Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(kushoto), Akisalimiana na wafanyakazi wa Mashirika mbalimbali ya
Kitaifa na Kimataifa Yanayoshirikiana na Serikali ya Tanzania kutoa
huduma katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, iliyoko wilayani Kasulu,
mkoani Kigoma.Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi
ikiwemo kutembelea kambi za wakimbizi zilizopo ndani ya mkoa wa Kigoma.
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia),
akizungumza Na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ibungho, Anatory
Nsamizanala(wa kwanza kushoto), Mara baada ya kufika katika shule hiyo
inayotoa elimu ya awali katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu, iliyopo
wilayani Kasulu, mkoani Kigoma. Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa
ziara ya kikazi ikiwemo kutembelea kambi za wakimbizi zilizopo ndani ya
mkoa wa Kigoma.Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald
Guninita.
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(kulia),
akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Ruth Msafiri (wa pili kulia),
kukagua ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Mabamba kilichopo wilayani
Kibondo,mkoani Kigoma.Kituo hicho cha Polisi kinajengwa kwa ushirikiano
kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Kimataifa la kuhudumia
Wakimbizi(UNHCR). Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi
ikiwemo kutembelea kambi za wakimbizi zilizopo ndani ya mkoa wa Kigoma.
Mkimbizi
kutoka nchini Burundi, Exavery Christopher (aliyevaa kofia nyeupe),
akitoa maelezo mbele ya Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(wa kwanza kushoto), wakati akijibu maswali
aliyoulizwa na Naibu Waziri muda mfupi baada ya kuwasili katika kituo
cha Uhamiaji cha Mabamba tayari kwa kusajiliwa kabla ya kupelekwa
kambini.Wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kibondo, Ruth Msafiri.
Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ikiwemo kutembelea
kambi za wakimbizi zilizopo ndani ya mkoa wa Kigoma.Ziara iliofanyika
tarehe 30/3/2016.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Waziri Makamba Afanya Mazungumzo Na Balozi Wa Spain Nchini Tanzania
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba akiongea na Balozi wa Spain nchini Tanzania Bw. Felix Costales.
Balozi huyo alimtembelea Mh. Makamba na kufanya mazungumzo ya kudumisha
uhusiano baina ya nchi hizo mbili katika sekta ya Hifadhi na Usimamizi
wa Mazingira.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba akiagana na Balozi wa Spain nchini Tanzania Bw. Felix Costales
mara baada ya kufanya mazungumzo Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam.
Serikali Kupitia Upya Mikataba ya TRL
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati)
akimsikiliza mmoja wa Abiria anayetumia usafiri wa reli ya kati mkoani
Kigoma. Kushoto ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe na Kulia ni
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Saveli Maketta.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza
na wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), mkoani Kigoma.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili
kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kapteni wa Meli ya MV Liemba ya
namna inavyoendeshwa, mkoani Kigoma.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu
kulia), akipata ufafanuzi wa namna ya injini za Meli ya MV Liemba
zinavyofanya kazi wakati alipotembelea Meli hiyo mkoani Kigoma.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (mwenye
kizibao cha njano), akimsikiliza Kapteni Winton Mwassa (wa kwanza
kulia), kutoka Kampuni ya huduma za meli mkoani Kigoma mara baada ya
kutembelea na kuona hali ya MV Liemba.
Na Mwamvita Mtanda
Serikali imeliagiza Shirika la
Reli Tanzania (TRL), kupitia upya mikataba ya ununuzi wa Vichwa vya
treni na mabehewa ili kubaini kasoro zilizojitokeza na kuchukua hatua
stahiki kabla ya maboresho ya reli ya Tanga-Moshi-Arusha.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa agizo hilo Mkoani Kigoma
wakati akikagua miundombinu ya reli na kusissitiza nia ya serikali
kufufua Reli ya kanda ya kaskazini ili kuimarisha huduma ya uchukuzi
katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.
“Kama Serikali tumewekeza vya
kutosha katika TRL, hivyo tunawataka mfanye biashara itakayolipa nasi
tutahakikisha popote reli ilipo inatoa huduma iliyokusudiwa na kuchangia
kukuza uchumi wa nchi”, amesema Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amewataka
wafanyakazi wa TRL kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kupata Bidhaa
na abiria wengi wa kuwasafirisha nchini kote.
Amesema Serikali imedhamiria
kuliongezea nguvu TRL ambapo baadhi ya mitambo kutoka Kampuni Hodhi ya
Rasilimali za Reli (RAHCO) itakabidhiwa kwa shirika hilo hivyo kulitaka
kuwa na mpango madhubuti wa kufanya biashara na kurudisha hadhi ya
usafiri wa reli hapa nchini.
“Fanyeni bidii ili mpate mzigo wa
kusafirisha kutoka Tanga kwenda Moshi na Arusha ili kufikia lengo la
kubeba mzigo wa tani milioni moja kwa mwaka”, amesisitiza Waziri Prof.
Mbarawa.
Amezungumzia umuhimu wa TRL
kuafanya kazi kwa karibu na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini
(TPA), ili kuongeza kasi ya huduma za uchukuzi nchini, kuongeza fursa za
ajira na kukuza pato la shirika na taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa
TRL, Bw. Masanja Kadogosa amesema TRL imejipanga kutafuta masoko ndani
na nje ya nchi ili kuboresha huduma za uchukuzi na kukuza pato lake.
Katika hatua nyingine Prof.
Mbarawa amekagua Meli ya MV Liemba na kuitaka Mamlaka ya Usimamizi wa
usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), kuhakikisha meli za MV Liemba Na MV Mwongozo zinakaguliwa na kufanya kazi inavyostahili katika Ziwa la
Tanganyika.
“Tumieni fursa ya kuwa karibu na
nchi za maziwa makuu kufanya biashara ili meli zetu zipate Mzigo wa
kutosha na kuongeza mapato kwa taifa”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa ambaye yupo katika
ziara mkoani Kigoma amewataka viongozi na wafanyakazi wa taasisi zilizo
chini ya wizara yake kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuibua fursa za
kiuchumi katika ukanda wa magharibi na hivyo kufufua miundombinu
itakayochochea uchumi wa mikoa ya magharibi mwa Tanzania yenye fursa
nyingi za kibiashara.
No comments:
Post a Comment