Je Tunaenzi Muungano Uliowekwa na Waasisi Wetu Hayati Karume na Mwalimu Nyerere?
“Kuifufua
Tanganyika ni kuiua Tanzania Sikubaliani kabisa na Suala hili, kwa Sifa
tu na Uroho Wa Madaraka na Huku Wakishabikiwa na Mazuzu kuna Watu Watafanya kila hila Zanzibar ijitenge na Tanganyika. Nasema Dhambi hii
ya Utengano na iwatafune, NaombaMungu Anisamehe, hakika Dhambi ya Utengano na iwatafute Hawatabaki salama”.
Maneno haya aliyasema Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo Yamesaidia kudumisha na kuuenzi
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hadi leo hii Umetimiza miaka 52 tangu
kuasisiwa kwake na Abeid Amani Karume pamoja na Mwalimu Nyerere
Kwa kutambua hilo Mwenyekiti Taifa wa
Chama Allience fo Democratic Party (ADC), Said Miraji anasema ili kuenzi
na kudumisha kile Waasisi wa Muungano Walichotuachia ipo haja Ya
kuepusha siasa katika Muungano kwa kuwapa uhuru Watanganyika na
Wazanzibari kujadili Na kuamua kile wanachokitaka.
Anasema Muungano Haulindwi kwa Mtutu wa Bunduki kama ilivyosasa na kupelekea kubaguana kwa Misingi ya Udini,
ukabila na kiitikadi bali Watanzania Wauenzi na kuuishi Sambamba na kuwa
na Sera ya Watanganyika na Wazanzibari itakayohakikisha Chama chochote
cha Siasa kinapoingia Madarakani Kinaheshimu na kuulinda Muungano.Pamoja na Mambo Mengine pia Kiongozi
huyo amezungumzia Changamoto na faida Zitokanazo Na Muungano; Unaweza
kumsikiliza hapa Chini akifafanua
No comments:
Post a Comment