Sunday, 26 February 2017

Yoweri Museveni ametoa wito wafanyabiashara wa Kitanzania kwenda kuwekeza nchini Uganda.

MUSEVENI
Na. Immaculate Makilika na Lilian  Lundo- MAELEZO.
.
Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Museveni ametoa wito wafanyabiashara wa Kitanzania kwenda kuwekeza nchini Uganda.
Rais Museveni ametoa kauli hiyo leo wakati alipotembelea viwanda vya Kampuni ya  Bakhresa vinavyozalisha Unga na Juisi  vya  Buguruni na Vingunguti jijini Dar es Salaam.
“Nawakaribisha  wafanyabiashara wa Kitanzania kuja nchini Uganda kuwekeza kwani kufanya hivyo kutasaidia kuzalisha bidhaa, upatikanaji wa soko pamoja na ajira” alisema Rais Museveni.
Kauli hiyo ya Rais Museveni imetokana na mafanikio yanayotokana na Mwekezaji wa Kitanzania Said Salim Bakhresa aliyewekeza nchini Uganda ambapo anamiliki Kiwanda cha kusanga ngano nchini humo.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa  Mahusiano wa Kampuni za Bakhresa Hussin Sufiani amesema kwamba Kampuni hiyo iko mbioni kuongeza uzalishaji wa unga wa ngano kutoka tani 1,100 hadi kufikia tani 2,000 kwa siku nchini Uganda.
Aidha, amesema kutokana na uwekezaji wa Kampuni hiyo nchini Uganda jumla ya Waganda 650 wamenufaika na ajira mbalimbali ambazo zinasaidia kuwapatia kipato.
Kwa upande wa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwaijage amesema kuwa Uganda na Tanzania zimeingia makubaliano  ya ushirikiano katika sekta mbalimbali  ikiwemo sekta ya viwanda.
Amesisitiza Watanzania wanaweza kwenda kuwekeza nchini Uganda kwa vile nchi hiyo wanalima tani milioni 4 za mahindi lakini wana uwezo wa kutumia tani milioni moja pekee, hivyo ni fursa kwa wafanyabiashara wa Kitanzania kwenda kuwekeza nchini humo.
“Tunawahamasisha wafanyabiashara wa Uganda na Tanzania kuwekeza katika nchi zao ili kuzalisha , bidhaa na ajira za kutosha kwa wananchi” alisema Waziri Mwijage.

Rais wa FIFA azindua ujenzi wa Hoteli Rwanda

Rais wa FIFA Gianni Infantino amezindua ujenzi wa Hoteli ya chama cha soka cha Rwanda kwa gharama za FIFA.
Bwana Infantino ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Hoteli hiyo inayojengwa mjini Kigali karibu na uwanja wa taifa Amahoro.
FIFA tayari imeshatoa kitita cha dolla za Marekani milioni 4,1 kwa ajili ya ujenzi wa Hoteli hiyo huku zikiwa zimesalia dolla milioni 2.
Mwenyekiti wa chama cha soka cha Rwanda FERWAFA Bwana Nzamwita De Gaule, amesema Hoteli hiyo itatumiwa kupokea timu mbali mbali kutoka ng'ambo zinazokwenda kucheza nchini Rwanda.
"Hii Hoteli itakuwa na vyumba 48 vikiwemo vyumba 4 vitakavyojengwa kwa ajili ya walemavu.itakuwa na uwezo wa kupokea timu mbili za taifa kwa wakati mmoja au vilabu 3 kwa wakati mmoja".Amesema mkuu wa chama cha soka cha Rwanda.
Amesisitiza mradi wa Hoteli hiyo ulilenga kukiwezesha chama cha soka cha Rwanda kuwa na uwezo wa kupata pesa za kuendeleza soka nchini Rwanda.
"Tumekuwa tukigharamia kulipia hoteli timu zinazokuja kucheza hapa Rwanda katika mashindano mbali mbali ,hata timu yetu ya taifa kuipeleka katika hoteli nyingine ilikuwa gharama kubwa.Sasa mradi huu utatusaidia na kuturuhusu kuingiza pesa za kuendeleza soka letu."
Rais wa FIFA Gianni Infantino amesema aliidhinisha kugharamia mradi wa ujenzi wa Hoteli hii kwa sababu aliutambua kama mradi mzuri wa kusaidia chama cha soka cha Rwanda kwa sababu una malengo mazuri ya kuendeleza soka ambayo pia ndiyo malengo yake.
FIFA itakuwa na mkutano wa kamati tendaji mwezi wa 10 mwaka huu nje ya makao yake mjini Zurich,na Rwanda tayari imekwishaomba kuwa mwenyeji wa mkutano huo.Kuhusu hilo Rais wa FIFA amesema uwezekano upo:
"Mpango ndio huo,lakini bado tunalijadili hilo.Tunaitambua Rwanda kutakuwa na mazungumzo zaidi kuhusu hilo" amesema Infantino.

Sitahudhuria hafla ya waandishi wa habari White House - Trump

Rais Trump ametangaza kuwa hatahudhuria hafla ya kila mwaka inayoandaliwa na chama cha waandishi wa habari wa Ikulu ya White House.
Hafula hiyo kwa kawaida huwavutia wageni mashuhuri, wanasiasa na waandishi wa habari.
Tangazo lake limetolewa juma moja baada ya Rais kuimarisha mashambulizi yake dhidi ya mashirika ya habari.
Kwa kawaida hafula hiyo ya kila mwaka ya White House hutoa nafasi kwa waandishi wa habari na Rais kusahau tofauti zao kwa muda.
Marais 15 wamewahi kuhudhuria hafula hii ya jioni ambayo huwavutia nyota wengi na imeendelea kwa zaidi ya miaka 100.
Hata hivyo uhusiano kati ya waandishi na Rais Trump umezorota kwa majuma machache yaliyopita.
Rais amewasema baadhi ya waandishi wa habari na taasisi wanazofanyia kazi kama habari bandia na kuwataja kama maadui wa wa Marekani.
Mnamo Ijumaa, Ikulu ya White House iliwafungia nje waandishi wa habari katika mkutano wa waandishi wa Rais. Miongoni mwa waliofungiwa nje ni CNN, New York Times pamoja na BBC.
Hafula hiyo ya jioni huzalisha habari za kitaifa lakini mwaka wa 2011 haukuwa mzuri wa Bwana Trump kwa sababu hafla hiyo ya chakula cha jioni, ilitoa nafasi kwa Rais Obama kumkebehi Bwana Trump kwa madai aliyokuwa ameyasambaza kila mahali kuwa Bwana Obama hakuzaliwa Marekani kwa hivyo hakustahili kuwa Rais wa taifa hilo.

Waumini msichanganywe na maneno - Chimeledya

.Askofu Mkuu wa Anglikana Tanzania, Dk Jacob Chimeledya amesisitiza kuwa dayosisi ya Dar es Salaam ipo chini yake katika kipindi hiki baada ya Askofu Dk Valentino Mokiwa kuamriwa kujiuzulu.
Aliwataka waumini wasichanganywe na maneno  kwani taratibu na katiba ilifuatwa katika kumuondoa Mokiwa.
"Nawaomba waumini wa kanisa hili kuwa  watulivu, msichanganye na maneno yanayosemwa juu ya uamuzi wa kumtaka Dk Mokiwa kujiuzulu.Tulifuata taratibu zote na hivi sasa mimi ndiye msimamizi mkuu wa dayosisi hadi hapo askofu wa jimbo atakapopatikana," amesema Dk Chimeledya
Dk Chimeledya ametoa msisitizo huo leo wakati aliposhiriki ibada ya misa ya asubuhi  iliyoongozwa na Jaji mstaafu Augustino Ramadhan iliyofanyika katika kanisa la St Albano Posta na kusema kuwa Katiba inaruhusu yeye kulisimamia kanisa kutokana na Mokiwa, kutakiwa kujiuzulu .


Malaysia yatangaza uwanja wa ndege kuwa salama baada ya kuuwawa Kim Jong-nam

Maafisa wa usalama wa Malaysia wametangaza kuwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuala Lumpur ni salama baada ya kuuawa kwa Kim Jong-nam.
Kim Jong-nam, kaka wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un aliuawa katika uwanja huo siku 12 zilizopita.
Awali, polisi walipekua jengo husika wakichunguza iwapo kulikuwa na sumu kali iliyotumiwa katika mauaji hayo aina ya VX, au sumu nyingine yo yote.
Mwanamke kutoka Indonesia, aliyekamatwa kwa kuhusika na mauaji ya ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini, anasema alilipwa dola 90, kushiriki katika kile alichofikiri, ni kitendo cha mzaha.
Wanabalozi wa Indonesia waliokutana na Siti Aisyah, wanasema aliwaambia kuwa wanaume wawili, walionekana kama Wakorea au Wajapani, walimpa mafuta yaliyofanana na yale ya mtoto kumpaka usoni mwanamme mmoja.
Mafuta hayo sasa yanafikiriwa yalikuwa na kemikali VX, moja kati ya sumu kali kabisa. Hadi sasa watu watatu wametiwa mbaroni kutokana na mauaji hayo.

kocha wa Mo Farah huenda alikiuka sheria za dawa za kuongeza nguvu za mwili

Ripoti iliyofuja inaonyesha kuwa Alberto Salazar, ambaye ni Kocha wa bingwa wa olimpiki Mo Farah, huenda alivunja sheria za dawa za kuongeza nguvu za mwili ili kuboresha matokeo ya wanariadha.
Ripoti hiyo ya kuanzia mwezi Machi mwaka uliopita ya shirika na Marekani la kupambana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu za mwili Usada, ilipewa gazeti la Sunday Times na wadukuzi wa Urusi.
Inadai kuwa bwana Salazar huenda aliwapa baadhi ya wanariadha hao dawa ya kuongeza nguvu za mwili ya L Carnitine, ambayo inaruhusiwa kutumika kw kiwango kidogo.
Bwana Salazar na Mo Farad wote wamekana kukiuka sheria za kuzuia matumizi ya dawa hizo.
Shirika Usada linasema kuwa linaifahamu ripoti hiyo na linachunguza ikiwa sheria ilikiukwa.

Saturday, 25 February 2017

ZILIZOCHUKUA NAFASI KATIKA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI FEB 26 2017


 

John Legend aomba radhi baada ta twitter yake kumtusi Trump

Kumbe sio bongo tu hata mbele wizi wa mitandao ya kijamii ya mastaa upo! Ijumaa hii John Legend alikiona cha moto baada ya akaunti yake ya Twitter kuibiwa na kuanza kutumika vibaya ikiwemo kumtukana Rais Donald Trump.
Moja kati ya ujumbe uliopostiwa kwenye akaunti hiyo wakati imechukuliwa uliandikwa, “I can’t stand by and be silent . @reakDonaldTrump you’re a bi*ch ass nigga and if I see you, I’m stopping your shit you Fu*kin cheetah.”
Lakini hatimaye muimbaji huyo amefanikiwa kuikomboa akaunti yake na kuamua kuomba radhi kutokana na kile kilichofanyiaka. John kupitia mtandao huo ameandika:

Baada ya kufukuzwa Leicester City, Claudio Ranieri asema ya moyoni

Aliyekuwa mkufunzi wa klabu ya Leicester City Claudio Ranieri baada ya kufungishiwa virago wiki hii, amesema kuwa ndoto yake imepotea ya kuendelea kuifundisha klabu hiyo.
Ranieri mwenye umri wa miaka 65 aliiongoza Leicester kushinda taji hilo licha ya kuorodheshwa kuwa na nafasi moja kati ya 5000 kushinda taji hilo.
Leicester sasa iko pointi moja juu ya eneo la kushushwa daraja huku ikiwa imesalia mechi 13.

Watu 7 wamefariki dunia kutokana na mvua kubwa ilionyesha

Watu saba wamefariki dunia wilayani Arumeru katika matukio tofauti yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha usiku wa kuamkia  leo (Februari ishirini na nne )
Akielezea matukio hayo kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa  Arusha  DCP Charles Mkumbo amesema tukio la kwanza ambalo limepoteza maisha ya watu watano limetokea katika kata ya Enaboishu baada ya  gari aina ya Toyota Premio lenye namba za usajili T 579 BSG kusombwa na maji.
Yusuph Jacob ndiye aliyekua dereva wa gari lililosombwa na maji wakiwa wanatoka kwenye sherehe za kukabidhiwa mwali anasema baada gari kuzidiwa na maji alilazimika kuegesha gari lakini maji yalizidi nguvu.

Baadhi wa mashuhuda walioshuhudia tukio hilo wanasema ushirikiano wa wananchi umesaidia kupatikana kwa miili yote ambayo imehifadhiwa kwenye nyumba ya kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru.

M/kiti wa CCM mkoa wa Kigoma afariki dunia

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma, Samson Naingo (76) amefariki dunia akiwa anapata matibabu katika hospitali ya rufaa mkoa wa Kigoma, Maweni.
Akitoa taarifa ya kifo chake, msemaji wa familia, Amon Ndinande amesema merehemu alikuwa anasumbuliwa na kisukari na shinikizo la damu, hali iliyosababisha kupata ugonjwa wa kiharusi.
Amesema kabla ya kufikwa na mauti marehemu alilazwa hospitali ya Maweni alipokuwa akipatiwa matibabu, kuanzia Februari 10 mwaka huu hadi alipofariki dunia.
Naingo aliitumikia CCM kwa miaka 20 akiwa kiongozi wa wilaya ya Kasulu na mkoa wa Kigoma.

Kaburu afunguka asema Simba wasiwe chanzo cha fujo leo

Makamu wa Rais wa klabu ya Simba SC, Godfrey Nyange Kaburu.
Makamu wa Rais wa Simba Godfrey Kaburu amefunguka na kuwataka mashabiki wa klabu ya Simba kutokuwa chanzo cha vurugu na fujo zozote katika uwanja wa Taifa katika mechi yao leo dhidi ya watani wao wa jadi Yanga kwani fujo zinarudisha nyuma klabu hiyo.
Godfrey Nyange Kaburu akiongea na EATV amesema kuwa anaamini mashabiki wa Simba ni wastaarabu na wanaipenda klabu yao hivyo wasiwe sehemu ya kuirudisha nyuma klabu hiyo

"Klabu ya Simba inapiga vita fujo na haipendelei kuona fujo zozote zile uwanjani pale leo, kwa sababu fujo zozote zile zinapelekea kurudisha nyuma maendeleo ya klabu kwa mfano utaona kutokana na fujo za kipindi kile tulipata adhabu kadhaa,  klabi imetumia pesa nyingi kugharamia miundo mbinu ile ambayo iliharibiwa na mashabiki wetu, lakini pia mmeona tulisimamishwa kwa muda kutumia Uwanja wa taifa, kwa ustarabu ambao Simba wanao si jambo jema sisi kuonekana ni vyanzo vya fujo, Simba ni watu wastarabu, watu wanapenda mchezo, ni watu ambao wanapenda klabu yao" alisisitiza Kaburu
Mbali na hilo Kaburu amewataka mashabiki kujiandaa kupokea matokeo ya aina yoyote ile kwa ustaarabu na kuepukana na fujo ambazo zinaweza kuirudisha nyuma tena klabu yao

Askari Polisi 350 katika mchezo wa Simba na Yanga

Askari Polisi wapatao 350 watamwagwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi kulinda usalama wakati Simba na Yanga zikipambana katika mchezo namba 169 wa Ligi Kuu Bara.
Askari hao watakuwa wakilinda usalama wa ndani na nje ya uwanja huo uliopo Manispaa ya Temeke na mtu yeyote atakayefanya fujo au uharibifu ataishia mikononi mwao.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas amesema, askari hao watashirikiana na watu wengine kutoka majeshi mengine na kampuni binafsi za ulinzi kuhakikisha usalama unatawala uwanjani hapo.
“Kuna polisi 350 ambao leo  watafanya mazoezi uwanjani wakijipanga kwa ajili ya kulinda kesho (leo) kuhakikisha hakuna vurugu au uhalifu wowote utakaotokea.


Friday, 24 February 2017

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI FEB 25 2017

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgBIpy0pY5kuMG6I68T5q8CD1IaJ8Jb755ySeAtc0rxism-9WcC0jdu5c5hHSE60oRi3PrTVO56vAGq2-WyFZ3M2BOsqHFqV5mSx94Z9VGydkG1Ryarund6t8Vd3ofWaGhfqT-u0BaYDw8/s1600/1.PNG

Paul Makonda:Agoma kuzungumzia tuhuma za mitandaoni

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda 
  Licha ya kuandamwa na tuhuma za kughushi vyeti,  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema hawezi kuzungumzia suala hilo kwani majibu yake yapo mtandaoni sakata lilipoanzia.
Makonda amesema  hayo leo (Ijumaa) alipoulizwa swali na wanahabari kuhusu uhakika wa taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa alinunua vyeti na kutumia jina lisilo lake.
"Maswali ya mitandaoni yanaishia mitandaoni siko hapa kupoteza focus (mwelekeo).Ukiona maneno mengi yanaibuka kwenye ishu ya dawa za kulevya ndiyo ujue vita imefika penyewe,"amesema Makonda.ag

Rooney asema atabaki Manchester United

Wayne Rooney

Nahodha wa Uingereza Wayne Rooney anasema kuwa atasalia katika klabu ya Manchester United baada ya kuhusishwa na uhamisho wa China.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 amesema kuwa anatumai kwamba atashirikishwa kamili katika mechi zilizosalia za klabu hiyo msimu huu.
Mkufunzi wa United Jose Mourinho amekataa kukana kwamba Rooney huenda akaondoka klabu hiyo mwezi huu, ijapokuwa uhamisho huo huenda usikamlike kabla ya kufungwa dirisha la uhamisho nchini China mnamo tarehe 28 Februari.
''Ni wakati wa furaha kubwa katika klabu hii na ningependa kusalia '', alisema Rooney.
Ajenti wake Paul Stretford, alisafiri kuelekea China kuona iwapo arafanikiwa kupata makubaliano, ijapokuwa haijulikani alizungumza na klabu gani.


Rais Magufuli amemteua John Kedi Mduma kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).

  Image result for magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo amemteua Dkt. John Kedi Mduma kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. John Kedi Mduma umeanza tarehe 23 Februari, 2017.
Dkt. John Kedi Mduma ni Mhadhiri Mwandamizi, Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Dkt. John Kedi Mduma anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bi. Grace Rubambey ambaye amemaliza muda wake.

Wema:Sijachukua pesa yoyote kutoka Chadema




Akizungumza na waandishi wa habari akiwa ameambata na mama yake mzazi nyumbani kwao Sinza Jijini Dar es Salaam, Wema amesema sababu kubwa ya kuhamia CHADEMA ni ili kupata nafasi ya kupigania demokrasia anayodai kuwa inapotea nchini Tanzania Tanzania.
Sababu nyingine aliyoieleza Wema ni kutelekezwa na CCM licha ya kujitolea kutoa mchango wake kwa chama hicho wakati wa kampeni cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kiasi cha kuwa hatarini kumwagiwa tindikali visiwani Zanzibar.
"Kuanzia sasa mimi siyo tena mwanachama wa CCM, na muda mfupi ujao nitachukua kadi yangu ya CHADEMA... Nimeamua kuingia CHADEMA kwa sababu nataka kupigania demokrasia, laiti ningejua, ningeingia zamani sana, najua nimewahi kusema kuwa nitakufa nikiwa CCM, lakini sikujua kama itakuwa hivi, laiti ningejua mapema basi nisingesema vile na ningejiunga CHADEMA muda mrefu sana". Amesema Wema Sepetu

 Amesisitiza kuwa hajaamia CHADEMA kwa sababu ya pesa kama ambavo imekuwa ikidaiwa, bali ni kwa ajili ya kupigania demokrasia, na kuweka wazi kuwa kuanzia sasa ameingia kwenye mapambano ya kupigania demokrasia akiwa kwenye chama ambacho anaamini kuwa ni chama peke chenye uwezo wa kurejesha demokrasia inayopotea.
"Sijachukua pesa yoyote kutoka CHADEMA, kama nimechukua hata shilingi 10,000 ya CHADEMA basi kaburi la baba yangu huko Zanzibar litikisike" - Amesema Wema
Wema pia amejibu kuhusu baadhi ya wasanii kuidai CCm ambapo amesema "Ni kweli kuna madeni mengi wasanii tunaidai CCM, lakini kila wakati tukidai tunaambiwa tukamdai JK" - Wema Sepetu

Baada ya Wema kukabidhi kadi ya CCM, mama yake pia amerudisha kadi ya CCM kusema
"Tutatembea Tanzania nzima kuinadi CHADEMA". Kauli hiyo ilikuja baada ya mama huyo kueleza jinsi ambavyo CCM haikumtendea haki


Star TV,Channel ten, Clouds FM na Times FM.vimepewa onyo kali na (TCRA)

. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  imetoa adhabu kali kwa vituo vinne vya utangazaji  kwa kukiuka maadili ya utangazaji kwa mujibu wa sheria na kuvitaka viombe radhi siku tatu mfululizo kuanzia leo (Ijumaa) kupitia taarifa ya habari.
Akitoa adhabu hizo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Valerie Msoka amesema vituo hivyo vimepewa onyo kali ikiwa ni pamoja na kutozwa faini na kuomba radhi wasikilizaji wake.
Amevitaja vituo  hivyo kuwa ni Star TV,Channel ten, Clouds FM na Times FM.

Shule za sekondari hapa nchini zinakabiliwa na changamoto sugu ya kuwepo kwa upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi

Waziri wa  elimu sayansi na teknolojia Profesa Joyce Ndalichako kushoto akiwa na na Mbunge wa Jimbo la Rufiji wa  kulia Mohamed Mchengerwa akizungumza na walimu pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari Utete wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kujionea chanagamoto mbazi mbali zinazoikabili sekta ya elimu.
2
Waziri wa elimu Sayansi na teknolojia Profesa Joyce Ndalichako kulia akiwa na baadhi ya viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Rufiji mara baada ya kufanya ziara yake  ya kikazi ya kutembelea shule mbali mbali zilizopo Wilayani Rufiji.
3
Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa aliyesimama akizungumza na walimu wa shule ya sekondari ya Ikwiriri pamoja na walimu wa shule za msingi hawapo pichani,kushoto kwake ni Waziri wa Elimu wa sayansi na Tekonolojia katika ziara hiyo.
4
Baadhi ya viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Rufiji wakiwa katika shule ya sekondari ya Ikwiriri  wakiteta jambo na Wazairi wa  elimu sayansi ya na Tekonolojia Professa Joyce Ndalichako aliyefanya ziara yake ya kutembelea shule mbali mbali Wilaya hiyo.
 NA VICTOR MASANGU, RUFIJI
Shule za sekondari hapa nchini bado zinakabiliwa  na changamoto sugu ya kuwepo kwa  upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi pamoja na kutokuwa na  vifaa vya  maabara kunachangia kwa kiasi kikubwa kushuka na kuzolota  kwa kiwango cha ufaulu kwa  wanafunzi  kutokana na kufanya vibaya katika mitihani yao ya kumaliza  kidato cha nne na sita.
Katika kuliona  hilo Waziri wa elimu sayansi na teknolojia Profesa Joyce Ndalichako alisema  kwamba serikali ya awamu ya tano kwa sasa imeshaanza kufanya mchakato kwa ajili ya kuweza kuanza kusambaza vifaa vya maabara katika shule zipatazo 1625 sambamba na  kuwaajiri walimu wa masomo ya sayansi wapatao 4200 ambao wataweza kuleta mabadiliko chanya katika kuongeza kasi ya ufundushashi.
 Waziri Ndalichoko aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi  katika Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani  ambapo aliweza  kutembelea  katika shule tatu za sekondari ikiwemo shule ya Utete,Muhoro pamoja nna Ikwiriri  kwa lengo la kuweza kujionea chagamoto zinazowakabili wanafunzi pamoja na walimu ili kuweza kuzitatutia ufumbuzi wa kudumu.
“Ni kweli changamoto hii ipo ya uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi pamoja na  vifaa vya maabara lakini nipende kuwaahidi kuwa serikali ya awamu ya tano katika kuboresha sekta ya elimu kwa sasa  ipo katika mchakato wa kuana utekeleaji wa kusambaa vifaa vya maabara katika shule 1625 pamoja na kuajri walimu wengine hivyo kwa Wilaya ya Rufiji msiwe na shaka kabisa katika hili,”alisema Ndalichako.
Aidha Prosefa Ndalichako alisema kuwa mchakato huo amabao unatarajiwa kuanza rasmi mwezi wa tatu mwaka huu pia utazigusa na baadhi ya shule za sekondari zilizzopo katika halamashauri ya Wilaya ya Rufiji ili kuweza  kuondokana kabisa na hali hiyo na kuweza kuwapa fursa wanafunzi waweze kufanya vizuri katika mitihani yao bila ya kuwa na vikwazo vyovyote vile.
Aidha Waziri huyo katika hatua nyingine alipiga marufuku kwa wanafunzi wenye tabia ya kuamua  kwenda kukesha katika ngoma  za usiku au kwenda disco na badala yake sasa  amewataka wahakikishe kwamba  wanajikita zaidi katika kuongeza juhudi na mahalifa katika  masomo yao ili kuweza kuongeza kiwango cha ufaulu.