Kamishna Mstaafu wa TRA Kitllya na Waliokuwa Wafanyakazi wa Stanbic Bank Wamerudishwa Rumande mpaka 27 Mwezi huu
Na Mwamvita Mtanda
Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya Sambamba Na Waliokuwa
Wafanyakazi wa Benki ya StanBic Tanzania, Na , Wakiwa kwenye Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini
Dar es Salaam
Sheria ni Msumeno hukata huku na huku,
kauli hii iliyosema na wahenga imewakumba baadhi Ya vigogo akiwemo
aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Harry Kitilya,
Afisa Mwandamizi wa Benki ya Stanbic Tawi la Tanzania ambaye ni Mshindi
wa Taji la Miss Tanzania 1996 Shose Sinare na Sioi Solomoni na baada ya
kupandishwa kizimbani Aprili Mosi Mwaka huu.
Watuhumiwa hao walikutana na mkono wa
sheria kwa kuburuzwa kizimbani kwa tuhuma Zilizokuwa zikiwakabili
zikiwemo za kula njama, kutenda kosa pamoja na kosa la kughushi na
kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Hakimu Mkazi Emillius Mchaurukwa amesema
kesi hiyo itasikilizwa April 27 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam baada ya kushindwa kusikilizwa leo
kutokana na kushindwa kukamilisha uandikaji wa uamuzi wa kuondoa shitaka
la
Utakatishaji fedha linalowakabili washtakiwa wote watatu.
Watuhumiwa wote watatu aWmerudishwa Rumande wakisubiri hadi 27 April Mwaka Huu ambapo kesi hiyo itasikilizwa tena.
No comments:
Post a Comment