Historia ya Uchaguzi wa Mwaka Jana Hautafutika Vichwani Mwa Watanzania Walio Wengi
Na Kalonga Kasati
Katika historia ya Siasa za Tanzania
mwaka 2015 Umeweka Historia katika Uchaguzi Mkuu Uliofanyika Oktoka Ukihusisha Wabunge, Madiwani na Rais.
Mchuano Ulikuwa Mkali Baada ya Vyama vya
Upinzani kuungana na kumsimamisha Mgombea Mmoja wa Urais kupitia Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, Chini ya Mwavuli
wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) huku mgombea wa Chama Tawala
(CCM) Dk. John Pombe Magufuli, akipata Upinzani Mkali Baada ya Wapinzani
kuunganisha Nguvu na Kuwa kitu kimoja.
Nchini Marekani Mtia nia wa Chama cha
Republican, Donald Trump amekumbana na Upinzani wa Baada ya Viongozi Wanaowania Nafasi Moja kutangaza kuungana ili kukabiliana Na Mgombea
huyo.
Seneta wa Jimbo la Texas, Ted Cruz na
Gavana wa Ohio, John Kasich Wametangaza Rasmi kuungana ili kumuwekea
vikwazo Trump ambaye anakubalika katika Majimbo Mengi hadi Sasa, huku
akikabiliwa na changamoto ya kupata Wajumbe Wanaohitajika kumpa Ushindi
kabla ya Kongamano Kuu la Kitaifa la Chama Julai mwaka huu.
No comments:
Post a Comment