Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP
Simon Sirro akipokea kombe la ushindi wa tatu kutoka kwa Inspekta
Hashim Abdallah wakati wa mapokezi ya wanamichezo wa Polisi waliokuwa
wakishiriki Michezo ya Majeshi ya Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki
(EAPCCO Games) nchini Uganda
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP
Simon Sirro akimpongeza Mwanariadha wa Polisi PC Basili John baada ya
kushinda medali ya Dhahabu katika Michezo ya Majeshi ya Polisi kwa nchi
za Afrika Mashariki (EAPCCO Games) nchini Uganda hivi karibuni ambapo
Polisi Tanzania ilishika nafasi ya Tatu kati ya nchi saba zilizoshiriki
michezo hiyo
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP
Simon Sirro akimpongeza Mwanamichezo wa Polisi Koplo Gaston Komba baada
ya kushinda medali ya shaba kwa upande wa Taikondo katika Michezo ya
Majeshi ya Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO Games) nchini
Uganda hivi karibuni ambapo Polisi Tanzania ilishika nafasi ya Tatu kati
ya nchi saba zilizoshiriki michezo hiyo
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP
Simon Sirro na Viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na
Wanamichezo wa Polisi walioshiriki katika michezo ya Majeshi ya Polisi
kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO Games) nchini Uganda hivi karibuni
ambapo Polisi Tanzania ilishika nafasi ya Tatu kati ya nchi saba
zilizoshiriki michezo hiyo.
Picha na Jeshi la Polisi
Na. Jeshi la Polisi.
Wanamichezo wa Polisi walioshiriki
michezo ya Majeshi ya Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO
Games) Kampala Uganda wamerejea nchini ambapo wamefanikiwa
kujinyakujilia jumla ya medali 6, 1 ya dhahabu, 2 za fedha na 3 za Shaba
na hivyo kuibuka mshindi wa tatu kwa ujumla katika michezo hiyo
iliyoshirikisha majeshi ya Polisi kutoka nchi saba.
Wanamichezo hao wamepokelewa na
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro ambapo alisema Jeshi hilo
litaendelea kushiriki michezo mbalimbali ili kujenga afya na ukakamavu
kwa Askari pamoja na kuboresha mahusiano ya utendaji kazi katika
kubadilishana uzoefu na kuiletea sifa nchi.
IGP Sirro alisema wanamichezo hao
wamefanya kazi kubwa ambapo pamoja na uchache wao wameonyesha kuwa wako
vizuri katika michezo jambo ambalo ni hazina kubwa kwa Jeshi la Polisi
Tanzania.
Kwa upande wake Kamishna wa Polisi
Jamii Mussa Ali Mussa alisema michezo hiyo imeliletea sifa taifa la
Tanzania na Jeshi la Polisi kwa ujumla hivyo kuna haja ya kuhakikisha
kuwa wanamichezo hao wanakaa kambini muda mrefu pindi itakapojitokeza
michezo mingine ili waweze kufanya vizuri zaidi.
Naye mshindi wa medali ya Dhahabu
katika riadha mita 800 PC Basil John amesema Michezo hiyo ilikuwa na
ushindani mkubwa lakini walijitahidi kupambana ili kuhakikisha wanarejea
na medali licha ya kuwa wachache katika michezo hiyo ya majeshi ya
Polisi.
Michezo hiyo ilifanyika Agosti 25
mpaka 30 mwaka huu ambapo nchi zilizoshiriki ni pamoja na mwenyeji
Uganda, Tanzania, Kenya, Rwanda, Sudan, Burundi pamoja na Sudani Kusini
ambapo Uganda ilichukua ushindi wa kwanza, Kenya wa pili na watatu
Tanzania.
No comments:
Post a Comment