Makamu wa Rais wa
Kenya William Ruto atafahamu leo iwapo kesi inayomkabili katika Mahakama
ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) itatupiliwa mbali.
Mwanahabari Joshua arap Sang, aliyeshtakiwa pamoja na Bw Ruto, pia atafahamu leo iwapo ana kesi ya kujibu.Bw Ruto anakabiliwa na mashtaka ya mauaji, kuhamisha watu kwa lazima na mateso yaliyotekelezwa wakati wa vita vya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Amekana mashtaka hayo na mawakili wake wanataka kesi hiyo itupiliwe mbali kutokana na ukosefu wa ushahidi.
Watu takriban 1,200 waliuawa wakati wa mapigano hayo.
Upande wa mashtaka umekabiliwa na changamoto kadha kwenye kesi hiyo dhidi yake.
Mwezi Februari, Majaji katika mahakama hiyo waliizuia afisi ya mwendesha mashtaka kutumia Ushahidi wa Mashahidi ambao tayari wamejiondoa.
Mashahidi kadha muhimu walibadilisha taarifa zao za ushahidi, jambo ambalo waendesha Mashtaka wanasema lilitokana na vitisho na kuhongwa.
Mawakili wa Bw Ruto wanasema anafaa kuondolewa kesi hiyo kwa sababu mashahidi wengi wa Upande wa mashtaka wamejiondoa au wakabadilisha taarifa zao asili za ushahidi.
- Ruto ashinda rufaa mahakama ya ICC
- Mashahidi wa Ruto katika ICC
- Bensouda:Sikabiliwi na shinikizo zozote
Msemaji mmoja wa ICC ameambia mwandishi wa BBC Anna Holligan mjini The Hague kwamba kuna mambo kadha ambayo yanaweza kutokea.
Majaji wanaweza kuondoa mashtaka yote Dhidi ya Bw Ruto, wanaweza kuutaka upande wa Mashtaka Ubadilishe mashtaka au wanaweza kukataa tetesi za upande wa mshtakiwa na kuamua kesi iendelee.
Mwaka 2014, Mwendesha Mashtaka aliondoa Mashtaka sawa Dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta Akisema Mashahidi walikuwa wametishiwa na kubadilisha Ushahidi wao.
Hatima ya kesi hiyo sasa inaonekana kutegemea iwapo mwendesha Mashtaka alithibitisha kwamba Ana Ushahidi wa kutosha wa kupinga msimamo wa upande wa mshtakiwa kwamba Hana kesi ya kujibu.
Suala la kutumiwa kwa Ushahidi wa Mashahidi Waliojiondoa Huongozwa na Kanuni 68 ya Mkataba Wa Roma, Uliounda Mahakama ya ICC.
Mawakili wa William Ruto walisema haikuwa haki kwa sheria hiyo kutumiwa kwenye kesi Dhidi yake kwani mabadiliko ya kuruhusu kutumiwa kwa ushahidi wa Mashahidi Waliojiondoa yalifanywa Baada ya kesi Dhidi yake na Mwanahabari Joshua arap Sang kuanza.
Jaji Judge Piotr Hofmanski aliamua kwamba Ushahidi wa Mashahidi Waliojiondoa ulitumiwa Bila kuwapa Mawakili wa Washtakiwa fursa ya kuwahoji Mashahidi hao.
Alisema haingekuwa haki kwa ushahidi huo kutumiwa Dhidi ya Washtakiwa.
Bw Sang, anadaiwa kutumia Vipindi vyake vya Redio kupanga Mashambulio baada ya Uchaguzi.
Baada ya majaji kuamua ushahidi wa mashahidi waliojiondoa haufai kutumiwa, Bw Sang Alisema Hiyo ilikuwa „hatua moja kuelekea kwa uhuru wetu”.
Bw Ruto na Bw Kenyatta Walikuwa kwenye Mirengo pinzani wakati wa Uchaguzi wa 2007 lakini Waliunda Muungano wa kisiasa na wakashinda Uchaguzi mkuu wa 2013.

No comments:
Post a Comment