Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura Akipokelewa na
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja Alipofanya Ziara katik ofisi za Baraza hilo leo jijini Dar es
Salaam.Kutoka kulia ni mjumbe wa BMT Bibi. Jenifer Mmasi Shang’a na
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge.
Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura Akizungumza na
wafanyakazi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) alipofanya Ziara katika
ofisi za Baraza hilo leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sana na Michezo Bibi. Nuru Halfani Mrisho Milao
akizungumza jambo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe.
Annastazia James Wambura (katika) katika ofisi za Baraza la Taifa la
Michezo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa BMT Mohamed
Kiganja.
Katibu Mkuu wa BMT Mohamed
Kiganja akifafanua jambo mbele ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (kushoto) alipofanya Ziara katika ofisi za Baraza hilo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Afisa Utumishi wa BMT Bw. Jacob Nduye na wapili kulia ni mjumbe wa BMT
Bibi. Jenifer Mmasi Shang’a.
Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura, Naibu Katibu
Mkuu na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge
wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja wakati wa
ziara yake katika ofisi za Baraza hilo lep jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura Akiwa katika
picha ya pamoja na wafanyakazi wa BMT leo jijini Dar.Kutoka kushoto
waliokaa Ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo na wa mwisho kulia
waliokaa ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed
Kiganja.
Na Kalonga Kasati
BMT yaagizwa kuongeza kasi ya
ufuatiliaji wa viwanja vya michezo vilivyovamiwa nakuvirejesha kwa jamii
kwa ajili ya matumizi ya michezo.
Agizo hilo limetolewa leo na na
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nuru Khalifani
Milao alipofanya ziara katika ofisi za Baraza hilo kwa ajili ya kujionea
hali ya utendaji katika baraza hilo.
Mhe. Wambura alisema kuwa
kumekuwa na changamoto ya maeneo mengi yaliyotengwa kwa Shughuli za
kijamii ikiwemo michezo kuvamiwa na watu na kufanya shughuli kinyume na
taratibu.
“Kama ilivyo katika Ilani ya
uchaguzi BMT mnawajibika kufuatilia maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili
ya shughuli za michezo fuatilieni kwa karibu kikiwemo na kile cha
Tandika ambacho tulikwisha anza nacho” Alisema Naibu Waziri.
Aidha Wambura alihimiza Bmt
kuhakikisha inahamasisha ushiriki wa wanawake katika Michezo kwa kuwa
michezo ipo kwa ajili ya wote na kuongeza kuwa mbali na mashindano
michezo pia utumika kujenga afya za mwanadamu.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja Alisema kuwa pamoja na
changamoto zilizopo watahakikisha wanapiga hatua katika kukuza Sekta ya
michezo kwani BMT ndiyo mkono pekee wenye dhamana ya kusimamia michezo
kisheria.
Hata hivyo alielezea changamoto
zinazowakabili katika kutekeleza majukumu yao kuwa ni kuwa ni ufinyu wa
bajeti, upungufu wa wafanyakazi na muingiliano wa Wizara mbili katika Utekelezaji katika ngazi ya Manispaa na Halmashauri Maafisa Michezo
wanawajibika chini ya Wizara ya TAMISEMI hivyo kuna haja ya kukaa pamoja
na kuangalia namna bora ya kushirikiana.
Mtaka Aula Shirikisho La Riadha La Kimataifa (IAAF)
SHIRIKISHO la Riadha la
Kimataifa (IAAF), limemteua Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT),
Anthony Mtaka, kuwa miongoni mwa wajumbe wanaounda kundi la ushauri Wa
mikakati ya mawasiliano ya shirikisho hilo.
Rais wa IAAAF ,Lord Sebastian Coe alitangaza uteuzi huo hivi
karibuni ambapo wajumbe Wengine ni Abrahamson Alan wa Marekani, Rodan
Joe Junior ,Sierra Calixto ,,Karamarinov Dobromir kutoka Bulgaria
na Rochdi Souad wa Ufaransa.
Akizungumza kuhusu uteuzi huo Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa mkoa
wa Simiyu, alisema Amepokea uteuzi huo kwa furaha kutokana na kuwa ni
nafasi ya juu ktk sekta maarufu ya michezo katika ngazi ya kimataifa.
“Nimefurahishwa na uteuzi huu hasa ukizingatia nimeteuliwa
nikiwa Rais wa shirikisho la Riadha mwenye umri mdogo kuliko wote kwa
sasa atakuwa na fursa ya kujifunza mambo mengi mazuri.”alisema Mtaka.
Alisema uteuzi huo ni faida kubwa kwa maendeleo ya michezo
katika taifa letu, hasa kipindi Hiki ambapo serikali ya awamu ya tano
inapoandaa mkakati wa kuiweka sekta ya michezo kuwa sehemu kubwa ya
ajira.
Mtaka alisema Tanzania itapata nafasi pana zaidi ya kuwakilishwa
katika mikutano Mikubwa Ya mchezo wa riadha duniani (Decision Making)
eneo ambalo linatoa fursa kubwa kwa Maandalizi ya mashindano makubwa
yajayo baada ya mashindano ya Olyimpiki yatakayofanyika katika jiji la
Rio de Jeneiro mwaka huu.
“Taifa litarajie uwakilishi
wenye tija, sababu mimi nimeteuliwa kati ya wajumbe nane ambao kila
mmoja wao anawakilisha eneo kubwa, hivyo kama nimepewa dhamana ya
kuiwakilisha Bara Zima la Africa, kwa vyovyote nitaweka maslahi ya nchi
yangu mbele bila kuathiri utendaji wa jukumu nililopewa.”alisema Mtaka.
“ Uteuzi wangu ni sifa kwa
taifa zima, sifa ambayo itafufua mtazamo mwema ulioonyeshwa na Wanariadha wakongwe walioiletea taifa sifa kama Filbert Bayi, Suleiman
Nyambui, Gidamis Shahanga, Juma Ikangaa bila kumsahau Mzee John Stephen
Akhwari aliyeshiriki Mexico City Games 1968.”aliongeza Mtaka.
Aidha Mtaka alisema uteuzi huo umeongeza hamasa ya kuwekeza
maradufu katika kambi ya Timu ya taifa ya riadha iliyopo katika hosteli
ya Chuo cha misitu cha FITI kilichopo West Kilimanjaro wilayani Siha na
Arusha.
No comments:
Post a Comment