Friday, 1 September 2017

Rc Makonda kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu wa mkoa wa Dar es Salaam

nda
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ujenzi wa ofisi za kisasa 402 za walimu kwa shule za msingi na sekondari zilizobainika kukosa ofisi hizo.

Mkuu wa mkoa wa dar es salaam, Paul Makonda leo ametambulisha kamati ya ujenzi wa ofisi za kisasa 402 za walimu kwa shule za msingi na sekondari zilizobainika kukosa ofisi hizo.
Kamati ya ujenzi wa ofisi za walimu itaongozwa na Mwenyekiti Kanali Charles Mbunge kutoka JKT, Makamu Mwenyekiti ACP Solomon Urio kutoka Jeshi la Magereza, Katibu wa kamati ambaye pia ni afisa elimu wa mkoa  Hamis Lissu, Katibu Msaidizi SACP Juma Hamis kutoka jeshi la polisi pamoja na wajumbe wengine.
Makonda amesema ujenzi wa ofisi hizo utaanza september 5, 2017 chini ya vyombo vya ulinzi na usalama kutoka JKT, Polisi na Magereza walioamua kuunga mkono juhudi za mkuu wa mkoa.
Amesema kuwa hadi sasa JKT wametoa vijana 300 kwajili ya ujenzi huo huku jeshi la magereza likitoa wafungwa watakaofanya kazi ya kutengeneza matofali.
Aidha makonda amewaomba wadau na wananchi kuchangia fedha na vifaa ikiwemo mabati, nondo, saruji, kokoto, mchanga, mbao na nguvu kazi ya watu ilikuwafanya walimu wafanye kazi katika mazingira mazuri.

 
Amesema kuwa wananchi wanaweza kuchangia fedha kupitia account ya
Crdb namba 0150296180200 au kuwasilisha michango yao ofisi ya mkuu wa mkoa.
Katika ujenzi huo channel ten wameamua kumuunga mkono rc makonda kwa kuhamasisha jamii katika uchangiaji.

No comments:

Post a Comment