Monday, 25 April 2016

CAG amekabidhi Ripoti ya Ukaguzi wa Fedha 2016/2017 Bungeni leo


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad amekabidhi ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 bungeni leo mjini Dodoma ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la Bajeti ya mwaka 2016/2017.

Katika Ripoti yake, CAG ametoa Mapendekezo kadhaa ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi ili kuboresha Matumizi ya fedha za Serikali kwa Malengo Yanayokusudiwa.

Miongoni mwa maeneo ambayo CAG ametoa mapendeklezo ni Ofisi ya Masjili wa Vyama vya Siasa nchini ifuatilie suala la Uwasilishaji wa Taarifa Za fedha kwa wakati kulingana na Matakwa ya sheria.

Hatua hiyo ya CAG inafuatia ukaguzi uliofanywa kwenye vyama vya siasa Nchini vyenye usajili wa kudumu ambavyo jumla yao ni vyama 22.

Prof. Assad alisema kuwa kati ya vyama hivyo vyenye usajili wa kudumu, ni Chama kimoja ndicho kilichowasilisha hesabu zake kwa kipindi cha miezi Sita kuanzia Januari hadi Juni 2015 ambacho ni Chama cha Wananchi (CUF).

Vyama vingine 21 havikuwasilisha vitabu vya hesabu kwa ajili ya ukaguzi kinyume cha kifungu Na. 14 cha Sheria ya vyama vya siasa Na. 5 ya mwaka 1992.
 
4. Ripoti ya Jumla ya Miradi ya Maendeleo 2014/2015

No comments:

Post a Comment