Katibu Mkuu wa Wizara ya
Afya,Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya
akimkabidhi mkataba Makamu wa Raisi wa kampuni ya Neusoft Medical
System Ltd bwana Dan Zhang wakati wa kikao cha kusaini makubaliano na
kampuni yake inayotengeneza vifaa vinavyotumika katika hospitali
kilichofanyika mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini
Dar es salaam.

Baadhi ya watumishi wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto walioshiriki katika
Kikao cha kusaini makubaliano kati ya Wizara ya Afya, na kampuni ya
Neusoft Medical System wakiongozwa na Katibu Mkuu Dkt. Mpoki
Ulisubisya kilichofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.

Makamu wa Raisi wa kampuni ya
Neusoft Medical System Ltd bwana Dan Zhang akimueleza jambo Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya katika kikao cha kusaini
makubaliano na kampuni hiyo kutoka China inayotengeneza vifaa
vinavyotumika katika hospitali, katikati yao ni Mkuu wa Kitengo cha
Sheria Wizara ya Afya Tunu Temu.

Makamu wa Raisi wa kampuni ya
Neusoft Medical System Ltd bwana Dan Zhang na Mkurugenzi wa kampuni
hiyo Bi. Ying Liu wakipiga makofi kuashiria kufanikiwa kwa makubaliano
hayo yaliyoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya (Hayupo kwenye
Picha) katika tukio lililofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya
Afya,Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya
na Makamu wa Raisi wa kampuni ya Neusoft Medical System Ltd bwana Dan
Zhang wakisaini mkataba wa makubaliano baina ya Wizara ya Afya na
kampuni ya Neusoft Medical System kutoka China inayotengeneza vifaa
vinavyotumika katika hospitali , tukio lililofanyika mapema leo Ofisi
ndogo za Wizara Jijini Dar es salaam.

Makamu wa Raisi wa kampuni ya
Neusoft Medical System Ltd bwana Dan Zhang akimueleza jambo Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya katika kikao cha kusaini
makubaliano na kampuni hiyo kutoka China inayotengeneza vifaa
vinavyotumika katika hospitali, katikati yao ni Mkuu wa Kitengo cha
Sheria Wizara ya Afya Tunu Temu na wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa
Tiba Wizara ya Afya Dkt. Dorothy Gwajima.
No comments:
Post a Comment