Sunday, 31 January 2016

WAZIRI MAKAMBA ATOA MSAADA MABATI 300 KWA WAHANGA AMBAO NYUMBA ZAO ZILIZOEZULIWA NA UPEPO JIMBONI KWAKE.

93
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshugulikia Muungano na
Mazingira,January Makamba ametoa msada wa mabati 300 kwa wananchi
ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo uliosababishwa na mvua kubwa
iliyonyesha maeneo mbalimbali jimboni humo.
Nyumba hizo zilikuwa 40 ikiwemo  Kanisa  na Msikiti zimeezuliwa mapaa
katika kijiji cha Msamaka kilichopo wilayani Bumbuli kufuatia Mvua
kubwa iliyoambatana na upepo kunyesha.
Mvua hiyo imesabisha  kaya  hizo  kukosa  mahali pa kuishi , huku
wengi wa  waathirika  wakipewa hifadhi  kwenye  nyumba  za majirani
zao.
Akizungumza  na waandishi wa habari hapo Jana Afisa Mtendaji wa kijiji
cha Msamaka Mbazi Shemhando alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo
January 27 mwaka huku saa kumi jioni.
Alitaja sehemu zilizo athirika zaidi  kuwa  ni Vitongoji vya Kwemchaa,
Nazareti,CCM, Kwakorosi pamoja na kitongoji cha Kwamingojo ndio
vimeweza kuathirika na maafa hayo.
Hata hivyo aliongeza kuwa waathirika watukio hilo Kwa sasa
wamehifadhiwa kwenye nyumba za Jirani wakati utaratibu mwingine wa
kuwasaidia ukiendelea kuwekwa.
Akikabidhi msaada huo Makamba alisema kuwa kutokana na tukio hilo
anatanguliza msaada huo kwanza wakati akiendelea kutafuta msaada
zaidi.
“Nimejikusanya Kwa hiki kidogo ili kiweze kusaidia pale penye uhitaji
Kwa haraka wakati tukiendelea na utaratibu  mwingine” alisema Makamba
Makamba   aliwataka  wananchi  wote  kupanda  miti ili kuepuka  upepo
mkali  unaosababishwa  na  mvua  zinazoendelea kunyesha  katika
maeneo tofauti

Suala LaAda Elekezi Kuhusisha Wadau Wote – Waziri Mkuu

3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizunguza katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo iliyofanyika kwenye kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema suala la ada elekezi linaendelea kufanyiwa kazi na Serikali na likifika hatua nzuri litahusisha wadau wote ili kupata maoni yao.

Ametoa ahadi hiyo leo mchana (Jumapili, Januari 31, 2016) wakati akizungumza na mamia ya waumini walioshiriki ibada ya kumuingiza kazini Mkuu Mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Fredrick Onaeli Shoo iliyofanyika kwenye usharika wa Moshi Mjini, Dayosisi ya Kaskazini.

Waziri Mkuu Majaliwa ambaye alihudhuria ibada hiyo kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli alikuwa akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa na Dk. Shoo ambaye alisema kama Serikali inataka kuondoa ada elekezi haina budi kuziimarisha shule zake ili ziwe kama zilivyokuwa zamani.
Akijibu hoja kuhusu miundombinu ya reli, Waziri Mkuu alisema Serikali imeamua kufufua Miundombinu hiyo na kwamba hivi sasa inafanya mapitio ili kujua gharama halisi kwa maeneo husika. Alisema Serikali imepanga kuanza na maeneo manne ambapo la kwanza alilitaja kuwa ni reli ya kutoka Dar es Salaam – Mwanza – Tabora – Kaliua – Mpanda hadi Karema.

“Eneo la pili ni reli ya ukanda wa Kaskazini ambayo itatoka Dar es Salaam – Tanga – Arusha hadi Musoma. Ya tatu ni ya kutoka Tabora – Kahama – Kigali (Rwanda) na kuishia nchini Burundi Ambayo tunataka isaidie kusafirisha mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam. Reli ya nne ni ile ya kutoka Mtwara kupitia Tunduru kwenda Songea hadi Mbamba Bay,” alisema.

Kuhusu ulinzi wa demokrasia ndani ya Bunge, Waziri Mkuu alisema anakubaliana na Askofu Dk. Shoo juu ya mihimili yote mitatu kuheshimiana na kwamba ameshukuru kwamba ameonya juu ya lugha zinazotumika ndani ya Bunge.

“Bunge ni eneo linaloweza kujenga jamii mpya kwa sababu Bunge ni kioo na jamii ya Watanzania inatuangalia sisi tuliomo mle. Ni vema tuwe na lugha nzuri, tabia njema na hata jinsi tunavyovaa ili wanaotuona wapate hamu ya kuiga,” alisema.

Kuhusu ombi la kuibuliwa upya mchakato wa Katiba mpya, Waziri Mkuu alisema suala hilo amelichukua na anaenda kulifanyia kazi. “Nakuhakikishia Baba Askofu ushauri ulioutoa kwa Serikali tumeupokea,” alisisitiza.

Mapema, akitoa hotuba yake, Askofu Mkuu Dk. Shoo alisema Bunge ni nyumba ya demokrasia kwa hiyo jamii inatarajia kuona hoja zikijadiliwa kwa haki na amani badala kutumia ubabe na mabavu au nguvu ya dola.

“Nimewaona baadhi ya wabunge mko hapa… hili ninalolisema ni lenu na linawahusu ninyi na spika wenu. Wabunge tunzeni heshima yenu na Mungu awasaidie kulitimiza hilo. Wewe Waziri Mkuu ni Msimamizi wa shughuli za Serikali bungeni kwa hiyo una kazi ya kusimamia. Kila mhimili unapaswa utunze heshima yake…,” alisisitiza.

Kuhusu Katiba mpya, Askofu Dk. Shoo alisema Watanzania wengi wana kiu ya kuona mchakato huo ukiibuliwa upya na kukamilishwa ili nchi ipate Katiba mpya yenye kukidhi kiu ya watu wake na inayoheshimu matakwa ya wengi.

“Mchakato huo ukianza utumike kuganga majeraha yote yaliyopita. Tukifanya hivyo tutakuwa tumeisaidia Serikali ya Awamu ya Tano kuipelekea nchi yetu kule ambako imedhamiria. Yote yanawezekana tukitaka na tukipenda,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Askofu ambaye amemaliza muda wake wa kuliongoza kanisa hilo, Dk. Alex Malasusa alisema anamshukuru Mungu kwa kupata kibali cha kushuhudia Mkuu mpya wa kanisa hilo akipokea kijiti cha uongozi kutoka kwake.

“Si kwa akili na uwezo wangu bali ni kwa uweza wa Mungu kwamba nimeweza kuishuhudia siku ya leo. Ninamuomba Mungu akusaidie kuongoza kanisa hili, akusaidie kukemea na kuonya kwa upole. Najua Mungu atakupunguzia hata marafiki kwa sababu ya matamshi utakayokuwa ukiyatoa, lakini si wewe bali ni uweza wa Bwana na roho mtakatifu anayekuongoza,” alisema.
Aliahidi kuendelea kuwaombea Rais Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Majaliwa katika majukumu waliyonayo. “Msiogope kwa ajili ya majukumu mliyopewa, msihofu tunaendelea kuwaombea kwa sababu tuko pamoja na sisi ni sehemu ya utumishi wa Taifa,” alisema.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu Mkapa

2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa. Rais Dkt. Magufuli Alikwenda kumsalimia Rais mstaafu Mkapa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam Mwishoni mwa wiki

Mtaa Wa Gongo La Mboto Manispaa Ya Ilala JijiniDar Salaam WaendeleaKuunga Mkono Kauli Ya Rais Dk.John Pombe MagufuliYa Kufanya  Usafi

 Mwenyekiti wa Kikundi chaYetu Envorotec Group kinachojishughulisha na kufanya usafi katika Mtaa wa Gongo la Mboto Manispaa ya Ilala,  Ali Mwinyimkuu (kulia), akishiriki kufanya usafi na wananchi Dar es Salaam jana, ikiwa ni utaratibu waliojiwekea wa kufanya usafi kila baada ya wiki mbili ili kuunga mkono kauli Rais Dk. John Magufuli ya kufanya usafi katika maeneo tunayoishi na kufanyia shughuli zetu nchini.
 Kazi ya usafi ikiendelea.
 Mwenyekiti wa Kikundi chaYetu Envorotec Group kinachojishughulisha na kufanya usafi katika Mtaa wa Gongo la Mboto Manispaa ya Ilala,  Ali Mwinyimkuu Omari akiwaongoza wenzake kufanya usafi.
 Hapa ni kazi tu tunaukataa uchafu.
 Wanawake wakishiriki kufanya usafi eneo la relini.
 Mwenyekiti wa Mtaa huo, Bakari Shingo (Aliyevaa kaputura), akishiriki kufanya usafi na wananchi wake Dar es Salaam jana, ikiwa ni utaratibu waliojiwekea wa kufanya usafi kila baada ya wiki mbili ili kuunga mkono kauli Rais Dk. John Magufuli ya kufanya usafi katika maeneo tunayoishi na kufanyia shughuli zetu nchini.
 Usafi ukiendelea.
Wasanii wa Kikundi cha Rock Star wa Mtaa huo nao walishiriki kufanya usafi.
…………………………………………………………………………………..
Na Kalonga Kasati
 
WANANCHI wa Mtaa wa Gongolamboto Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wameendelea kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa kufanya usafi katika eneo hilo kwa wiki mara mbili ili kuyaweka mazingira yao katika hali ya usafi.
 
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea mtaa huo Dar es Salaam jana kujionea shughuli za usafi katika eneo Mwenyekiti wa mtaa huo Bakari Shingo alisema lengo lao kubwa ni kuiunga mkono kauli ya Rais Magufuli ya kufanya usafi ambapo wao wameamua kufanya usafi kwa wiki mara mbili.
 
Alisema lakini wao walianza kufanya usafi katika eneo kabla ya rais kuanza kuhimiza lakini kauli ya Magufuli ilichochea zaidi moto wa kufanya usafi kwa wananchi wa eneo hilo.
 
Shingo alisema katika mtaa wao kunavikundi ambavyo vinasaidia kufanya usafi ambapo wamegawa maeneo  na utaratibu huo umesaidia kuyaweka mazingira katika hali ya usafi.
 
Mwenyekiti wa Kikundi chaYetu Envorotec Group kinachojishughulisha na usafi katika mtaa huo Ali Mwinyimkuu  Omari alisema kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa katika suala zima la usafi katika eneo hilo kutokana na utaratibu waliojiwekea.
 
 
Alisema wanamshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Issaya Mngulumi kwa kujitoa kwake kuwapa gari la kusomba takataka kila wanapofanya usafi hali ambayo inawapa moyo wananchi wa kufanya usafi hivyo kumungana mkono Rais Dk. John Magufuli katika suala zima la usafi nchini.

 Mkuu wa Wilaya Kinondoni Paul Makonda
 
Na Kalonga Kasati
Mnamo tarehe 23 wilaya yangu iliamua kufanya upimaji wa bure wa magonjwa ya Moyo, upimaji ambao niliamini ungebeba faida kubwa nne: moja, kujenga Utamaduni wa kupima afya mara kwa mara miongoni mwa wananchi, pili kubaini Watu ambao tayari wanasumbuliwa na magonjwa ya moyo, tatu kuchukua hatua za Awali za kuwasaidia wale ambao tayari wameshashambuliwa na magonjwa hayo na Mwisho kutoa elimu juu ya namna ya kujikinga dhidi ya magonjwa yote ya moyo. 

Ugonjwa wa moyo ni ugonjwa unaoweza kuzalisha magonjwa mengi sana na kama hujafanya vipimo sahihi ni rahisi kushughulika na matokeo ya ugonjwa huku Ukiacha chanzo kikizaa magonjwa mengine. Mathalani, unaweza kujikuta Unahangaika na kuvimba kwa miguu au kuhangaika na macho ama figo aukisukari Na hata kupoteza nguvu za kiume ukifikiri ndio tatizo kumbe tatizo la msingi ni Moyo. 

Kimsingi ni kwasababu hizo nilizozianisha nilichukua hatua ya kukiomba taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete kinachosimamiwa na Profesa Janabikinisaidie kutoa huduma hiyo bure ndani ya wilaya yangu.

Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru na kuwapongeza sana madaktari kutoka taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete pamoja na mwananyamala kwa kuitikia wito na kushiriki kikamilifu kulifanya zoezi hilo. zoezi ambalo lilikuwa kubwa na Zito kwani kwa makadirio ya awali tulitegemea kupata watu wasiozidi 2000 ila Badala yake walijitokeza wananchi zaidi ya 7000 ila kutokana na umahiri wa Madaktari hao tuliweza kuhudumia zaidi ya wananchi 5900 ingawa tulilazimika kulifanya zoezi hilo kwa siku ya pili yake ambayo ilikuwa ni tarehe 24. 

Na kwa watu wengine zaidi ya 1200 waliokuwa wamebaki, zoezi lao tulilipanga na kulifanya tarehe 30 ya mwezi huu huu wa kwanza. Ukweli ni kwamba, mambo mengi yalijitokeza kwa siku hizi tatu za upimaji; wapo waliolazimika kukimbizwa kwa ambulance kuelekea hospitali za mwananyamala na muhimbili, wapo waliolazimika kupewa appointments za kuwaona madaktari, wapo waliopewa Ushauri wa matumizi ya dawa na wengine kubadilishiwa dawa sambamba na Maelekezo ya utumiaji wa chakula na ufanyaji wa mazoeziili kupunguza uzito. 

Nichukue tu fursa hii kuwapongeza wanakinondoni kwa kuitikia wito na kuniamini Mkuu wao wa wilaya na serikali yangu kwa ujumla kwamba tuna nia njema na Tunawapenda wananchi wetu kwa kuwahakikishia afya zao zinastawi na kuendelea kuwa bora siku zote. 
Kutokama na maelezo niliyoyatoa hapo juu sambamba na sababu zilizonisukuma kufanya zoezi hilo na kutokana na muitikio mkubwa wa wananchi bila kusahau matokeo ya vipimo vilivyofanyika na kupata majibu ya kwamba watu wengi wanahitaji matibabu, kubadilishiwa dawa, maelekezo ya matumizi sahihi ya vyakula pamoja na mazoezi nimefanya uamuzi wa kulifanya zoezi hili la kudumu na tayari nimeshafanya mazungumzo na hospitali kubwa na nimetafuta njia na utaratibu bora zaidi wa kulifanya zoezi hili kuwa ni zoezi la kudumu.

Sasa basi, natamka rasmi kuwa serikali ya wilaya ya kinondoni inaanza utaratibu wa kupima bure mara tatu kwa mwaka, utaratibu ambao utaanza katikati ya mwezi wa nne. Zoezi hili litafanyika kwa kupima zaidi ya magonjwa kumi ikiwemo yafuatayo: moyo, kisukari, kansa, macho, figo, meno, kifua kikuu (TB), typhoid, magonjwa ya ngozi, presha, animonia, kansa ya kizazi, kansa ya matiti, mabusha na matende. 

Kama nilivyosema hapo awali ya kwamba, nimeshafanya mazungumzo na hospitali kubwa na kila hospitali itatoa vitengo viwili au vitatu na utaratibu utakuwa hivi. Kwa mfano, utakuta banda limeandikwa Jakaya Kikwete Cardiac Institute ndani ya Banda hilo utakuta madaktari waliobobea kwenye upande wa moyo na upimaji wa Presha kwahiyo mtu anayetaka kupima moyo ama presha atakwenda moja kwa Moja kwenye banda husika. 
Ama unaingia kwenye banda limeandikwa Ocean Road hospital kwahiyo yeyote Anayetaka kupima kansa ataingia humo…hivyo hivyo kwa magonjwa mengine yote: kutakuwa na mabanda tofauti yaliyoandikwa ni hospitali gani na wanapima magonjwa gani, lengo ikiwa ni kumpa urahisi mpimaji atakayejitokeza. 

Mwisho ila si kwa umuhimu niwashukuru sana wananchi wote wa wilaya nyingine Na wale waliotoka mikoa mbalimbali ikiwemo Tanga, Pwani, Morogoro, Lindi na Dodomakwa imani yao kubwa juu ya tukio hili iliyowafanya kutoka mbali na kujisogeza mpaka viwanja vya leaders wakiwa na imani ya kupatiwa Huduma hata kama zoezi hili lilikuwa limewalenga wakazi wa wilaya ya Kinondoni. 

Sambamba na kuwashukuru wananchi niwashukuru pia waandishi wa habari Ambao wamekuwa mstari mbele kulitangaza tukio na kuhakikisha wananchi Wanapata taarifa kwa wakati. 


 

Saturday, 30 January 2016

Baadhi ya Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Baadhi ya Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Kulia ni Dkt.Peter Maziku ambae ni Daktari katika kitengo cha CTC katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure akiwa pamoja na Dkt.Charles Ludibuka ambae ni Mfamasia katika Hospitali hiyo Sekour Toure walishiriki zoezi la usafi katika Mazingira ya Hospitali hiyo.
Katika picha wakichoma uchafu baada ya usafi.
Baadhi ya Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Hapa wakiwa katika barabara ya Machemba Jijini Mwanza ambayo inatoka na kuingia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sour Toure.
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Hapa wakiwa katika barabara ya Machemba Jirani na Kituo cha mafunzo ya Lugha mbalimbali cha International Language Training Centre Jijini Mwanza ambayo inatoka na kuingia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sour Toure.
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Hapa wakiwa katika barabara ya Machemba Jirani na Kituo cha mafunzo ya Lugha mbalimbali cha International Language Training Centre Jijini Mwanza ambayo inatoka na kuingia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sour Toure.
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Hapa wakiwa katika barabara ya Machemba Jirani na Kituo cha mafunzo ya Lugha mbalimbali cha International Language Training Centre Jijini Mwanza ambayo inatoka na kuingia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sour Toure.
Wanafunzi pamoja na Watumishi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM tawi la Mwanza, pia nao walishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.

BONDIA mzaliwa wa Tanzania Omari Kimweri ambaye ni bingwa wa uzito wa flyweight nchini Deer Park, Victoria, Australia anatarajia kucheza mpambano wake mwingine  feb 26 akizipiga na  Michael Camellion kutoka Philippines  mpambano wa raundi kumi wa ubingwa wa WBA Pan African light flyweight title .
The Melbourne Pavilion, Flemington, Victoria, Australia
 
Kimweri Mpaka sasa amepanda ulingoni mara 17 tangia aanze kucheza ngumi za kulipwa mwaka 2007 akiwa Ameshinda Michezo 14 na kupoteza michezo 3
 
Bondia huyo Mtanzania anayefanya shughuli zake Australia  amewaomba watanzania kumuombea Dua kwa ajili ya mchezo wake  huo ili afanye vizuri na kushinda Mchezo huo  ambapo baada ya hapo atakuwa na Uwezo wa kupigania Ubingwa wa Dunia wa WBA.
 Kwa kuwa Maandalizi anayoyafanya kwa sasa ni Mazuri na sapoti anayoipata ni nzuri sana 
 Akishinda Mchezo huo itabadilisha maisha ya mchezaji huyo  wa masumbwi na kuwa na kipato kikubwa Wakati akipigania mikanda mikubwa inayotambulika Duniani akianzia na mkanda wa WBA ambao Ameahidiwa kucheza Baada ya kushinda mechi yake hii ya Feb. 26
 
Kimweri alitoa shukrani kwa wadau wanaomsapoti kwa makocha wa Tanzania aliokwisha fanya Nao kazi ambapo mpaka sasa anawakumbuka kwa mchango wao mkubwa kwake katika mchezo Wa Masumbwi, makocha hao ni Baba yake mzazi Idd Kimweri, kaka yake Riadha Kimweri, Habibu Kinyogoli , Rajabu Mhamila ‘Super D’ 
 
Kocha wa Tanzania Prison Remmy Ngabo,Kameda Antony pamoja na Mabondia wa mkoa wa Tanga na Antony Edoa pamoja na kaka zake wote katika mchezo wa masumbwi Twalib Kimweri Mzonge Hassan, Ibrahimu Mashi, na mama zake wote kutoka mkoa wa Tanga 
 
Ambao wamekuwa chachu kwake katika mchezo wa ngumi mpaka amefikia hatua ya kuwa hapo Alipofikia na hata kama anaishi nje ya Tanzania amesema hawezi  kusahau asili yake kwa kuwa kitovu Tanzania ndipo kitovu chake kilipozikiwa.
11
Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakipata maelezo ya Kitaalam kutoka kwa Mshauri Mwelekezi walipotembelea mradi huo kujionea hatua mbalimbali za ujenzi. Wengine ni Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Kilombero.
……………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu Morogoro
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba Yahya Amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya “Tanzania Building Works ya Jijini, Dar es Salaam” inayojenga Mradi wa Umwagiliaji Gereza la Kilimo Idete kuukamilisha mradi huo katika muda Walioongezewa ili kuwezesha kuanza kwa shughuli za uzalishaji gerezani hapo.
 
Akizungumza na Wakandarasi wa Kampuni hiyo alipofanya ziara ya kikazi Gereza Idete, Balozi Yahya amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo ni mkombozi kwa Jeshi la Magereza kwani Utawezesha uzalijashi wa chakula cha kutosha cha wafungwa waliopo magerezani pamoja na kuzalisha ziada itakayouzwa kwa Wananchi ili kuongeza Mapato Serikalini.
“Ni matarajio yangu kuwa Mkandarasi wa Mradi huu kwa kushirikiana na Mshauri Mwelekezi na Wadau wa Jeshi la Magereza atakamilisha mradi huu kwa wakati kama alivyotuahidi hivyo kuanza mara moja shughuli za uzalishaji”. Alisisitiza Balozi Yahya.
 
Naye Msimamizi wa mradi huo Mhandisi Lodia Mallion alisema kuwa mradi huo umekamilika kwa asilimia 60 ambapo tayari uchimbaji na ujenzi wa mifereji itakayokuwa ikipitisha maji kwenda mashambani imekwisha kukamilika.
 
“Mito inayotumika kama vyanzo vya maji ni mto Kilombero pamoja na mto Kiwiliwili ambapo Banio linalotunza maji kwa shughuli za umwagiliaji tayari limekamilika”. Alisikika Mhandisi Mallion.
 
Awali Mkuu wa Gereza Idete, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Nsajigwa Mwakenja akiwasilisha taarifa kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Yahya amesema kuwa kazi ya kuandaa mradi huu ilianza rasmi mwaka 2013 ambapo mradi huo unatarajiwa kukamilika Mwaka huu 2016 ambapo gharama za mradi huo zinakadiriwa kufikia kiasi cha Tsh. 2.5 Bilioni
.
Aidha amesema kuwa chakula kitakachopatikana katika mradi huo wa Gereza Idete kitatumika kulisha wafungwa waliopo magerezani na ziada itakayopatikana itauzwa kwa Wananchi hivyo kuongeza pato la Taifa.
 
Gereza la Kilimo Idete lipo Wilayani Kilombero, Mkoani Morogoro linajishughulisha na Kilimo cha Mpunga wa chakula na pia mpunga kwa ajili ya mbegu bora za Kilimo hapa nchimi. Gereza hilo lilianzishwa rasmi mwaka 1983 kwa ajili ya Kilimo cha mazao mbalimbali hususani Kilimo cha mpunga.

Mwonekano Wa Unavyoonekana Katika Lango Kuu La Kuingilia Uwanja Wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Mwonekano katika lango Kuu la Kuingilia katika Uwanja wa mpira wa CCM Kirumba Jijini Mwanza pindi mvua inaponyesha. Ni zaidi ya Usumbufu, kero na Adha kwa wanaoingia na kutoka Uwanjani hapo pindi mvua inaponyesha.
Ni zaidi ya Usumbufumbu kwa mashabiki wa mpira pindi mvua inaponyesha wanapokuwa wakiingia amba kutoka Uwanjani, katika Uwanja wa CM Kirumba Jijini Mwanza kutokana na maji kutuama katika barabara inayoingia na kutoka katika lango Kuu la kuingilia Uwanjani hapo.
Wahusika mlione hili kama changamoto inayopaswa kutafutiwa utatuzi.
IMG_4361 (1024x683)Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akizungumza na wanahabari ofisini kwake kuhusu ugeni wa Waziri mkuu ,Majaliwa Kassim Majaliwa mkoani Kilimanjaro.
IMG_4355 (1024x683)
Baadhi ya wanahabari wa mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amosi Makala ali-pozungumza nao ofisini kwake.

Na Mwandishi wetu
WAZIRI mkuu, Majaliwa Kassimu Majaliwa, leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ibada Maalum ya kumuingiza kazini askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kiluteri Tanzania(KKKT),Askofu Dk Frederick Shoo katika kanisa kuu la Moshi mjini.
Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla,amesema Waziri mkuu anatarajiwa kuwasili mkoani Kilimanjaro kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) ambapo atapokea taarifa ya mkoa kabla ya kufanya shughuli za kanisa.
Alisema waziri mkuu hataongozana na waziri yeyote wa serikali ya awamu ya tano bali wasaidizi wake na baada ya ziara hiyo maalum atarejea Dodoma kuendelea na shughuli za serikali.
Ibada hiyo maalumu itajumuisha viongozi mbalimbali wa serikali ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro sanjari na viongozi wa madhehebu tofauti ya dini,wadau wa maendeleo,waumini na Wananchi kwa ujumla.
Kutokana na ujio huo wa waziri mkuu, mkuu wa mkoa,aliwataka wananchi hususani katika wilaya za Hai na Moshi kujitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi huyo ambaye pia atapokea changamoto mbalimbali zinazoukabili mkoa
Kadhalika waziri mkuu anatarajiwa kutoa maelekezo ya serikali kulingana na changamoto zitakazojitokeza wakati anapewa taarifa ya mkoa.
Dk Shoo ambaye pia ni askofu wa dayosisi ya Kaskazini amechaguliwa kuongoza kanisa hilo kwa miaka minne na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na mtangulizi wake askofu Dk Alex Malasusa ambaye amemaliza muda wake wa uongozi.
Askofu Dk Shoo alichaguliwa mapema mwezi Agosti mwaka jana katika mkutano mkuu wa 19 wa kanisa hilo uliofanyika chuo kikuu cha Tumaini jijini Arusha baada ya kuwashinda wenzake wawili.
Uchaguzi wa nafasi hiyo uliwashindanisha askofu Dk Stephen Munga wa dayosisi Kaskazini Mashariki na Askofu Charles Mjema wa dayosisi ya Pare.

 
Na Kalonga Kasati
Charles Mombeki (Kulia) ambae ni Mkurugenzi wa International Language Training Centre akizungumza na George Binagi kuhusiana na Umhimu wa Watanzania kujifunza lugha za Kimataifa hususani Kiingereza kwa ajili ya kuendana na muingiliano wa Kimataifa uliopo katika shughuli mbalimbali ikiwemo biashara
 
“Watanzania wengi wanakosa fursa mbalimbali zilizopo. Wengine wanakosa fursa za kibiashara pamoja na kazi kutoka katika Mashirika na Makampuni mbalimbali duniani kutokana na kushindwa kufahamu lugha za Kimataifa hususani kiingereza, Kijerumani, Kifarasa, Kichina na hata lugha nyingine. Hivyo niwasihi waamue kujifunza lugha, kwa kuwa lugha inafungua milango ya mafanikio maishani”. Anasema Mombeki.
 
Anasema, Watanzania wawaandae watoto wao katika lugha ya Kiingereza katika kupata elimu, akiunga mkono shule za watu ama Mashirika binafsi kutumia lugha ya Kiingereza kufundishia, tofauti na ilivyo kwa shule za Serikali kutumia lugha ya Kiswahili katika kufundishia katika shule za msingi akitanabaisha kwamba bado kiswahili hakijawa na nafasi kubwa kutumika kimataifa kama ilivyo kiingereza ambayo ni lugha inayowaunganisha watu wote Kimataifa. 
Mombeki anadokeza kuwa wanafunzi waliofundishwa kwa misingi ya kiingereza tangu wakiwa wadogo wana nafasi kubwa ya kufikia malengo yao ikilinganishwa na wale walioanza elimu yao ya  awali na msingi kwa lugha ya kiswahili.
 
Anabainisha kuwa kuna wanafunzi wengi kutoka Mataifa ya Afrika, Amerika na Ulaya wanapenda kufika katika Centre hiyo ambayo ilianza kutoa elimu ya lugha mbalimbali tangu mwaka 1998. Pia inafundisha lugha ya Kiswahili pamoja na lugha za asili ikiwemo Kisukuma pamoja na Mila na Desturi za Tanzania.

Friday, 29 January 2016


Rais-wa-Shirikisho-la-Mpira-wa-Miguu-Jamal-Malinzi-akioneshwa-kukerwa-na-waamuzi-kuuza-mechi-600x360S

  Na Kalonga Kasati
Kufuatia Malalamiko ya klabu kadhaa za Ligi Kuu Bara juu ya Azam FC kuruhusiwa kwenda nchini Zambia wakati ligi hiyo ikiendelea, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeibuka na kuomba radhi juu ya Kitendo hicho.
TFF iliipa ruhusa Azam kwenda Zambia kushiriki michuano Maalumu iliyoandaliwa na timu ya Zesco ya Nchini Humo ambapo kikosi hicho kiliondoka Jumatatu ya wiki hii na kusababisha michezo yao miwili kupigwa kalenda, hali ambayo imezua taharuki miongoni mwa Timu za ligi kuu ambazo nazo Zimekuja Juu na kutaka zipewe Ruhusa ya kusafiri.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi, jana alizungumza na wanahabari na kusema kuwa wanaziomba radhi timu za ligi kuu kwa kitendo kilichotokea cha kuipa ruhusa Azam kwa kuwa Hakikuwa katika utaratibu mzuri.
“Kiukweli tunaomba radhi kwa kitendo ambacho tumekifanya kwa kuipa Azam ruhusa ya kwenda Zambia Hali ambayo imezua taharuki kwa timu nyingine na kusababisha wao pia kuomba ruksa ya kwenda nchi Mbalimbali, lakini tutajitahidi kuwabana pale watakaporudi kwa kuwachezesha Mara Mbili kwa wiki ili kuwafanya wawe sawa kimichezo na wenzao.

“Lakini niseme tu kuwa Tumekosea kwa Azam lakini Hatutaki kuona Timu nyingine zinachukulia Mwanya huo Nao kuleta Barua zao kwa kutaka kwenda nje ya nchi kama ilivyofanyika kwa timu hiyo.
“Hatutakuwa tayari kufanya jambo ambalo tumelikosea na tunasema hatutaipa ruhusa timu yoyote ile hata Hawa Yanga ambao nimesikia wanaomba kwenda Afrika Kusini safari hiyo haitakuwepo, watambue hilo,” Alisema Malinzi.
01 Waziri  Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na wabunge wa Mkoa wa Simiyu, Ofisini kwake Mjini Dodoma Januari 29, 2016.  Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa huo Erasto Mbwilo.
03Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Mbunge wa Vunjo, James Mbatia kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Januari 29, 2016.
z1
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akizungumza na Kaimu Mkuu wa Chuo cha ulinzi wa Taifa (NDC) Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba wakati wa ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho Makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam jana .
Z2
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, DIGP Abdulrahman Kaniki akimkabidhi zawadi Kaimu Mkuu wa Chuo cha ulinzi wa Taifa (NDC) Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba wakati wa ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho Makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam jana.DIGP ni mmoja wa Viongozi waliopitia katika chuo hicho.
Z3
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, DIGP Abdulrahman Kaniki akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa NDC (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho Makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha ulinzi wa Taifa (NDC) Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba na Brigedia Jenerali Minja.
Z4
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, DIGP Abdulrahman Kaniki akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha ulinzi wa Taifa (NDC) wakati wa ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho katika makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam jana.

BAWATA waunga mkono tamko la Serikali

WMkurugenzi wa Baraza la Waganga Tanzania (BAWATA)David Wiketye akiongea na waandishi wa Habari kuhusu waganga wanaokiuka taratibu na sheria zilizowekwa na Serikali juu ya utoaji Huduma ya tiba asili nchini, kulia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo Shaka Mohamed Shaka.

Na Kalonga Kasati
 
Baraza la Waganga Tanzania (BAWATA) wameunga mkono tamko la Serikali la kukataza waganga wa tiba asili kujitangaza katika vyombo vya habari.
 
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Baraza la Waganga Tanzania Shaka Mohamed Shaka alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu waganga wanaokiuka taratibu na sheria zilizowekwa na Serikali juu ya utoaji huduma ya tiba asili nchini.
‘’Sisi kama Baraza la Waganga Tanzania tukishirikiana na Serikali tunatoa wito kwa vyombo vya habari wasitoe matangazo ya waganga wa tiba asili kwakua jambo hili ni kosa kwa mujibu wa sheria”alisema Shaka
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Baraza hilo David Witekye ameiomba radhi Serikali kutokana na tamko la Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili Tanzania (SHIVYATIATA) Abdulraham Lutenga kwa kuitisha mkutano na waandishi wa habari bila kushirikiana na kamati yake tendaji wala vyama vinavyounda shirikisho hilo na kuwatetea wafanyabiashara wa tiba asili ambao wamejivika kilemba cha utabibu asili.
 
“kwa niaba ya BAWATA, tunaiomba radhi Serikali kutokana na tamko la Mwenyekiti wa SHIVYATIATA kupinga tamko la Serikali, tunaamini lile ni tamko lake binafsi na sio la shirikisho”. alisema Wiketye.
 
Ameongeza kuwa,wameafiki tamko la Serikali kuhusu upimaji na usajili wa dawa asili na  kupendekeza  zoezi hili kuangaliwa upya ili kuwezesha watabibu asilia kumudu gharama hizo.
Tamko hilo lilitolewa baada ya kujitokeza kwa changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoa huduma wa tiba za  asili kutozingatia Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali inayohusu afya ya ja


B2
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma Eng. Leornad Chimagu (kulia),akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu athari za mafuriko katika kingo za barabara ya Gairo-Dodoma eneo la Kibaigwa mkoani Dodoma.
B3
Muonekano wa Daraja la Dumila mkoani Morogoro lilivyo sasa kufuatia mvua zinazonyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma na kusababisha mafuriko yanayoelekea katika Mto Mkondoa.
B4
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa kingo za barabara zilizo athiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma na kusababisha uharibifu wa barabara katika eneo la Kibaigwa mkoani Dodoma.
B5
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akitoa maelekezo kwa Meneja wa TANROADS mkoa wa Dodoma Eng. Leornad Chimagu kuhusu ujenzi wa kingo za barabara hiyo kabla hazija athiri huduma za usafirishaji.
B6
Gari likipita sehemu iliyoathirika zaidi katika eneo la Kibaigwa barabara kuu ya Gairo-Dodoma.
B7
Magari yaliyoegeshwa katika kingo za barabara yanavyochangia uharibifu wa barabara na kusababisha ajali, hili ni eneo la Kibaigwa mkoani Dododma.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemwagiza Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Dodoma Eng. Leonard Chimagu kuhakikisha ukarabati wa barabara katika eneo la Kibaigwa unaanza jumapili.
Profesa Mbarawa ameyasema hayo alipokuwa akikagua athari za uharibifu wa barabara zilizosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya Iringa – Dodoma na kusababisha mafuriko yanayoharibu kingo za barabara.
 
“Hakikisheni Jumapili kazi ya ujenzi hapa inaanza na ikamilike kwa muda mfupi ili kutoathiri huduma ya usafiri katika barabara hiyo kutokana na umuhimu wake”, alisema Prof. Mbarawa.
Waziri Mbarawa amewataka TANROADS washirikiane na Kikosi cha Usalama Barabarani kudhibiti magari yanayoegeshwa katika maeneo yasiyo rasmi na hivyo kusababisha ajali na uharibifu wa barabara hususani katika maeneo ya Dumila mkoani Morogoro na Kibaigwa mkoani Dodoma.
Mapema Waziri Mbarawa alikagua ujenzi wa kingo za barabara unaoendelea katika eneo la Dumila mkoani Morogoro ambapo amemuagiza Meneja wa TANROADS mkoa wa Morogoro Eng. Dorothy Ntenga kuhakikisha ujenzi huo wa kudhibiti barabara na daraja la Dumila unakamilika kabla ya Februari 15 ili kukabiliana na mafuriko wakati wa mvua za masika zinazokaribia kuanza.
 
“Chimbeni mchanga kwenye mto ili kuwezesha maji kupita kwa urahisi na kuondoa tishio la mafuriko yanayo athiri daraja hilo wakati wa mvua za masika”, alisisitiza Waziri Mbarawa.
Naye Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro, Eng. Dorothy Ntenga amesema ili kudhibiti mafuriko katika eneo la Dumila juhudi zinaendelea kupunguza mchanga na hivyo kuwezesha kupita maji kwa urahisi.
 
Profesa Mbarawa alikuwa katika ziara ya kukagua athari za mafuriko katika barabara ya Morogoro-Dodoma ambapo maeneo ya Dumila na Kibaigwa yameathirika zaidi.

Thursday, 28 January 2016


Kivuko cha Mto Kilombero chapinduka


Mv Kilombero
WATU wapatao 30 Wameokolewa mpaka sasa Baada ya kivuko cha Mto Kilombero kushindwa kuhimili upepo mkali ulioambatana na mvua ya radi na kisha kugonga nguzo za pembeni ya mto na kukosa mwelekeo hivyo kupinduka ndani ya maji.

Tukio la kivuko hicho cha Mto Kilombero kushindwa kumudu upepo sio mara ya kwanza kujitokeza katika eneo hilo la mpakani mwa Wilaya za Kilombero na Ulanga, ambapo juzi hali kama hiyo ilijitokeza pia.

Waziri Mkuu- Serikali Imeafiki Bunge Kutorushwa Live

 Waziri Mkuu- Serikali Imeafiki Bunge Kutorushwa Live
 
 
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majiliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kwamba matangazo ya bunge hayatarushwa yote live na Television ya Taifa kama serikali ilivyosema na tayari hatua hiyo imekwisha kuanza.
Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la papo kwa papo la Mbunge wa Hai ambaye pia Ni msemaji wa kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe aliyetaka kujua kwanini serikali imefanya maamuzi ya kuzuia wananchi wasione matangazo ya Bunge moja kwa moja.
Akijibu swali hilo Waziri Mkuu amesema kwamba uamuzi wa kutoonyeshwa kwa matangazo ya moja kwa moja uliombwa na chombo cha umma chenyewe kwamba hakina uwezo kujiendesha na Uamuzi wao huo umeungwa mkono na serikali.

”Maamuzi ya chombo hiki yameungwa Mkono na serikali na Waziri Nape Nnauye amefanya kipindi Maalum kuhusiana na jambo hilo na wananchi wameelewa vizuri na wameiunga mkono serikali kwamba matangazo yatarekodiwa na yatarushwa kama kipindi Maalum usiku” Amesema Waziri Majaliwa.

Aidha chombo cha umma kitakuwa kinarusha matangazo ya moja kwa moja kwa Muda wa maswali Na Majibu kwa serikali na baada ya hapo matangazo yatarekodiwa na kurushwa katika kipindi kiitwacho leo katika Bunge.

Wabunge wa upinzani watoka tena bungeni leo

12642553_842504182527224_7294943873863264032_n
Wabunge wa upinzani wakitoka nje.
Hali ya sintofahamu imeendelea kugubika vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini Dodoma baada ya wabunge wote wa upinzani leo kutoka nje ya Bunge mara Baada ya wabunge kuanza kuchangia Hotuba ya Rais.
 
Baada ya kipindi cha maswali na majibu, yalifuata matangazo na baada ya hapo wabunge walitakiwa kuanza kuchangia hotuba ya Rais Magufuli lakini baadhi ya wabunge wa upinzani walianza kuomba Mwongozo kuhusu kauli ya waziri mkuu kuhusu ishu ya michango ya chakula wanayoendelea kulipishwa wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule za Bweni. 
 
Hata hivyo, licha ya Baadhi ya wabunge wa Ukawa akiwemo Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea kuendelea kuomba mwongozo, naibu spika aliwanyima nafasi hiyo, jambo lililosababisha Wasusie kikao hicho na kutoka nje huku wakilalamika kwamba wamezibwa midomo.

Elimu ya sheria Dar kuanza Januari 31

katanga
 
Na Kalonga Kasati

Uongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa sheria wanatarajia kutoa elimu ya sheria katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.
Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Hussein Kattanga alipokuwa akisisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupata elimu hiyo.
‘’Natoa wito kwa wananchi kuhudhuria maadhimisho ya siku ya sheria nchini yanayoashiria kuanza mwaka mpya wa shughuli za mahakama”Alisema Kattanga.
Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ya mwaka huu ni “huduma za haki kumlenga mwananchi:wajibu wa mahakama na wadau”
Ameongeza kuwa,miongoni mwa wadau watakaoshiriki katika kutoa elimu ya sheria ni pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Taasisi ya Sheria kwa Vitendo Tanzania (Law School), Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA),Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Takukuru pamoja na Polisi.
Aidha Kattanga amesema kwamba wadau hao watatoa huduma za kisheria na kimahakama kwahiyo wananchi wenye mashauri ya muda mrefu,malalamiko yoyote na mapendekezo ya uboreshaji wa utendaji kazi wa mahakama wafike na kuonana na waheshimiwa Majaji, Mahakimu,Wasajili na Watendaji wa Mahakama.
Maadhimisho hayo hufanyika nchini kila mwaka katika wiki ya kwanza ya mwezi wa pili ambapo kwa Jiji la Dar es salaam inatarajia kufanyika tarehe 31 Januari hadi Februari 3.

Serikali kuendelea kujenga barabara zaidi kwa kiwango cha lami

UJ1
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Mhe Eng Godwin Ngonyani akijibu maswali ya wabunge katika kikao cha Bunge la 11linaloendelea Mjini Dodoma.

Na Kalonga Kasati
Serikali imeahidi kuendelea na ujenzi wa barabara katika maeneo tofauti nchini kwa kiwango cha
lami ili kutatua adha kubwa ya Ubovu wa barabara ulipo katika maeneo mengi nchini.
 
Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Eng Godwin Ngonyani akijibu maswali ya wabunge waliouliza kuhusu mpango wa serikali kuboresha barabara zilizopo na kujenga mpya ili kukabiliana na adha ya ubovu wa barabara nchini.
 
Akijibu swali la Mhe Richard Mganga Ndassa Mbunge wa Sumve (CCM) lililohitaji  ufafanuzi wa serikali ni lini ujenzi wa barabara ya Magu-Bukwimba –Ngudu-Hungumalwa itajengwa kwa kiwango cha lami, Mhe Eng Godwin Ngonyani amesema katika  mwaka wa fedha 2014/15 na 2015/16 serikali ilitenga jumla ya shilling millioni 200 kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 70 na taratibu za kumtafuta Mhandisi Mshauri zinaendelea na baada ya kukamilika kwa usanifu na kupata gharama za Mradi huo, Serikali itatafuta fedha za kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
 
Aidha akijibu pia swali la Mhe Fredy Atupele Mwakibete  Mbunge wa Busokelo (CCM) Aliyehitaji kujua ni lini barabara ya Katumba-Mbambo-Tukuyu yenye urefu wa Kilometa 82 inayoanzia Katumba(RDC) kupitia Mpombo,Kandete,Isange,Lwanga, Mbambo (BDC) hadi Tukuyu (RDC) itajengwa kwa kiwango cha lami.
 
Akijibu swali hilo, Mhe. Eng Godwin Ngonyani amesema kuwa Serikali kupitia  Wakala wa Barabara (TANROADS) kwa kutambua umuhimu wa barabara hii, katika mwaka wa fedha 2009//10 Serikali ilianza maandalizi ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami na Ambapo upembuzi yakinifu na sanifu wa kina ulikamilika na baadae Serikali iliamua kujenga kilometa 10 ambapo mwezi April,2014 Wakala wa Barabara na kampuni ya CICO ilijenga barabara hiyo kuanzia Lupaso hadi Buseji,Wilayani Busokelo.
 
Serikali kupiti Wakala wa Barabara (TANROADS) inaendelea na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika Kata, Wilaya na Mikoa mbalimbali nchini  ili kukabiliana na adha ya Ubovu wa barabara ambao umesababisha watu kukosa mawasiliano baina ya maeneo.
DI3
Waandishi wa habari wakifatilia kwa makini maelezo ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Kamishina Diwani Athuman hayupo pichani wakati wa mkutano wa kuelezea mikakati na Malengo ya Serikali katika kupamabana na kudhibiti wahalifu wa kuhujumu uchumi uliofanyika leo jijini Dar  es salaam.

Na Kalonga Kasati
Serikali inaendelea kusimamia urejeshaji wa mali zilizopatikana kwa njia ya kihalifu kupitia mpango wa kupambana na uhalifu ulioanzishwa mwaka 2012 kwa kuwashtaki na kuwataifishia mali zao pindi upelelezi ukikamilika na kubainika mhalifu ana makosa hayo.
Baadhi ya watuhumiwa kadhaa wamepelewa mahakamani na kufungwa, ikiwemo mali zao kutaifishwa na kuwa mali ya Serikali.
Hayo yalisemwa na  Mkurugenzi wa Mashtaka nchini ( DPP) Biswalo Mganga wakati wa Mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ofiisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi   jijini Dar es salaam, ambapo  alisema kuwa hatua hizo zimechukuliwa mara baada ya  upelelezi wa makosa ya kuhujumu uchumi kukamilika na kumbaini mhusika.
Aidha Mganga aliongeza kwamba  mhusika  hushtakiwa na mali zake kutaifishwa kulingana na kosa lake, pia suala hili litamgusa kila mtu, wakiwemo  watumishi wa umma.
“Mhalifu wa kuhujumu uchumi wa nchi ikiwemo usafirishaji wa nyara za Serikali, uuzaji wa madawa ya kulevya na kujipatia mali kwa njia ya rushwa watatumikia adhabu ya kulipa faini, kufungwa jela na kutaifishiwa mali zake pindi atapobainika na makosa hayo” alisema  Mganga.
Alisema kufuatia mkakati huo, Jeshi la Polisi limekamilisha upelelezi wa kesi 23 ambazo ziliwasilishwa kwa DPP na kati ya hizo tatu (3) zimetolewa uamuzi na nyingine ishirini (20) ziko katika hatua ya maombi ya kupata amri ya mahakama ili ziweze kuziwa au kutaifishwa.
Alizitaja baadhi ya kesi za dawa za kulevya ambazo zimefikia ukomo na kutolewa uamuzi Januari 27, mwaka huu.
Mkoani Kilimanjaro kesi mojawapo ni Josephine Waizela, ambaye ni raia wa Kenya aliyetiwa hatiani  kwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya Cocaine  zenye uzito wa kilogram tatu zikiwa na thamani ya Sh. Milioni 162 na kufungwa kifungo cha maisha.
Kesi nyingine ni namba 46 ya mwaka 2014 kutoka pia mkoani Kilimanjaro ambayo ilihusisha watu watatu, mmoja kati yao ambaye ni Hamis Mbwana alitiwa hatiani kwa kukutwa na dawa za kulevya aina Heroine zenye uzito wa gram 3191.11 na thamani ya Sh. Milioni 143, watuhumiwa wengine wawili katika kesi hiyo waliachiwa huru.
Mganga alizitaja baadhi ya kesi nyingine za uhujumu uchumi ni namba 6 ya mwaka 2015, ilisikilizwa mkoani Mbeya ambayo iliwahusisha raia wanne kutoka nchini China waliotiwa hatiani kwa kosa la kukutwa meno ya vifaru 11. Raia hao ni  Song Lei , Xiao Shaodan, Chen Jianlin na HU Liang, ambao wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 na kulipa faini ya Sh. Milioni 9,288 kwa kila mmoja.
Kesi nyingine  ya uhujumu uchumi namba 3 ya mwaka 2016 iliyomhusisha raia wa Tanzania Amani Rashid Ngaza aliyetiwa hatiani  kwa  kosa la kukutwa na meno ya tembo nane iliyosikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Katavi, wilaya ya Mpanda. Mtuhumiwa huyo amefungwa kifungo cha miaka 30 na kullipa faini ya Sh. bilioni 1.2.
Katika mkutano huo, Mkurugenzi Maganga alibainisha baadhi ya mali zilizotaifishwa kutoka kwa wananchi kuwa ni magari matano aina ya Toyota Rv 4 mbili ,Suzuki, Toyota Surf , Hiace pamoja na nyumba  kutoka kwa washtakiwa mbalimbali wa makosa ya kuhujumu uchumi.
Aidha,  Mganga alitoa rai kwa wananchi kutoa ushirikiano bila uwoga katika kufichua mali za mafisadi ili sheria ichukue mkondo wake pamoja na kuwataka wananchi wasijihusishe kwa njia yoyote ile ili kuficha umiliki wa mali ya mtu mwingine aliyoipata kiharamu kwa nia ya kuficha uhalifu wake kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.
“Kwa mujibu wa Sheria aliyeshirikikuficha mali ya mtu mwingine inayohusiana na uhalifukwa njia yoyote ile pia anaweza kushitakiwa kama aliyetenda kosa la ufisadi,” alisema.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Kamishna Diwani Athumani alisema kuwa atakayekamatwa na kosa la wizi au mali ya haramu atatumikia adhabu na mali zake kutaifishwa.
“Mhalifu akibainika na mshataka ya wizi au kujipatia mali kwa njia ya haramu atatumikia adhabu na kutaifishiwa mali zake kama vile magari, nyumba, boti, viwanja na fedha taslimu” alisema Kamishna Athumani.
Aidha, Kamishna Athumani aliongeza kuwa uzoefu wao unawaonyesha kwamba wahalifu wanatumia majina ya wake zao, waume zao, watoto wao na wakati mwingine kutumia majina ya watu ambao hawapo ili kuendelea kufaidika na mali walizozipata kwa niia za uhalifu.
“Hakuna mhalifu atakayepona katika mapambano haya pia uhalifu haulipi na hauna nafasi nchini” alisistiza Kamishina Athuman.
Mbali na hayo, Mkurugenzi wa upelelezi Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) Alex Mfungo pia alisema kuwa wameanzisha kitengo cha kutaifisha mali zilizopatikana kwa njia ya uhalifu ikiwemo rushwa.
Tangu mwaka 1990, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitambua utaifishaji wa mali zilizopatikana kwa njia ya kihalifu kama kipaumbele katika mfumo wa haki jinai wa kupigana na uhalifu.  Haisadii sana katika jitihada za kupambana na uhalifu ikiwa mhalifu atapata adhabu ama ya kutozwa faini au kwenda jela ikiwa ataachiwa uhuru na kupewa fursa ya kutumia fedha au mali iliyopatikana kwa uhalifu huo.
Zaidi, fedha zilizoibwa na wanasiasa wala rushwa pamoja na wahalifu wengine, zinahitaji kutaifishwa na kuelekezwa katika maeneo muhimu yenye mahitaji.
Sheria ya Utaifishaji wa Mali Haramu ilipitishwa na Bunge mwaka 1991 ili kuendana na muelekeo wa Kimataifa pamoja na mikataba ya Kimataifa ambayo imeridhiwa na nchi yetu.

Wednesday, 27 January 2016

Mjane Tabu Salum Tambwe
Kalonga Kasati
 
MTU mmoja ambaye ametajwa kuwa ni raia wa Kenya anadaiwa kuiteka Manispaa ya Ilala kwa kushiriana na watendaji wasio waaminifu wa manispaa hiyo kudhulumu viwanja vya watu eneo la Pugu Mwakanga.
Raia huyo wa Kenya ametajwa kuwa ni Phinians Otieno ambaye amefungua ofisi yake eneo la Pugu Kinyamwezi Chanika ili kuwa jirani na viwanja ambavyo inadaiwa anaviuza kiujanjajanja kwa kushirikiana na watendaji wa manispaa hiyo wasio waaminifu akiwemo ofisa ardhi mwandamizi mmoja na ofisa mwingine wa manispaa hiyo ambao majina yao yanahifadhi.
 
Imeelezwa kuwa katika manispaa hiyo mkenya huyo ana ndugu zake watano ambao Wameajiriwa hapo akiwepo shemeji yake ambao wanampa siri ya viwanja vilipo na kukamilisha udhulumaji wa viwanja vya wananchi hasa katika maeneo ambayo Hayajapimwa na amekuwa akitamba kuwa hakuna mtu wa kumbabaisha kwani hata waziri Lukuvi anafahamiana naye.
 
Imedaiwa kuwa raia huyo wa kenya aliingizwa katika mchongo huo wa viwanja na kigogo mmoja wa manispaa hiyo ambaye alitimuliwa kutokana na kujihusisha na vitendo vya Rushwa ambaye alimpa tenda ya kuwapimia viwanja wananchi waliohamishwa Kipawa kupisha ujenzi wa uwanja wa ndege katika eneo hilo la Pugu Mwakanga na baada ya kupima viwanja hivyo ameingia eneo la wakazi wa Mwakanga akidai ni lake.
 
Katika tukio la aina yake ni jaribio la mkenya huyo la kutaka kumpora viwanja mjane mmoja wa eneo hilo Tabu Salum Tambwe (pichani) akidai ni vyake kwa kushirikiana na baadhi ya watendaji wa manispaa hiyo.
 
Viwanja vya mjane huyo ambavyo anataka kudhulumiwa na mkenya huyo ni 869-876 Vilivyopo Kitalu ‘N’ Pugu Mwakanga ambavyo mjane huyo amekuwa akivilipia kodi tangu avinunue lakini kutokana na mchezo mchafu unaofanywa kwa ajili ya kutaka kumdhulumu amekuwa akipigwa chenga ya kumilikishwa licha ya kutoa zaidi ya sh.milioni 21.
 
Akizungumza na Gazeti hili Tambwe alisema amepoteza fedha nyingi kwa ajili ya kupata Umilikishwaji wa viwanja hivyo ambavyo anataka kudhurumiwa.
 
Tambwe alisema kuwa tangu avinunue viwanja hivyo mwaka 2007 amekuwa akivilipia kodi na mara ya mwisho kuvilipia ilikuwa mwaka juzi ambapo alilipa sh.640,000 na kukabidhiwa stakabadhi namba 356568, 356569, 356570, 356565, 356567, 356565, 356563.
 
Mjane huyo alisema changamoto kuwa iliyopo ni kuhusu umilikishwaji wa viwanja hivyo ambapo aliambiwa ni lazima alipie kabla ya kupewa ofa ambapo katika kiwanja namba 872 alilipa sh.224,402.80, 876 alilipa sh.281,118.40, 870 alilipa sh. 247,964.80, 874 alilipa sh. 244, 567.20, 875 alilipa sh. 303,668.40, 873 alilipa sh.270,350.40 na kiwanja namba 871 alilipa sh.270,131 jumla ikiwa ni sh.milioni 21.2 fedha alizolipa kwa mkabidhi keshia mmoja ambaye yupo dirisha la malipo aliyemtaja kwa jina moja la Fatuma lakini hadi leo hii bado hajamilikishwa.
 
Hata hivyo baadhi ya maofisa wa manispaa hiyo wameoneshwa kukerwa na vitendo vinavyofanywa na mkenya huyo kwa kushiriana na wenzao na wamesema kuwa wapo tayari kutoa ushirikiano kwa Waziri Lukuvi ili kumsaidia mjane huyo apate haki yake kwani katika manispaa hiyo  wao wanaonekana kama ni takataka na mkenya huyo anaonekana ni mungu mtu.
 
“Tunawaombeni wanahabari mutusaidie katika jambo ili kwani watu wengi wanaendelea kuumizwa na watendaji wenzetu wasio waaminifu wakishirikiana na mkenya huyo ambaye si raia hapa nchini lakini amekuwa milionea kwa kuuza ardhi kiujanjaujanja sisi tupo tayari kusema ukweli” alisema ofisa mmoja wa manispaa hiyo kwa uchungu.
 
Imeelezwa kuwa mkenya huyo kwa wakazi wote aliyewauzia viwanja katika eneo hilo Amekuwa akiwatoza kodi ambayo ilipaswa kulipwa serikalini lakini uichukua na kuitia mfukoni mwake.
 
Mjane huyo anamuomba Waziri Lukuvi kumsaidia ili apate haki yake ambayo ipo hatarini kupotea kupitia watumishi wa waliochini ya wizara yake wanaoshirikiana na raia huyo wa Kenya.
 
Akitoa ufafanuzi wa madai hayo mkenya huyo alidai kuwa mama huyo alitapeliwa kwa kuuziwa viwanja hivyo ambavyo si vyake na mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Dullah na kwamba yeye alikuwa akimsaidia ili kupata haki yake.