Kaimu Mwenyekiti Mtendaji wa
kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na
Pan African Power Solutions (T) Limited Bwn. Joseph O. R. Makandege
(katikati), akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo
pichani) kuhusu taarifa ya upotoshaji iliyochapishwa na gazeti la
MwanaHALISI ikihusisha IPTL kutoa rushwa kwa viongozi waandamizi wa
ikulu na watendaji waandamizi wengine serikalini. Kulia ni Mkurugenzi wa
uendeshaji wa IPTL Bwn. Parthiban Chandrasakaran na kushoto ni msaidizi
wa mwenyekiti mtendaji Bwn. Rajiv Bhesania. Picha na mpiga picha wetu.
Makampuni ya kufua umeme ya
Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Pan Africa Power Solutions
(T) Limited (PAP), tumesononeshwa sana na taarifa iliyochapishwa na
gazeti la kila wiki la MwanaHALISI katika toleo namba 332 la tarehe 28 Machi 2016 lenye kichwa cha habari, “Siri za Kikwete, IPTL zafichuka ”; iliyoambatana na nukuu katika ukurasa wake wa mbele inayosomeka “…hadi ndani ya jumba jeupe (Ikulu kwenyewe), Singasinga alitembeza mlungula.
Taarifa hiyo iliyojaa uongo
pamoja na kashfa nzito ya rushwa kwa IPTL/PAP na kwa viongozi waandamizi
wa serikali ya awamu ya nne na wengine ambao bado wamo katika serikali
hii ya awamu ya tano, imediriki kudai kwa kunukuu maneno yafuatayo,….. “Sethi
alitoa rushwa kila mahali, ikiwamo Ikulu, ili kufanikisha mpango wake
huo….Alihonga kila mtu. Alitoa rushwa kwa kila aliyeona faili la Escrow.
Hadi maofisa wa Ikulu na viongozi waandamizi kutoka wizara ya
fedha……..hadi ndani ya jumba jeupe (Ikulu kwenyewe), Singasinga
alitembeza mlungula. Ni BoT pekee, ambako hakuhonga au kuombwa rushwa.”
Tungependa kukanusha taarifa hizi
za shutuma ya rushwa ambazo ni za uongo na uzushi mtupu wenye lengo la
kuichafua IPTL na wamiliki wake akiwemo Mwenyekiti Mtendaji, Bw.
Harbinder Singh Sethi. Taarifa hizi zisizo na chembe ya ukweli ndani
yake zinalenga kuchafua sifa ya Ikulu ambayo ni taasisi nyeti hapa
nchini kwa kuihusisha na upokeaji rushwa ambayo ni kosa la jinai kwa
mujibu wa katiba na sheria za nchi yetu.
Isitoshe taarifa hizi zimejaa
habari za uongo zilizobuniwa kwa nia na madhumuni maovu ya kuichafua
sifa za kampuni za IPTL/PAP na mwenyekiti wake Bw. Harbinder Singh Sethi
pamoja na kuwachonganisha dhidi ya wananchi wa Tanzania kwa kuwahadaa
na kuwaaminisha Watanzania kuwa IPTL/PAP inaendeshwa kwa misingi ya
rushwa na udanganyifu, hivyo basi haistahili kufanya biashara hapa
nchini.
Awali ya yote, tungependa
kuutarifu umma wa Watanzania kwamba tuhuma za rushwa ni tuhuma nzito na
wala siyo za kunyamaziwa kabisa. Rushwa ni moja kati ya makosa makubwa
ya kijinai ambayo vyombo vya dola vinatilia maanani sana. Hivyo basi,
kampuni ya IPTL/PAP haiwezi kukaa kimya wakati tuhuma kama hizi
zikiendelea kuchapishwa dhidi yake, huku ikiwahusisha viongozi
waandamizi wa serikali, bila ya gazeti husika pamoja na mwandishi wa
taarifa hizo kutoa udhibitisho wowote wa tuhuma hizo.
IPTL/PAP tunaamini kwamba
taratibu zote za kukabidhiwa kampuni ya IPTL (ikiwemo mali na madeni
halali) zilifuatwa. Tunaamini katika utawala wa sheria ambayo
inazingatia haki za kila mtu. Hivyo basi, haitakuwa busara kuendelea
kunyamazia vitendo vya kiovu vya kuichafua kampuni yetu vinavyofanywa na
baadhi ya vyombo vya habari kwa kisingizio cha “uhuru wa kutoa maoni” au “uhuru wa vyombo vya habari”. Kama
vyombo vya habari walivyo na uhuru wao, vivyo hivyo IPTL/PAP kama
kampuni ina uhuru wa kufanya shughuli zake kwa mujibu wa sheria za nchi
bila ya kubughudhiwa. Kwa kutuhumu IPTL/PAP au viongozi wake kutoa
rushwa, bila kuthibitisha, ni kuihujumu kampuni ili isiweze kutekeleza
majukumu yake ya kuchangia ukuwaji wa uchumi wa nchi yetu.
Joseph O. R. Makandege (ADVOCATE)
(Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria)
KAIMU MWENYEKITI MTENDAJI
Independent Power Tanzania Limited / Pan African Power Solutions (T) Limited.
(Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria)
KAIMU MWENYEKITI MTENDAJI
Independent Power Tanzania Limited / Pan African Power Solutions (T) Limited.
CCM Yajizatiti Kuwapatia Bima Ya Afya Watumishi Wake.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM, Rajabu Luhwavi akizungumza na viongozi na watumishi
wa CCM katika kikao chake maalum cha kuzungumza na wafanyakazi wa mkoa
wa Njombe kilichofanyika mjini Njombe. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoawa
Ruvuma Verena Shumbusho na kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Njombe Osea
Mbagike.
Na Kalonga Kasati
Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kimesema, kina mpango wa kuhakikisha kila mtumishi wake Anapatiwa huduma
ya Bima ya Afya ikiwa ni moja ya hatua ya kuboresha maisha ya watumishi
hao.
Kimesema kupitia mpango huo, kila mtumishi hadi wa ngazi za chini ataweza kupata matibabu yeye na familia yake nchini kote.
Ahadi hiyo ilitokewa jana na Naibu
Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Bara, Rajab Luhwavi Alipokuwa akizungumza
na watumishi wa Chama na Jumuiya zake mkoani Njombe akiwa katika Ziara
ya kikazi ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero na changamoto
zinazowakabili watumishi wa Chama.
Luhwavi alisema kwa sasa Chama
kimo katika jitihada za kutafuta fedha kwa ajili ya kuwapatia Huduma
hiyo ya bima ya afya watumishi wake ili wapate huduma ya matibabu kwa
urahisi badala ya kutaabika kupata matibabu waanapougua jambo ambalo
linawapunguzia ufanisi katika kazi.
Alisema, kwa sasa watumishi wengi
wa Chama hawawezi kuingizwa katika mpango huo wa bima ya afya kutokana
na vima vya mishahara yao kutokidhi viwango vinavyotakiwa ili kusajiliwa
na Taasisi zinazotoa huduma hiyo ya bima ya afya hivyo chama
kikishapata fedha kitajazia mishara ya watumishi wenye vima vidogo ili
kila mmoja aweze kuwa na sifa za kusajiliwa.
Naibu Katibu Mkuu huyo, aliongeza
kwamba mpango huo utaanza kwa watumishi wa CCM na Baadaye itakwenda hadi
kwa watumishi wa Jumuiya za chama ili nao wanufaike na utaratibu huo wa
bima ya afya.
“Nduguzangu siyo kwamba changamoto
zote hatuna uwezo wa kuzitatu, kwa kweli baadhi ya Changamoto tuna
uwezo wa kuzitatua isipokuwa kinachotakiwa ni namna ya kujipanga tu,
hivyo nina uhakika jambo hili litawezekana”, alisema Luhwavi.
Katika hatua nyingine Chama cha
Mapinduzi kimesema ili kuhakikisha mpango wake wa kuendana na mabadiliko
ya sasa unafanikiwa haraka, kinasimamia viongozi wake kwa karibu zaidi
ili kuhakikisha kila mmoja anawajibika ipasavyo katika kuwahudumia
watumishi walio chini yake hasa wa ngazi za chini.
Akitoa kauli hiyo wakati
akizungumza na watumishi wa Chama mkoani Njombe, Luhwavi alisema,
alisema ni lazima chama kiwasimamie viongozi wake kwa makini kwa sababu
viongozi kutohudumia kwa haraka na kwa uadilifu mkubwa wafanyakazi ni
miongoni mwa vikwanzo Vinavyoweza kukwamisha utekelezaji wa haraka lengo
hilo la Chama kwendana na mabadiliko ya sasa.
“Tunajua wapo baadhi ya viongozi
wa Chama chetu ambao bado wanafanyakazi zao kwa mtindo Wa kimangimeza
ikiwa ni pamoja na kutotoa ushirikiano watumishi walio chini yao
wanapohitaji Ufumbuzi wa matatizo au changamoto zinazokuwa zinawakabili
kwa namna mbalimbali”, alisema Luhwavi.
Alisema, imefika wakati sasa
viongozi wa Chama kuacha tabia ya baadhi yao kufanya kazi kwa Mazoea
badala yake wajikite katika kushirikiana na wananchi kwa karibu katika
kufanyakazi za kijamii kama ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu,
zahanati na miraji ya maji.
Makamu Wa Rais Afunga Maadhimisho Miaka 50 Ya Sayansi Chuo Kikuu UDSM
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akihutubia Viongozi na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam wakati
wa ufungaji wa maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya kitivo cha Sayansi
cha Chuo Kikuu cha Dar es salaam yaliyoadhimishwa leo April 01,2016 Chuo
kikuu Mlimani.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akimkabidhi zawadi maalum Atibele Biyamungu mshindi wa kwanza kwenye
Shindano la kuandika ESE katika maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya
kitivo cha Sayansi cha Chuo Kikuu cha Dar es salaam yaliyoadhimishwa leo
April 01,2016 Chuo kikuu Mlimani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan, akimkabidhi cheti Lulu Kaaya mmoja kati ya washiriki wa
mashindano ya aina mbalimbali ya maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya
kitivo cha Sayansi cha Chuo Kikuu cha Dar es salaam yaliyoadhimishwa leo
April 01,2016 Chuo kikuu Mlimani.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akipata maelezo juu ya utendenezajia wa sabuni na bidhaa za aina
mbalimbali alipotembelea maonesho ya maadhimisho ya sherehe za miaka 50
ya kitivo cha Sayansi cha Chuo Kikuu cha Dar es salaam yaliyoadhimishwa
leo April 01,2016 Chuo kikuu Mlimani.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akipata maelezo juu Ya utendenezajia wa sabuni na bidhaa za aina
mbalimbali alipotembelea maonesho ya maadhimisho ya sherehe za miaka 50
ya kitivo cha Sayansi cha Chuo Kikuu cha Dar es salaam yaliyoadhimishwa
leo April 01,2016 Chuo kikuu Mlimani.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
katikati akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi na wanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Dar es salaa wakati wa ufungaji wa Maadhimisho ya sherehe za
miaka 50 ya kitivo cha Sayansi cha Chuo Kikuu cha Dar es salaam
yaliyoadhimishwa leo April 01,2016 Chuo kikuu Mlimani.
Picha na OMR
No comments:
Post a Comment