Wanahabari Wanavyominywa Wasihabarishe Jamii na Watawala
Jumuiya ya Maripota Wasio na Mipaka
(RSF) imewakosoa viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa
kuwakandamiza waandishi habari.
Jumuiya hiyo imesema uhuru wa wanahabari
nchini humo unakandamizwa kwa lengo la kuwanyamazisha, kutokana na
Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika huku Rais Joseph Kabila akitazamiwa
kugombea kwa mara nyingine kiti hicho.
Jumuiya hiyo imesema waandishi wa habari
wanakabiliwa na vitisho vya kuuawa, kutiwa Nguvuni kwa sababu za
kisiasa ikiwemo kupigwa na vyombo vya dola kwa sababu ya kupinga Jaribio
la Rais Kabila kutaka kugombea kwa mara nyingine kiti hicho mara ya
tatu mfululizo.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inashika nafasi ya 158 kati ya nchi 180 kwenye orodha Uhuru wa vyombo vya habari duniani.
No comments:
Post a Comment