Mbivu na Mbichi leo Kujulikana Kati ya Yanga na Coastal Union
Na Kalonga Kasati
Mechi ya nusu fainali kati ya Yanga na
Coastal Union iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga mwishoni mwa
wiki iliyopita ilivunjika katika dakika ya 110 baada ya Wachezaji wa
Coastal kukataa bao la pili la Yanga na kuanzisha vurugu zilizosababisha Mshika kibendera namba mbili Charles Simon kupasuliwa jicho la kushoto
kwa jiwe lililotupwa na Shabiki.
Kaimu Mkurugenzi wa mashindano wa TFF,
Jemedari Said alisema wanasubiri ripoti ya Kamisaa na Mwamuzi ndipo
watoe maamuzi. “Jambo kama hilo likishatokea ni lazima kamati Ya
mashindano ikutane, kuangalia sheria na kanuni zinasemaje kabla ya kutoa
maamuzi,” Alisema.
“Taarifa tayari tunazo, ripoti zote
zinatarajiwa kuwasilishwa ofisini leo hii (jana) na kisha kamati chini
ya Mwenyekiti Geofrey Nyange ‘Kaburu’ itakutana haraka iwezekanavyo Kuamua,” alisema Said.
Katika mechi hiyo Coastal Union
iliyoonesha soka safi ilipata bao la kuongoza kupitia kwa kiungo Wake
Youssouf Sabo na Yanga ilisawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake Donald
Ngoma.
Dakika 90 za mechi hiyo zilimalizika
bila kupata mshindi na ndipo ilipoamuliwa timu ziende Muda Wa nyongeza
wa dakika 30, ambapo dakika za mwanzoni tu Amisi Tambwe aliifungia Yanga
bao la Pili na ndilo lililozua kizaazaa, ambapo Coastal ilidai Tambwe
alifunga kwa Mkono.
No comments:
Post a Comment