Mkuu
wa Mkoa wa Geita Meja Generali Mstaafu Ezekiel Kyungu akishuhudia
mabati yaliyotolewa ma Mfuko wa Pensheni LAPF kwa ajili ya ujenzi wa
madarasa wilayani Geita ikiwa jitihada za Mfuko wa LAPF kuunga mkono
jitihada za Serikali kutoa elimu bure. Jumla ya mabati 300 yenye thamani
ya Shs. 7,000,000/= yalikabidhiwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Meja Generali Mstaafu Ezekiel Kyungu akikagua mabati
yaliyokabidhiwa kama msaada na mfuko wa Pensheni wa LAPF wilayani Geita,
kulia ni Meneja Masoko wa Mfuko wa LAPF Bw. James Mlowe wengine ni
maofisa kutoka wilaya ya Geita.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Meja Generali Mstaafu Ezekiel Kyungu akiteta jambo na
Meneja Masoko wa Mfuko wa Pensheni LAPF pamoja na mbalimbali wa Wilaya
ya Geita mara baada ya makabidhiano ya msaada wa mabati kwa ajili ya
ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita akitoa neno la shikrani kwa Mfuko wa Pensheni LAPF kwa
msaada wa mabati 300 yanayotosheleza kuezeka vyumba sita (6) vya
madarasa yanayoweza kuchukua wanafunzi 45 kwa kila chumba na hivyo
kupunguza tatizo la ukosefu wa mazingira bora ya kufundishia.
TCRA Waikabidhi leseni ya Biashara kampuni ya Agano Safi
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) imeikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi inayokuja
kuwekeza katika huduma za mfumo wa malipo mbalimbali kwa kutumia mtandao
‘malipo ya huduma anuai kwa njia ya kidigitali’ (Digital Payment
Services). Leseni hiyo imekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba kwa kampuni ya Agano Safi huku
akiikumbusha kufanya shughuli zake kwa kuzingatia vigezo na masharti ya
leseni.
Akipokea leseni hiyo, Mkurugenzi
wa Kampuni ya Agano Safi Iyaloo Ya Nangolo alisema anaishukuru TCRA kwa
kuwaamini na kuwakambidhi leseni ya kufanya biashara ya mfumo wa malipo
kwa njia ya mtandao, hivyo kampuni hiyo itahakikisha inafanya kazi kwa
ufanisi na kushirikiana na vyombo husika ikiwemo BoT ili kuhakikisha
jamii na taifa linanufaika na shughuli hizo.
Alisema kampuni hiyo inayoundwa
na Wanamibia kwa ushirikiano na baadhi ya Watanzania imejipanga kuja na
teknolojia ya kisasa katika mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao kwa
kushirikiana na kampuni ya malipo ya MobiPay iliyojijengea heshima ya
huduma zake katika nchi za Kusini mwa Afrika huku ikiwa na makao yake
nchini Namibia.
Hafla hiyo ya makabidhiano
imehudhuriwa pia na Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia
Samaria ambaye amepongeza Agano Safi kufanikiwa kufanya biashara hiyo
nchini Tanzania jambo ambalo linaongeza ushirikiano baina ya nchi hizo
huku zikibadilishana teknolojia kwa masuala mbalimbali na ubunifu
kibiashara.
Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria akizungumza katika hafla ya TCRA kuikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi leo jijini Dar es Salaam. |
Baadhi ya maofisa wa TCRA wakiwa katika hafla hiyo. |
Baadhi ya maofisa wa kampuni ya Agano Safi (kulia) wakiwa na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla hiyo. |
Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria akipeana mkono na Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa TCRA, Fortunata Mdachi mara baada ya zoezi la kukabidhiana leseni kukamilika. |
Mabondia Wanne Wapigwa Pini Akiwemo Thomas Mashali, Francis Miyeyesho,Nassib Ramadhani Na Ramadhani Shauli
Bondia Thomasi Mashali katikati
akisaini mkataba mbele ya katibu mkuu wa chama cha gumi za kulipwa PST
Anton Ruta kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa wa Dunia na Muiran
Sajjad Mehrabi utakaofanyika mei 14 katika uwanja wa ndani wa taifa
kushoto ni bondia Fransic Miyeyusho
Bondia Ramadhani Shauli akisani
mkataba wa kuzipiga na Salim Salim kutoka Malawi mei 14 katika uwanja wa
ndani wa Taifa kulia ni kocha wa bondia huyo Cristopher Mzazi |
Kiongozi wa PST Anton Ruta akitia saini mkataba wa bondia Nassibu Ramadhani kushoto
Bondia Nassibu Ramadhani
akisaini mkataba wa kuzipiga na bondia kutoka nje ya nchi mbele ya
katibu mkuu wa chama cha gumi za kulipwa PST Anton Ruta kulia na kocha
wa bondia huyo Cristopher Mzazi |
Bondia Fransic Miyeyusho ‘Chichi
Mawe’ kushoto akisaini mkataba wa kuzipiga na bondia kutoka nje ya nchi
siku ya Mei 14 katika uwanja wa ndani wa taifa kulia ni katibu mkuu wa
PST Anton Ruta katikati ni bondia Thomas Mashali
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA wanne ambao wanatamba nchini Tanzania wamepigwa pini na promota wa Mchezo wa masumbwi nchini Ally Mwanzoa
Baada ya kuwasainisha mikataba
mabondia hao kwa ajili ya kucheza mpambano wa kimataifa Utakaofanika
jijini Dar es salaam Mei 14 katika uwanja wa ndani wa Taifa
Mabondia hao wenye majina makubwa
na ndio tishio kwa sasa katika tasnia ya mchezo wa Masumbwi nchini ni
Thomas Mashali atakayegombania ubingwa wa Dunia na Sajjad Mehrabi kutoka Iran
Bondia huyo aliemchachafya
Francis Cheka alipozipiga nae hapa nchini Aprili 19 mwaka 2014 katika
ukumbi wa P.T.A Sabasaba na kutoka nae droo sasa anakuja kuzipiga kwa ajili ya ubingwa wa Dunia nchini Tanzania
Mabondia wengine waliotia saini ya kuzipiga siku hiyo ni Ramadhani Hauli atakayezipiga na Salim Salim kutoka Malawi na Nassibu Ramadhani pamoja na Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ watatafutiwa wapinzani kutoka nje ya nchi. Nae katibu wa shirikisho la maswumbwi ya kulipwa PST Anton Ruta aliyekuwa msimamizi kwa upande wa chama amesema
kuwa Mpambano huo wa kimataifa kwa mabondia wote ambapo takribani ugeni
wa nchi nne kwa Pamoja utakuwa nchini Tanzania kwa ajili ya kuzipiga
hapa nchini likiwemo pambano moja la ubingwa wa Dunia linalosubiriwa kwa
hamu kubwa sana
No comments:
Post a Comment