Uchaguzi wa marudio wa urais nchini Kenya huenda ukaahirishwa kutoka tarehe 17 mwezi ujao.
Tume ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, imekuwa ikikutana kuangalia uwezekano
wa kuahirisha Uchaguzi huu baada ya kampuni ya Ufaransa ya Safran Morpho
kuomba muda zaidi kuboresha mitambo inayotumiwa kuwatambua wapiga kura.
Mbali na hilo, Muungano wa Upinzani Nasa, unaoongozwa na Raila Odinga,
umesema Uchaguzi hautafanyika iwapo marekebisho hayatafanyika ndani ya
Tume ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kujiuzulu kwa Ezra Chiloba
Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo.
Chama cha Jubilee cha rais Uhuru Kenyatta kinashutumu shinikizo hilo la
upinzani na kusisitiza uchaguzi ufanyike kama ulivyopangwa.
No comments:
Post a Comment