Staa wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akitoa neno katika Kanisa la Living Water Centre.
Dar
es Salaam: Baada ya hivi karibuni kukiri kanisani kuwa ameokoka na
kumkubali Mungu kuwa bwana na mwokozi wake kisha kukengeuka na kupiga
picha chafu za nusu Utupu, waumini wamemlipua staa wa Bongo Muvi,
Elizabeth Michael ‘Lulu’ (pichani akiwa na biblia) kwa madai kuwa anatia
aibu.
Tujiunge na Kanisa La Makuti-Kawe
Mara Baada ya kushinda Tuzo ya
Mtayarishaji Bora wa Filamu Afrika Mashariki nchini Nigeria Mapema mwaka
huu kupitia Filamu ya Mapenzi ya Mungu, Lulu alihudhuria Ibada kwenye
Kanisa la Living Water Centre (Makuti-Kawe) la Apostle Onesmo Nyakura
Ndegi lililopo maeneo ya Mahakama ya Zamani, Kawe jijini Dar, kisha
akatoa sadaka ya shukrani kwa Mungu aliyemwezesha kutwaa tuzo hiyo.
Mbali
na sadaka hiyo, Lulu akiwa kanisani hapo, aliombewa na kufungukia
kuokoka, Jambo lililoibua shangwe kubwa za kumrudishia Mungu sifa na
utukufu miongoni mwa Waumini wa kanisa hilo.
Tamko La Lulu
Katika Tamko lake baada ya zoezi hilo kanisani hapo, Lulu alisema:
“Nina kila Sababu ya kumshukuru Mungu pamoja na baba yangu (Michael Kimemeta) na Mama yangu (Lucresia Karugila).
“Sijutii kuokoka kwangu na hata wakisema vyovyote I don’t care (mimi sijali) ilimradi Namuomba Mungu na Mambo yangu yana
No comments:
Post a Comment