Na Kalonga Kasati
Kumekuwa na imani potofu kwa wanawake kwamba Hawawezi kumwambia ukweli Mwanaume anampenda Kwanza Mpaka Mwanaume aanze lakini ukweli usiopingika ni Kwamba wao pia Hupendi na Mara nyingi wao Wakianza kupenda Hupenda kweli kufikia Stage Hata ya kuhisi kuumwa. Hizi ni dalili za Mwanamke anaekupenda ila anagoma kukwambia tu.
Hufanya mambo ambayo yatamfanya kuona kama Unampenda na kumthamini au la mfano wa Mambo hayo ni kama kujifanya anaumwa na kauangalia Respond yako kwake ni kiasi gani Unamjali na kiasi gani Utahangaika kwa ajili yake.
Kucheka kwa Nguvu Hata kwa kitu kisicho chekesha Endapo Wewe Umezungumza. Mara Nyingi Ataonesha Uso wa furaha Hata kama si furaha ya kweli
Hujisikia wivu anapokuona na Wasichana Wengine. Ukiwa unachart nao na Ukiwaita Majina Ya kimahaba. Hapendi na hupenda yale afanyiwe Yeye tu Hata kama Sio Mpenzi wako.
Anakumbuka siku zako Muhimu. Hukumbuka kama Vile siku yako ya kuzaliwa hatoweza kuisahau kufanya ipite Bila kukutakia heri ya Siku ya kuzaliwa kama sivyo Ukifaulu Mtihani Au chochote katika Maisha yako atakuwa Mbele kukupongeza.
Eye contact hupendelea sana kukuangalia machoni Muda Wote ambao Mtakuwa Mkizungumza pamoja akidhani kuwa utamuelewa ni kiasi Gani anakupenda kupitia vile Anavyokuangalia. Ila Wengine Huona aibu kuwatazama Wavulana Wanaowapenda hivyo Huweka Jicho la wizi na kukuvizia.
Hupenda kukaa muda mwingi na wewe. Hawezi kupoteza Hata Sekunde Ukimuhitaji kwa Mazungumzo. Anajisikia furaha kukaa na Wewe Muda Mrefu bila kuchoka. Anaweza akaacha Kila kitu anachokifanya ili ajumuike na Wewe na akikaa na Wewe hupendelea Sana Mwanzoni Kukujua Wewe Zaidi na Hukujengea Mazingira ya Wewe Uwemuwazi ili Umwambie Mengi kuhusu Wewe na pia akiwa na Wewe atakuwa Muwazi zaidi Hadi Mavazi aliyovaa Hupenda Sana kujua Yako na kukuambia yake na Hupenda kujua ni Mavazi Gani Yeye akivaa Anakuvutia zaidi Na atajitahidi kuwa anavaa ya style hiyo kukufurahisha.
Kama Msichana anakupenda yupo Tayari kusacrifice. Ni kitu ambacho Hakuna mtu ambaye Anaweza akafanya kwa Mtu Mwingine. Utamuona Vipi huyo Msichana alivyo kwako na kwa Wengine. Yaani yupo Tayari akose lakini Wewe Upate na kwa Mwingine anaweza Akamwambia Hana alichoombwa lakini akakupa Wewe kama Pesa na vitu vingine.
Mikwaruzano ikitokea katika Urafiki wenu Hayupo tayari kukupoteza kabla hajakwambia Nakupenda.Kwa kuwa anakupenda endapo ikitokea mikwaruzano Basi atafanya Juu chini Kuyaweka Mambo sawa ili asikukose.
Mwanamke anaekupenda hupenda kujua Mengi sana kuhusu Wewe na hapo inamsaidia kukununulia Zawadi za Mitego kama Boxer , na Mara nyingi Hupenda Rangi Nyeupe, au kukununulia perfume , aSbuni ya kuoge ya Manukato,soksi, vest, bukta, Saa,raba, t-shirt. Na kama Mkitoka Wote Mkaenda Shopping ataakutega kwa kukuonyesha Vitu na Wewe Ukionekana Umependa kitu Hatonunua siku hiyo ila atanunua iSku inayofuata na kukuletea kama suprise.
Mwanamke anaekupenda ili akujue zaidi Hupendelea msosi mle Sehemu Mmoja na kama ikitokea Mwanaume Hawezi kuhama Sehemu anayokula Mwanamke Yupo Radhi kubadili na kumfuata Mwanaume Hata kama Sehemu hiyo yeye Haipendi na kama Unakula kwako Basi Atakutega na kuja kupika kwako ili Mle na atakuwa anapenda Kununua vitu vya kupika ili tu Akutekena Uone Upendo wake.
Ukiona Dalili kama Hizi Mwanaume Tafadhali Fanya Mpango wa kumweka ndani (oa) Mwanamke huyo kabla ujachelewa alafu Ukaja kuangukia kwa wale Wanawake Wenye sifa ya Mbaya
No comments:
Post a Comment