Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimia wananchi wa Mkoa wa Katavi
alipowasili katika mkoa huo jana kukutana na wadau wa sekta Anazozisimamia pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa mkoa
wa Katavi na kutembelea mitambo ya kurushia matangazo ya TBC. Kushoto ni
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Mhe. Paza Mwamlima.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na watendaji wa Mkoa wa
Katavi alipowasili katika ofisi za mkoa huo na badae kukutana na wadau
wa sekta anazozisimamia pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari
wa mkoa wa Katavi na kutembelea mitambo ya kurushia matangazo ya TBC.
Wadau wa sekta za Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mkoa wa Katavi wakimsikiliza Waziri mwenye
dhamana na sekta hizo Mhe. Nape Nnauye (hayupo pichani) alipofanya kikao Nao jana mkoani hapo na kuahidi kutatua baadhi ya kero zinazowakabili.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akikagua iPad kabla ya kumkabidhi Mkuu
wa wilaya ya Mpanda Mhe. Paza Mwamlima iPad nne kwa ajili ya maafisa
habari waliopo katika Mkoa wa Katavi na Wilaya zake jana mkoani Katavi.
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Mhe.
Paza Mwamlima akifurahi na kumpa mkono Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo baada ya kupokea iPad nne kwa ajili ya maafisa habari
waliopo katika Mkoa wa Katavi na Wilaya zake jana mkoani Katavi.
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo, Katavi
Na: Mwamvita Mtanda
Taasisi za serikali zimetakiwa
kuwashirikisha maafisa habari waliopo katika taasisi zao katika vikao
vya maamuzi ili waweze kua na taarifa na kufahamu maamuzi ya michakato
inayoendelea hivyo kupata nguvu na uelewa mzuri wa kwenda kueleza umma
pale wanapotakiwa kutolea ufafanuzi.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye wakati wa ziara
yake jana katika Mkoa wa Katavi kukutana na wadau wa sekta
anazozisimamia pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa Mkoa
huo na kutembelea mitambo ya kurushia matangazo ya TBC.
Mhe. Nnauye amesema kuwa maafisa
habari katika taasisi za serikali wamekuwa wakinyimwa nguvu ya kushiriki
katika vikao vya taasisi hivyo kushindwa kutolea maamuzi masuala
mbalimbali pale wanapohitajika katika vyombo vya habari.
Aidha Mhe. Nnauye amewataka
waandishi wa habari kufanya kazi kwa kufuata sheria kanuni na taratibu
kwani serikali inawajali na kuwathamini kwa kazi nzuri wanayoifanya ya
kuelimisha jamii.
“Mswada wa sheria ya huduma wa
vyombo vya habari umelinda maslahi ya waandishi wa habari na Sheria hii
imebana vigezo ambapo kama itapita itasaidia kupambana na utitiri wa
vyuo visivyokuwa na sifa pamoja na changamoto zingine zinazoikabili
sekta hii” amesema Mhe. Nnauye.
Aidha Mhe. Nnauye amewaomba watu
wa TCRA kusimamia vizuri maudhui ya Radio na Television kwa kuwa wakali
na kuacha kucheka na watu ambao wanaweza kutumia vibaya mabadiliko ya
sayansi na teknolojia kuwaga jamii yetu kidini, kikabila, kikanda na
rangi kwa kufanya matangazo ya kuligawa taifa letu.
Naye mwandishi wa habari kutoka
Clous FM Bw. Ezron Mahanga ameiomba serikali kuendelea kupambana kulinda
maslahi ya waandishi wa habari kwa kuwasimamia kwa karibu ili wamiliki
wa vyombo vya habari waache kuwatumia kwa maslahi yao binasfi bila
kujali utu wa waandishi wa habari wanaofanya kazi katika mazingira
magumu.
TAMKO LA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KULAANI KUBAKWA NA KULAWITIWA KWA MTOTO KATIKA MANISPAA YA MIKINDANI, MKOANI MTWARA
Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesikitishwa na kukemea vikali tukio la
mzazi kumbaka na kumlawiti mtoto wake wa kufikia mwenye umri wa mwaka
mmoja na nusu, kitendo kilichofanywa na John Donald (35) mkazi wa
Kiyangu, Manispaa ya Mikindani mkoani Mtwara.
Tukio hili la kubaka na
kulawitiwa ni ukatili wa hali ya juu dhidi ya mtoto maana husababisha
maumivu makali ikiwa ni pamoja na kumdhuru mtoto kimwili, kisaikolojia,
kijamii na kihisia. Aidha, vitendo hivi, vinaacha kovu la kudumu
kimwilini, kiakili, kimaadili, kijamii, ulemavu, maumivu, na wakati
mwingine husababisha kifo; jambo ambalo linahitaji ulinzi thabiti katika
kuhakikisha watoto wanaishi mazingira salama na rafiki.
Ukatili alilofanyiwa mtoto eneo
la Kinyangu, manispaa ya Mikindani, ni ukiukwaji mkubwa wa haki za mtoto
ambao huchangia kurudisha nyuma ustawi na maendeleo ya Mtoto na ni
kinyume cha Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009.
Wizara inatoa pongezi kwa Jeshi
la Polisi mkoani Mtwara kwa kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha mahakamani
ili hatua za kisheria zichukuliwe. Vile vile, Wizara inaipongeza
Mahakama ya Wilaya ya Ilala, mkoani Dar es salaam dhidi ya Omary hamisi
(25), mkazi wa Gongo la Mboto, Dar es salaam, ya kutumikia kifungo cha
maisha jela, baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka
tisa mwenye ulemavu wa kusikia na kuongea. Uamuzi huu ni kielelezo kuwa,
wananchi wakitoa ushahidi wa matukio ya ukatili dhidi ya watoto,
watuhumiwa watachukuliwa hatua kali ili kuwa fundisho kwa wananchi
wanaowanyanysa watoto.
Wizara inamwelekeza Afisa Ustawi
wa Jamii na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Mtwara kuwasiliana na
wadau wengine katika ngazi zote kuhakikisha mama na mtoto wanapata
huduma ya afya na ushauri na kufuatilia mwenendo wa shauri hili.
Imetolewa na
Erasto Ching’oro
Msemaji wa Wizara
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na WatotoSerikali yahaidi kuboresha usikivu wa shirika la utangazaji la taifa Mikoa ya pembezoni
: Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe.
Zelote Stephen (kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe.
Mathew Sedoyeka (kushoto) wakiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye baada ya kuwasili katika Mkoa wa
Rukwa jana kuzungumza na wadau wa sekta anazosimamia.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na viongozi wa CCM Mkoa wa
Rukwa jana wakati wa ziara yake mkoani humo kukutana na wadau wa sekta
anazozisimamia. Kushoto kwa Waziri ni Mwenyekiti wa CCM Rukwa Bw.
Hypolitus Matete
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Zelote
Stephen (kushoto) akuzungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Nnauye alipofika ofisini kwake wakati wa ziara ya
kukutana na wadau wa sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja
na kutoa vitendea kazi kwa maafisa mawasiliano jana Mkoani Rukwa.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizugumza na watendaji kutoka
Mkoa wa Rukwa pamoja na wadau wa kada za Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo alipokutana nao jana Mkoani hapo kujadili mambo mbalimbali
katika sekta hizo pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa mawasiliano.
Baadhi ya watendaji kutoka Mkoa
wa Rukwa pamoja na wadau wa kada za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) alipofanya ziara yake jana
Mkoani Rukwa kujadili mambo mbalimbali pamoja na kukagua ofisi za TBC
na kutoa vitendea kazi kwa Maafisa Mawasiliano wa Mkoa wa Rukwa.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiikagua iPad kabla ya
kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Zelote Stephen (kushoto) kwa ajili
ya kuboresha utendaji kazi kwa maafisa mawasiliano waliopo Mkoani hapo.
Mhe. Nnauye alikabidhi iPad tatu kwa Mkoa wa Rukwa jana baada ya
kufanya ziara fupi na kuonana na wadau wa sekta anazozisimamia
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi
Kimanta akitoa taarifa fupi kuhusu sekta za Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo kwa Waziri wa sekta hizo Mhe. Nape Moses Nnauye alipofanya
ziara Wilayani hapo jana Mkoani Rukwa.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza moja kwa moja
kupitia radio ya Wilaya NKasi FM alipofanya ziara katika radio hiyo
kuona mafanikio yaliyoletwa na Wilaya ya Nkasi kwa kuwa na radio ya
Wilaya.
Picha na: Genofeva Matemu- Maelezo, Rukwa
Kamati Ya Bunge Yatembelewa Wizara Ya Mambo Ya Ndani Ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akisalimiana na Mjumbe wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Kangi
Lugola, wakati Kamati hiyo ilipotembelea Makao Makuu ya Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi. Kushoto ni mjumbe mwingine wa kamati hiyo, Juliana
Shonza.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu,
akiongoza kikao wakati Kamati hiyo ilipokutana na Viongozi na Watendaji
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo Meja Jenerali Projest Rwegasira.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Viongozi Na Watendaji Wakuu
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakiwa katika mkutano Uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar
es Salaam wakati Kamati hiyo ilipotembelea Makao Makuu ya Wizara hiyo.
Katikati meza kuu ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Balozi Adadi Rajabu na
kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Wakiongozwa na Mwenyekiti wa
kamati hiyo, Balozi Adadi Rajabu (wa tatu kulia), wakikagua Mojawapo ya
samani za ofisi ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Balozi Simba Yahya, ambazo zimetengenezwa na Jeshi la Magereza,
wakati Kamati hiyo ilipotembelea Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba, akizungumza
wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,
ilipotembelea Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam kuona
shughuli Mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo. Wa kwanza kutoka
kushoto (waliokaa) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Meja Jenerali Projest Rwegasira na wa tatu ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Balozi Adadi Rajabu.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Uzalishaji Vitambulisho wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),
Alphonce Malibiche, akielekeza jinsi ya kutambua taarifa sahihi za
mwombaji wa kitambulisho cha Taifa kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (hawapo pichani), wakati Kamati
hiyo ilipotembelea Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati), akizungumza
na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama, Balozi Adadi Rajabu (kushoto) mara baada ya Kamati hiyo
kumaliza ziara yake katika Makao Makuu ya Wizara hiyo na Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (Nida). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Balozi Simba Yahya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, Akiagana na Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi
Adadi Rajabu (kushoto), mara baada ya Kamati hiyo kumaliza ziara yake
Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Balozi Simba Yahya.
No comments:
Post a Comment