Said Miraji:ADC Kuna Watu Wenye Uchu wa Madaraka Wanaotaka kuharibu Taswira Njema ya Chama kwa Maslahi Yao Binafsi
Na Chrispino Mpinge
Kuna usemi usemao “hakuna rafiki wa kudumu kwenye siasa na hakuna adui wa kudumu Kwenye siasa, na wengine wanasema siasa ni mchezo mchafu”. Semi hizi zina maana kubwa Sana Na hii inatokana na mabadiliko ya wanasiasa kwa kufuata upepo.
Hivi karibuni Chama Cha Allience For
Democratic Change (ADC) kiliingia kwenye mgogoro Baada ya Mwenyekiti wa
chama hicho Said Miraj kuifuta Idara ya Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama
iliyokuwa inasimamiwa na Omari A. Costastine, ambapo mwenyekiti huyo
alifanya Hivyo kwa Mujibu wa Tamko la vyama vya siasa kutoviruhusu vyama
kuwa na vikundi vya Ulinzi na Usalama.
Maamuzi Hayo ya Mwenyekiti Said Miraj Yaliipelekea Bodi ya Wadhamini kutoutambua Uongozi wa Said Miraj na
kuunda Kamati Tendaji, jambo lililopelekea Mwenyekiti kupeleka Malalamiko hayo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, ambapo ametoa maamuzi ya
kumtambua Mwenyekiti wa chama hicho na kueleza kuwa kwa Mujibu wa
Katiba ya ADC Bodi ya Wadhamini haina Mamlaka ya kuufuta Uongozi wa
chama hivyo Maamuzi hayo ni batili.
Hivyo Mwenyekiti huyo wa Chama cha ADC
Said Miraji amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini kusimamia maamuzi
yake ambayo yanakiukwa na Bodi ya wadhamini, huku Akieleza kuwa bodi
hiyo inaitisha vikao vya chama kinyume na katiba ya ADC inayohitaji Ridhaa ya Kamati Kuu ya Uongozi.
Vilevile ameongeza kuwa ADC imevamiwa na
watu wenye Uchu wa Madaraka Wanaotaka kuharibu Taswira Njema ya chama,
kwa Maslahi yao Binafsi bila kufuata Taratibu na Sheria Za Chama hicho.
No comments:
Post a Comment