TCRA: Baadhi ya Wauzaji wa Simu Wanatoa Punguzo Kwa Wananchi ili kuwashawishi Kununua Simu Bandia kwa Bei Nafuu
Na Kalonga Kasati
Tarehe April 23 Mwaka huu China
ilizifungia Huduma za kampuni ya Apple katika mtandao Pamoja na zile za
filamu katika Harakati ya kuweka Sheria kali Zitakazosimamia kile
kitakachochapishwa Mtandaoni.
Nchi nyingi Duniani zimeridhia kupitisha
Sheria ya Makosa ya Mtandao, lengo kuu likiwa ni Udhibiti wa Uhalifu Mitandaoni na kuendelea kuboresha Teknolojia kadri inavyoendelea kukua,
Desemba 17 Mwaka Jana Ulizinduliwa Mfumo wa Uhifadhi namba Tambulishi za
vifaa Vya Mawasiliano kwa Simu za Mkononi (IMEI) kwa lengo la
kufuatilia namba tambulishi kwa Vifaa Vinavyoibiwa na vile Visivyokidhi Viwango.
Akibainisha kazi zilizofanyika tangu
kuzinduliwa kwa mfumo huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba amesema Mamlaka hiyo
imeendelea kufanya Uchambuzi wa kina ilikupata mwelekeo halisi kabla ya
kipindi kilichowekwa kuisha na Hatimaye simu ambazo hazikukidhi vigezo
kuzimwa rasmi Juni 17 Mwaka huu.
“Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania imeendelea kusimamia kwa karibu makampuni ya
simu Hapa nchini katika uendeshwaji wa kila siku wa mfumo wa rahisi za
namba za utambulisho wa Vifaa vya mawasiliano vya mkononi, ili kupata
mwelekeo halisi kabla ya kipindi cha mpito kuisha Juni 17, mwaka huu”. Alisema Kilaba
Pamoja na hayo changamoto inayokabili
mfumo huo ni pamoja na uaminifu mdogo kwa Baadhi ya wauzaji wa simu kwa
kutoa punguzo kwa wananchi ili kushawishi kununua simu Bandia kwa bei
nafuu.
No comments:
Post a Comment