Katibu Mkuu Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo
ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga akitoa taarifa kuongeza muda wa uhakiki wa
NGOs alipokutana na waandishi wa habari leo hii katika ukumbi wa
Mikutano ya Wizara UDOM, Dodoma.
Msajili wa Mashirika yasiyo ya
kiserikali Bw. Marcel Katemba akitoa ufafanuzi wa kazi ya uhakiki wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuhimiza wadau kuitikia zoezi hilo katika
muda uliowekwa na Serikali alipokutana na waandishi wa habari leo hii
katika ukumbi wa Mikutano ya Wizara UDOM, Dodoma.
Katibu wa Baraza la Mashirika
yasiyo ya Kiserikali (NACoNGO’s) Bw. Ismail Suleiman akieleza
kuridhishwa kwake na nafasi ya ushiriki wa NGOs katika uendeshaji wa
zoezi la kuhakiki mashirika hayo linaloendelea kote nchini.
Mwakilishi wa Mashirkia yasiyo ya
Kiserikali (NGO’s) Bw. Jaluo Karebe akieleza kuridhishwa kwake na
uwakilishi wa wadau wa NGOs katika kuendesha zoezi la uhakiki wa
Mashirika hayo katika kituo cha kanda ya Kati mkoani Dodoma.
Baadhi ya watendaji wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakimsikiliza Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto
anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga wakati akitoa
tamko la kuongeza muda wa uhakiki wa asasi hizo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo
ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa
mashirika yasiyo ya kiserikali muda mfupi baada ya kutoa tamko la
kuongeza muda wa uhakiki wa NGOs kutoka tarehe 4/9- 20/9/2017.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WAMJW
Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WAMJW
Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambayo inajukumu la kusajili, kuratibu na
kufuatilia uendeshaji wa shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
nchini imeamua kuongeza muda wa siku 16 kwa Mashirika ambayo bado
hayajahakiki taarifa zake kwa Msajili wa Mashirikka yasiyo ya
Kiserikali kukamilisha uhakiki huo.
Akizingumza na waandishi wa Habari
Mjini Dodoma leo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba
Nkinga amesema kuwa kumekuwa na mwitikio mkubwa wa Mashirika yasiyo ya
kiserikali kuja kuandikisha taarifa za asasi zao katika vituo mbalimbali
vya usajili vya kanda.
Bibi Sihaba ameongeza kuwa
Serikali ina nia njema ya na siyo mbaya kama watu wanavyohisi katika
utekelezaji wa zoezi hili la uhakiki linaloendelea nchi nzima katika
vituo vya Kanda tano (5), na lengo ni la zoezi ni kutambua takwimu
halisi ya Mashirika yanayofanya kazi ili kuweka utaratibu mzuri wa
kutambua mchango wa kila asasi katika kuhudumia jamii katika nyanja
mbalimbali.
“Niwaombee wadau wetu watumie muda
huu tuliouongeza vizuri kwa kujitokeza kwa wingi kufanya uhakiki wa
Mashirika yao na wale wenye changamoto tutawaelekeza namna bora ya
kuzitatua”alisema Bibi Sihaba.
Aidha Msajili wa Mashirika yasiyo
ya kiserikali Bw. Marcel Katemba amewahikikishia wadau wa mashirika
yasiyo ya kiserikali nchini kuwa hakuna tatizo katika zoezi la uhakiki
wao na ni muhimu sana kujihakiki ili kujiwekea mazingira mazuri ya
kufanya kazi zao kwa uhuru na uwazi.
“ Niwahakikishie wadau wetu kuwa
zoezi hili ni muhimu sana kwenu na kwetu pia katika namna ya kuboresha
utendaji kazi wetu”alisema Bw. Katemba.
Naye Katibu wa Baraza la Mashirika
yasiyo ya Kiserikali nchini Bw. Ismail Suleiman ameishukuru Serikali
kuwa kuandaa na kuratibu zoezi la uhakiki wa mashirika hayo na kuwaomba
wamiliki wa mashirka yasiyo ya kiserikali nchini kujitokeza kuhakiki
mashirika yao.
“Niwaombe wamiliki wa Mashirika
yasiyo ya kiserikali nchini tuendelee kujitokeza kwa wingi tuje tuhakiki
mashirika yetu ili tuondokane na usumbufu mara baada ya kumalizika kwa
kuda wa uhakiki ulioongezwa”alisema Bw. Ismail.
Zoezi la uhakiki wa Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali nchini lilizinduliwa na katibu Mkuu Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Agosti 21,2017 na uhakiki
huo ulitekelezwa kwa muda wa wili mbili mpaka Septemba 04,2017.
Hata hivyo kutokana na sababu za
kijiografia na mwitikio mkubwa wa mashirika kutaka kuhakikiwa ikaamuliwa
kuongeza kwa muda wa siku 16 mpaka Septemba 20 mwaka huu, ambao ndio
utakuwa mwisho wa uhakiki.
No comments:
Post a Comment