Muogeleaji wa Dar Swim Club, Marin
DE Villard akifanya vitu vyake wakati mashindano ya Taifa yaliyofanyika
kwenye bwawa la Hopac jijini. Marin yupo kwenye kikosi cha waogeleaji
60 wa Tanzania watakoiwakilisha nchi katika mashindano ya Cana Kanda ya
Tatu.
Na Mwandishi wetu
Jumla ya nchi sita zimethibitisha
kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana
zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19
-21.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi
ya Chama Cha kuogelea nchini (TSA), Leena Kapadia amezitaja nchi hizo
kuwa ni Afrika Kusini, Zambia, Kenya, Uganda, Djibouti na wenyeji
Tanzania.
Kapadia amesema kuwa walitarajia
kuona nchi nyingi zaidi zinashiriki katika mashindano hayo, lakini
kutokana na uhaba wa fedha zimeshindwa kufanya hivyo.
“Tumezipa nafasi zaidi kutafuta
fedha ili kushiriki, tutafunga mlango wa kuthibitisha wiki moja kabla ya
mashindano,” alisema Kapadia.
Alisema kuwa Tanzania
itashirikisha waogeleaji 60 wakigawanywa kwa timu mbili (Tanzania A na
B) chini ya makocha wao, Alex Mwaipasi na Michael Livingstone.
Nchi ambazo zimeongezewa muda
wa kuthibitisha kushiriki katika mashindano ni Ethiopia, Eritrea,
Somalia, Rwanda, Sudani Kusini ambazi zipo kanda ya tatu na za kanda ya
nne ni Angola, Botswana, Comoro, Madagascar, Lesotho, Malawi, Mauritius,
Seychelles, Msumbiji, Namibia, Zimbabwe na Swaziland.
Alisema kuwa kwa kamati yao
inatafuta wadhamini kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo. Wanahitaji
kiasi cha Sh 100 milioni ili kufanya mashindano hayo kwa hadhi
inayostahili.
Alisema kuwa wanatarajia waogeleaji zaidi ya 200 kushiriki katika mashindano hayo ambayo Tanzania ni mabingwa watetezi.
Mbali ya Kapadia, kamati hiyo pia
unaundwa na wajumbe ambao ni Inviolata Itatiro, Geeta Gokarn, Phillip
Saliboko, Imani Dominic, Hetal, Linges Ramasamy, Thauriya Diria, Amina
Karume, Nitesh Patel, Nelly Coehlo na Mary Mugurusi.
No comments:
Post a Comment