Mahakama
ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam, leo imefuta Shtaka la
utakatishaji fedha (money laundering) lililokuwa likimkabili Kamishna
Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya sambamba
na waliokuwa wafanyakazi wa Benki ya StanBic Tanzania, Sioi Sumari na
Shose Sinare.
Awali watatu hao walikuwa wamenyimwa dhamana. Kutokana na uamuzi Huo, mawakili wao sasa wanaweza kuwaombea dhamana.
Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), iliwafikisha Mahakamani
watatu hao April 1, kwa kisa la:- Kula njama na kujipatia kwa Udanganyifu kinyume na kifungu Na. 384 cha Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E.
2002) ; Kughushi kinyume na kifungu Na. 333,335 (a) na 337 cha Kanuni
ya Adhabu (Cap 16 R.E 2002) ; Utakatishaji wa fedha haramu kinyume na
kifungu Na. 12 (a) 13 (a) cha Sheria ya ya Utakatishaji fedha Na. 12 ya
Mwaka 2006 ‘Anti- Money Laundering Act’.
Watuhumiwa
hao walidaiwa kufanikiwa kujipatia fedha kwa njia ya kughushi Dola
milioni 6, kama malipo ya kufanikisha serikali ya Tanzania kupata Mkopo
wa dola milioni 550 kutoka Benki ya Stanbic ya Jijini London mkopo Ambao
ulipitia benki ya Stanbic tawi la Tanzania.
No comments:
Post a Comment