwezekezaji katika Benki ya Stanbic na Sioi,
Mwanasheria wa Benki ya Stanbic.
Amilis
Mchaura, Hakimu Mkazi Kisutu amesema kuwa, hana mamlaka ya kutolea
uamuzi wa kesi hiyo kutokana na jarada lake kuitishwa Mahakama Kuu leo
asubuhi.
Kutokana
na hali hiyo Hakimu Mchaura amesema kwamba, kesi itatajwa tena tarehe
12 Mei mwaka huu na watuhumiwa watarudishwa Rumande.
Muda
mfupi baada ya hakimu Mchaura kusema hivyo, Kitilya na wenzake
walirudishwa tena mbele ya Hakimu huyo baada ya hakimu kupata amri
kutoka kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Akimtaka
kesi hiyo itajwe Mei 3, mwaka huu badala ya tarehe 12 Mei mwaka Huu
aliyoipanga awali.
Hakimu
Mchauru amesema, sababu za kupewa amri hiyo hazijui, hivyo kesi
itatajwa tena tarehe 3 Mei mwaka huu na yale yaliyozungumzwa asubuhi
yatabaki kama ilivyo.
No comments:
Post a Comment