Saturday, 2 April 2016

Kamal steel Yasaidia Viungo Bandia Wenye Ulemavu

index 

Na Chrispino Mpinge

KAMPUNI ya kutengeneza chuma ya Kamal Steel Ltd, imetoa msaada wa viungo bandia,  kwa Watu wenye ulemavu 16, vyenye thamani ya zaidi ya  sh. milioni 80.

Akifunga kambi ya kutoa  viungo bandia hivyo, jana jijini Dar es Salaam sambamba na kukabidhi Vifaa hivyo,   Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe,  alisema,  serikali  itaendelea kuwawezesha watu wenye ulemavu nchini ili waweze kukabiliana na changamoto Zinazowazungika ikiwa ni pamoja na kuwapatia vifaa bandia.

Alisema, suala la ulemevu  linagusa  maisha ya kila mwanadamu na kwamba ,tu yoyote anaweza kufikwa na tatizo hilo.

Alibainisha,   viungo bandia vinauzwa kwa ghala makubwa ambayo watu wengi wenye ulemavu Hawawezi kumudu kununua  hivyo serikali  kwa kushirikiana na wadau wake itaendelea kutoa ,saada  wa vifaa hivyo.

“Jamii iamini kuwa wote ni walemavu watarajiwa. Kupoteza kiungo kimoja cha mwili ni Changamoto kubwa.  Tunaishukuru kampuni ya Kamal Steel kwa kutoa misaada hii muhimu  Ambayo tunaamini kuwa inasaidia kupunguza madhira ya  ulemavu,”alisema  Dk. Mwakyembe Ambaye kupitia msaada huo ameweza kuwasaidia watu wenye ulemavu wanne kutoka jimbo lake la Kyela mkoani Mbeya.

Mwenyekiti wa makampuni ya Kama Group , Gagan Gupta, alisema,kampuni yake haijatoa viungo bandia hivyo kama msaada, bali kama wajibu wake  kwajamii.
“Tunaamini kwamba, viungo hivi bandia vitawawezesha  kumudu kutembea, kufanya kazi Mbalimbali zitakazo waletea kipato,”alisema Gupta.

Katika  hatua nyingine,  Gupta aliahidi kumuajiri  mmoja  wawatu hao wenye ulemavu  mwenye taaluma ya ufundi mitambo,  Siaga Raphael ambapo alisema ajira yake itaanza  leo.
“Huyu  atafundishwa ufundi wa kutengeneza vifaa mbalimbali hasa vya watu wenye ulemavu hapa, ili aweze kusaidia  kuwafundisha watu wenye ulemavu wengine.Mradi anataaluma hiyo ataanza kazi kesho asubuhi (leo asubuhi),”alisema  Gupta.

Mkurugenzi Mkuu wa Kamal Steel, Sameer Gupta, alisema, kampuni hiyo imekuwa mstari wa Mbele katika kusaidia viungo hivyo bandia kwa watu wenye ulemavu ambapo mpaka sasa imesaidia watu 200.

“Tutaendelea kuwasaidia  kila mara  ili tuweze kuisaidiana na serikali yetu kuwaondolea changamoto wenzetu hawa. Tunaamini wakipewa viungo hivi bandia wanaweza kushiriki  shughuli Mbalimbali muhimu zitakazowaingizia kipato,”alisema.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake walio pokea msaada huo, Siaga Raphael,   aliipongeza kampuni hiyo kwa masaada wa vifaa hivyo na kuitaka serikali  kuwa kumbuka watu wenye Ulemavu kwa kuwasaidia pia kuwapa taaluma   ya ufundi itakazowawezesha kujimudu kimaisha.

No comments:

Post a Comment