Mkurugenzi Msaidizi
anayeshughulikia masuala ya TEHAMA toka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw.
Baltazar Kibola akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma
kuhusu uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa kuandaa Mipango,Bajeti na
kutoa Ripoti za Malaka ya Serikali za Mitaa utakaozinduliwa na Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Septemba
5,2017 mjini Dodoma kulia ni Mkuu wa Timu ya Rasilimali Fedha kutoka
mradi wa PS3 Dkt. Gemini Mtei na kushoto ni Mtaalamu kutoka ofisi ya
Rais TAMISEMI Bw. Elisa Rwamiago
Mkuu wa Timu ya Rasilimali Fedha
kutoka mradi wa PS3 Dkt. Gemini Mtei akizungumzia faida za mfumo huo
wakati wa mkutano na vyombo vya habari leo mjini Dodoma. Kushoto
ni.Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya TEHAMA toka Ofisi ya
Rais TAMISEMI Bw. Baltazar Kibola.
Mmoja wa Wataalamu kutoka ofisi ya
Rais TAMISEMI bw. Elisa Rwamiago akiongea wakati wa mkutano na
waandishi wa Habari leo mjini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi
anayeshughulikia masuala ya TEHAMA toka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw.
Baltazar Kibola
(Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo ,Dodoma
Na Beatrice Lyimo- MAELEZO
DODOMA.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Kassimu Majaliwa anatarajiwa kuzindua mfumo wa
kielektoniki wa kuandaa Mipango , Bajeti na Ripoti kwa Mamlaka ya
Serikali za Mitaa(PlanRep) na Mfumo wa Uhasibu wa Utoaji wa Taarifa za
Fedha kwenye Vituo vya Kutolea Taarifa(FFARS).
Akizungumza na waandishi wa habari
leo mjini Dodoma, Mkurugenzi msaidizi anayeshughulikia masuala ya
TEHAMA Ofisi ya Rais – TAMISEMI Baltazar Kibola amesema kuwa mifumo hiyo
inatarajiwa kuzinduliwa Septemba 5, 2017 katika ukumbi wa LAPF Mkoani
Dodoma.
Akifafanua Bw. Kibola alisema
kuwa lengo la mifumo hiyo ni kusaidia kuja na mfumo mmoja wa kitaifa
utakaowezesha kuwa na utaratibu wa kuandaa mpango na bajeti ambapo
utasaidia Hamlashauri zote nchini kuwa na muundo mmoja wa uandaaji wa
mipango na Bajeti za Serikali.
Aidha alisema kuwa lengo la Mradi
wa uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) ni kushirikiana na
Serikali katika kuimarisha mfumo ili kusaidia uandaaji wa Mipango na
Bajeti katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa katika ngazi ya kila kituo
husika.
Kwa upande wake Mkuu wa Timu ya
Rasilimali Fedha kutoka Mradi wa uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma
(PS3) Dkt. Gemin Mtei alisema kuwa lengo la mradi huo ni kufanya
maboresho ya mifumo katika Sekta za Umma ili kuongeza ufanisi.
“Mradi huu unalenga kufanya
maboresho katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la Utawala Bora,
Rasilimali watu, Rasilimali Fedha na pia katika maeneo ya TEHAMA ambapo
utasaidia ni namna gani mifumo inawezeshwa kufanya kazi kwa urahisi”
amesema Dkt. Mtei.
Aidha Dkt. Mtei amebainisha baadhi
ya maeneo yaliyolengwa kufanyiwa maboresho ikiwemo utoaji wa huduma,
kutambua watoa huduma na pia kuwekeza kwa watoa huduma ili kuwezesha
wananchi kuweza kunufaika na huduma hizo.
Vile vile Dkt. Meti alisema kuwa
Mfumo wa kielektroniki (PlanRep) iliyoboreshwa na Mfumo wa Uhasibu wa
Utoaji wa Taarifa za Fedha kwenye Vituo vya Kutolea Taarifa(FFARS)
Mradi wa (PS3) ikiwa ni mradi wa miaka mitano (2015 – 2020)
unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa (USAID) kwa
ushirikiano na Serikali ya Tanzania.
Naye Mtaalamu kutoka Ofisi ya Rais
TAMISEMI Bw. Elisa Rwamiago amesema kuwa mfumo umeundwa kwa kuzingatia
Ubora, Usimamizi wa fedha, ufanisi katika utendaji kazi wa umma,
kupunguza gharama za usimamizi na utendaji wa kazi.
“Mfumo uliokuwa ukitumika awali
ulitumia gharama nyingi, muda mwingi na pia ulihusisha watu wengi kukaa
kusafiri kukaa pamoja sehemu moja, ila mfumo huu ulioboreshwa
umerahisisha utendaji kazi na kupunguza gharama iliyokuwa ikitumika
awali” amesema Rwamiago
Akibainisha faida za mifumo hiyo
kwa Serikali Rwamiago amesema kuwa itawezesha ufuatiliaji kuanzia ngazi
za vituo vya Afya, Zahanati na shule hivyo utawezesha upatikanaji wa
taarifa kutoka katika kila kituo kwa wakati.
Vilevile amesema kuwa mifumo hiyo
ina manufaa katika ngazi zote za utendaji hivyo itasidia uunganishaji
wa Taarifa kuhusu fedha za Serikali kutoka katika ngazi ya vituo hadi
Halmashauri mpaka ngazi ya Taifa.
“Mifumo hiyo imeandaliwa katika
ubora kwa kuzingatia changamoto zilizokuwepo awali kwa lengo la kuleta
ufanisi katika utekelezaji wa kazi za Serikali” alifafanua Rwamiago.
Mradi wa uimarishaji Mifumo ya
Sekta za Umma (PS3) ni mradi uliounganisha Mikoa yote ya Tanzania na
Halmashauri zake ambapo wataalamu wa masuala ya Mipango, Bajeti,Waganga
wakuu wa Wilaya, Makatibu Afya, Mweka Hazina kutoka katika kila
Halmashauri wamepatiwa mafunzo kuhusu Mifumo hiyo.
No comments:
Post a Comment