Na Tabu Mullah
Mwanafunzi
wa Mwaka wa Pili katika Chuo Kikuu cha Elimu (Duce), jijini Dar es
Salaam, Bertha Mwarabu (23), ameuawa na Mwanafunzi mwenzake kwa kuchomwa
kisu kwenye titi na Tumboni kwa kinachodaiwa ni kutokana na Wivu wa
mapenzi.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye,
tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika hosteli za Chuo hicho
zilizopo Mabibo, jijini Dar es Salaam.
Kamanda
Kalunguyeye amemtaja mtuhumiwa wa mauaji hayo kuwa ni Masamba Musiba
(27) ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo hicho,
ambacho ni sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Amesema
mauaji hayo yalitokea juzi saa 3:45 usiku baada ya Musiba kuingia
chumbani kwa Marehemu ambaye inadaiwa alikuwa Mpenzi wake Na kuanza
kumshambulia kwa kisu.
Ameongeza
kuwa Baada ya marehemu kuanza kushambuliwa, alipiga kelele kuomba
msaada na ndipo wanafunzi wenzake walipokwenda na kumkamata Mtuhumiwa
wakati akijaribu kukimbia.
Amesema kelele za Marehemu, ndizo Zilizowashtua wanafunzi wenzake.
Kamanda Kalunguyeye alifafanua kuwa Marehemu alikimbizwa Hospitali kupatiwa Matibabu lakini alifia njiani.
Mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa Mahojiano zaidi na mwili wa Marehemu Umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
Kwa
upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa
Rwekaza Mukandala, amesema tukio la Mauaji hayo ni la kwanza kutokea
chuoni hapo.
Profesa
Mukandala alisema Tangu aanze kufanya kazi chuoni hapo kwa Miaka mingi, Hajawahi kushuhudia Tukio la namna hiyo na kuongeza kuwa Amesikitika
kwa kuondokewa na Mwananfunzi huyo.
No comments:
Post a Comment