Makamu
wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali
Iddi akifungua kongamano la kujadili Fursa za Uwekezaji kati ya Tanzania
na Urusi lililofanyika jana jijini Dar es salaam ambalo limewakutanisha
wafanyabiashara mbalimbali wa Mataifa hayo mawili.
Waziri
wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage Akifafanua kwa
waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu faida za ushirikiano
wa kibiashara kati ya Tanzania na Urusi Utakaochangia maendeleo katika
sekta za Kilimo, Usafirishaji na Nishati hapa nchini.
Waziri
wa Viwanda na Biashara wa Urusi Mhe. Denis Manturov Akizungumza kwenye
kongamano la kujadili fursa za Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi
lililofanyika jana Jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya washiriki wa kongamano la kujadili fursa za Uwekezaji kati ya
Tanzania na urusi wakifuatilia mada wakati wa kongamano hilo Jijini
Dar es salaam.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali
Iddi (kushoto) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania Bw. Reginald Mengi jana Jijini Dar es salaam mara
baada ya kufungua kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali
Iddi (wanne kutoka kushoto) akiwa na Wawakilishi wa Serikali ya Urusi,
anayefuata ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Charles Mwijage
akifuatiwa na Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar Mhe. Amina Salum
No comments:
Post a Comment