Mkuu wa Wilaya Ally Hapi Kinondoni ina Watumishi Hewa 89
Na Mwamvita Mtanda
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi
amesema idadi ya Watumishi Hewa katika Wilaya Hiyo, imeongezeka hadi
kufikia 89 wakiwa wamesababisha hasara ya zaidi ya Sh Bilioni Moja.Aidha,
Hapi amebaini uwepo wa watumishi vivuli 81 katika kada ya ualimu na
hivyo Kutoa Siku Saba kwa Maofisa Utumishi wa wilaya hiyo, kuhakiki
watumishi vivuli ili kubaini idadi yao na Hasara Waliyosababisha.
Hapi aliyasema hayo wakati akizungumza
na Waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, na kueleza
kuwa awali wakati akiingia katika ofisi yake wiki iliyopita alikuta kuna
watumishi hewa 34 waliokuwa wamesababisha hasara ya Sh milioni 512.
Alisema baada ya kufanya uhakiki zaidi
walibainika watumishi hewa wengine 55 Walioisababishia Serikali Hasara
ya Sh milioni 619 na hivyo kufanya jumla ya hasara kuwa Sh Bilioni 1.
“Bado uhakiki wa kina Unaendelea ili
kuhakikisha tunamaliza hili tatizo la watumishi hewa katika Wilaya ya
Kinondoni, awali walikuwa 34 lakini sasa wameongezeka 55 na kufikia 89,” Alisema Hapi.
Akifafanua kuhusu Watumishi vivuli,
Hapi alisema Watumishi hao ni wale ambao Walihamishwa bila kufuata
taratibu na hivyo kuendelea kupokea mshahara wa kazi yake ya Awali
badala ya kazi yake mpya.
No comments:
Post a Comment