Ijue Timu ambayo itavaana na Yanga fc Katika Klabu Bingwa Afrika
Na Mwamvita Mtanda
Grupo
Desportivo Sagrada Esperança, kwa ufupi inajulikana kama Sagrada
Esperança au GD Esperança. Inatoka katika mji wa Dundo, ulioko jimbo la
Lunda Norte, Kaskazini ambako imeanzishwa Desemba 22, mwaka 1976.
Inaaminika kuwa asili ya jina hilo imetokana na shairi la la Rais wa
kwanza wan nchi hiyo Agostinho Neto lililojulikana kama Sagrada
Esperança Ikimaanisha (Sacred Hope) au tumaini lenye utakaso.
Timu hii ilianzishwa na kampuni ya madini ya Almas ambayo kwa sasa
inafahamika kwa jina la Endiama ambayo kwa sasa ndiyo mdhamini mkuu wa
klabu hiyo Kama ilivyo ilivyo Mwadui FC kwa hapa Tanzania.
Kombe lake la kwanza tangu kuanzishwa ililipata mwaka 1988, ikiwa ni
Angolan Cup ambalo ni kama ilivyo kombe la FA nchini England au Kombe
la Shirikisho kwa Tanzania.
Mwaka 2005 iliweza kubeba ndoo ya ligi kuu nchini humo kwa mara ya
kwanza nay a mwisho na katika mwaka huo iklishiriki michuano ya klabu
bingwa barani Afrika na kutolewa na Asec Abidjan ya Ivory Coast katika
hatua ya 16 bora.
Ina uwanja wake ambao ulizinduliwa mwaka 2008, unaitwa Estádio
Sagrada Esperança katika mji wa Dundo una uwezo wa kubeba watu 8000.
Timu hii inashiriki ligi kuu ya Angola inayofahamika kwa jina la
Girabola na mwaka 2008 ilishuka daraja ilishiriki ligi daraja la kwanza
nchini humo na baadaye kurejea tena ligi kuu.
HISTORIA YAKE KATIKA MICHUANO YA AFRIKA
Michuano wa Klabu Bingwa Afrika imeshiriki mara 2 pekee, ambapo mwaka
2005 iliishia Raundi ya kwanza na mwaka 2006 ilitolewa mapema kabisa
katika hatua ya awali.
Katika michuano ya Shirikisho, mbali na mwaka huu, mwaka 1992
iliishia raundi ya 2 na Mwaka 1998 iliishia raundi ya kwanza, ambapo
katika mwaka huu, Yanga ilifika hatua ya Makundi.
Wakati ule bado kulikuwa na kombe la washindi ambako pia ilishiriki
mara 2, mwaka 1989 na mwaka 2000 na mara zote iliishia raundi ya 2.
KOCHA
Ina historia ya kukaa na kocha kwa mwezi mmoja pekee, ambapo mwaka jana,
ilimuajiri Kochas Frank Moniz mwezi machi na kumtimua mwezi April mwaka
huohuo, na baadaye ikamchukua Zoran Mackic ambaye alimaliza nayo msimu
ikiwa katika nafasi ya 10 ya Msimamo wa ligi.
MAFANIKIO YAKE NDANI YA ANGOLA
Imefanikiwa kutwaa taji la Girabola mara moja (2005) pamoja na Kombe la Angola (FA ya Angola) mara mbili mwaka 1988 na 1999.
No comments:
Post a Comment