Aliyekuwa Mfanyakazi wa TRA Kitengo cha Uhasibu alijilipa Mishahara Mara17
Mfayakazi wa Mamlaka ya Mapato Nchini
aliyetuhumiwa na Rais John Magufuli mwezi Uliopita kujilipa Mishahara 17
ya watumishi hewa, hayupo kwenye ajira ya TRA kwa siku Nyingi
zilizopita, imefahamika.
Habari kutoka ndani ya Mamlaka hiyo
zimesema kuwa mfanyakazi huyo alikuwa ni wa Idara ya Uhasibu ya TRA
lakini alishafukuzwa kazi siku nyingi zilizopita.
Chanzo cha kuaminika kutoka Makao Makuu
ya TRA kimeiambia Nipashe kuwa mfanyakazi huyo alifukuzwa kazi baada ya
kubainika kujilipa mishahara hiyo katika akaunti yake.
Chanzo chetu cha habari ambacho
hakikupenda kutajwa jina kwa sababu si msemaji wa Mamlaka, kilisema
mfanyakazi huyo baada ya kuhojiwa alikiri kujilipa mishahara hiyo.
“Huyu mfanyakazi alikuwa Idara ya
Uhasibu… ni kweli alijilipa mishahara hiyo na baada ya kuhojiwa alikiri
ndipo tukamfukuza kazi na kumpeleka mahakamani,” chanzo hicho kilieleza.
Rais Magufuli alimfichua mfanyakazi
huyo hivi karibuni akiwa nyumbani kwake katika Kijiji Cha Mlimani,
Wilaya ya Chato mkoani Geita, alipokuwa alihutubia kwa mara ya kwanza Tangu achaguliwe kuwa Rais Oktoba 25, mwaka jana.
No comments:
Post a Comment