AFISA Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara Bw. Julius Bujabhi Makwasa amehukumiwa kifungo cha Miaka 7 jela baada ya kupatikana na hatia ya Makosa 34 yakiwepo ya Rushwa.
Mnamo
mwaka 2013 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Mara
ilimfikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Serengeti Afisa uchaguzi wa
Halmashauri hiyo Bwana Julius Bujabhi Makwasa na wenzake wawili Wakishitakiwa kwa makosa thelathini na manne yakiwemo ya matumizi Mabaya
ya fedha za umma, kuisababishia hasara Halmashauri ya Serengeti,
kusaidia kutenda kosa, kughushi na kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri
wao.
Washitakiwa
wengine katika shauri hilo la uhujumu Uchumi E.C.C 130/2013 lililokuwa
likisikilizwa na Hakimu wa Mahakama hiyo Mheshimiwa Ismail Emanuel
Ngaile, walikuwa Bi Scola Daudi Mosi ambaye ni mtunza kumbukumbu wa
Halmashauri hiyo na Bwana Dickson Julius Makwasa Ambaye ni mtoto wa
mshitakiwa wa kwanza.
Ilidaiwa
na mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Wakili Martin Makani Mbele ya
mheshimiwa Ngaile kwamba mshitakiwa wa kwanza Julius Makwasa ambaye
majukumu yake yalikuwa pamoja na kuviteketeza vifaa Vya uchaguzi muda wa
uchaguzi unapopita na mshitakiwa wa pili Scola Mossy ambaye majukumu
yake ni pamoja kusimamia kumbukumbu Zinazoingia na zinazotoka nje ya
Halmashauri hiyo, kwa nafasi zao hizo, Walikuwa na jukumu la kuharibu
nyaraka za uchaguzi mkuu wa Octoba 2010 kama ilivyokuwa imeelekezwa na
Tume ya Taifa ya uchaguzi.
Katika
kutekeleza jukumu hilo ilielezwa kwamba, waliandaa majina ya Vibarua na
kuingiza majina hewa ishirini na tano (25) kuonyesha kwamba Majina hayo
hewa pia yalishiriki kuchimba mashimo, kusomba nyaraka Hizo za
uchaguzi na kuzipeleka kwenye mashimo kisha kuziteketeza kwa Moto hivyo
kustahili malipo.
Katika
udanganyifu huo ilielezwa kwamba, mshitakiwa wa kwanza na wa pili
waliweza kuandaa nyaraka za kuipotosha Halmashauri ya Wilaya ya
Serengeti na kuwawezesha kujipatia jumla ya shilingi million tatu laki
nane Na elfu hamsini (Tsh 3,850,000/=) kwa kutumia nyaraka kumdanganya Mwajiri .
Aidha
katika mashitaka hayo, mshitakiwa wa tatu Dickson Makwasa ambaye Ni
mtoto wa mshitakiwa wa kwanza yeye alishitakiwa kwa kosa moja la
kusaidia kutenda kosa kwa maelekezo ya baba yake Julius Bujabhi Makwasa,
ambapo ilielezwa na upande wa mashitaka kuwa alielekezwa na Baba yake
kutafuta na alitafuta wanafunzi wenzake na kuwapeleka ofisi za
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwa mtunza fedha na huko walitakiwa
kutia sahihi mbele ya majina hewa yaliyokuwa yameorodheshwa kisha
kulipwa fedha zilizoainishwa kwa kila jina kama kwamba ni wao walifanya
kazi ya kuteketeza vifaa hivyo vya uchaguzi.
Hata
hivyo baada ya kupokea fedha hizo wanafunzi hao walitakiwa wazikabidhi
kwa mshitakiwa wa tatu na wakazikabidhi, ambaye naye Alimkabidhi
mshitakiwa wa kwanza ambaye ni baba yake.
Baada
ya mahakama kupitia ushahidi uliowasilishwa na upande wa Mashitaka na
ule wa utetezi iliridhika kwamba mshitakiwa wa kwanza Alitenda makosa
yote (33) aliyoshitakiwa nayo na hivyo kuhukumiwa kifungo, kulipa faini
ya shillingi millioni tano (Tsh.5,000,000/=) au kifungo Jela miaka saba
na kurejesha fedha jumla ya shilingi million tatu, laki nane na hamsini
elfu ( 3,850,000/=) hasara aliyoisababishia Serikali, alishindwa kulipa
fedha hizo na kupelekwa jela kuanza kutumikia kifungo.
Mshitakiwa
wa pili alionekana hana hatia hivyo mahakama ilimuachia huru, kwa
upande wa mshitakiwa wa tatu ambaye kosa lake lilikuwa kusaidia kutenda
kosa kwa maelekezo ya baba yake alipatikana na hatia ya kosa hilo Na
alihukumiwa kulipa faini ya shilingi million moja (TSH.1000,000/=) au
kwenda jela miaka mitatu, aliweza kulipa fedha hizo na akaepuka kifungo.
TAKUKURU
Mkoa wa Mara inatoa mwito kwa wazazi hasa walio kwenye Utumishi wa umma
kuacha tabia ya kuwashirikisha watoto katika kufanikisha vitendo vya
uvunjaji wa sheria, kwa kuwa kuendelea kufanya Hivyo kutapelekea kujenga
jamii ya kihalifu kutokana na vijana kuiga tabia Za kihalifu
zinazoonyeshwa kwao na wazazi.
IMETOLEWA NA
HOLLE J. MAKUNGU
MKUU WA TAKUKURU(M)MARA
25 APRILL 2016.
No comments:
Post a Comment