Sunday, 24 April 2016

Obama:ni Makosa Makubwa Kuwatuma Wanajeshi Kumpindua Rais Assad wa Syria

Rais Barack Obama amesema kuwa, itakuwa ni makosa makubwa kwa mataifa ya Magharibi kutuma majeshi yake hadi nchini Syria ili kumuondoa madarakani rais wa Syria Bashar Al-Assad.

Akizungumza na BBC, Obama amesema itakuwa ni makosa makubwa kuwatuma wanajeshi wa nchi kavu nchini Syria kumpindua rais Assad kwa sababu hilo pekee halitasuluhusiha Matatizo ya Syria.

Rais huyo wa Marekani amerejelea maoni yake ya awali kuwa haina maana kwa makundi ya Waasi kama vile Islamic State ndani ya Syria, kuendelea na makabiliano huku akisema kuwa Jeshi la taifa hilo pekee lafaa kukomesha mapigano nchini humo.

Ameongeza kusema hii itakuwa vigumu mno huku akiongeza kusema kuwa ni muhimu kuendelea kushambulia ngome za Islamic State ndani ya Syria kwa pamoja na kuzidisha Juhudi za kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ya muda mrefu nchini humo.



Obama amesema itakuwa ni makosa makubwa kuwatuma wanajeshi wa nchi kavu Nchini Syria kumpindua Rais Assad kwa sababu hilo pekee halitasuluhusiha Matatizo ya kisiasa ya Syria.
Katika mahojiano ya kina, Bw Obama amesisitiza hitaji lake kuwa matatizo ya kimataifa inahitaji uwajibikaji wa muda baada ya muda.

Obama anasema kuwa itakuwa vigumu kwa majeshi yake ama hata muungano unaongozwa na Marekani kuitokomeza kabisa Islamic State katika kipindi cha miezi 9 za uongozi wake.
Cha mno anasema ni kudidimiza maeneo inayokalia IS na kushambulia ngome zake.

Aidha Obama anasema mashambulizi yatalenga haswa kukatiza msururu wa wapiganaji wanaoenda ulaya na kusababisha maafa makubwa.

No comments:

Post a Comment