Na Mwandishi wetu
Klabu ya Simba imemtangaza Jaji
Mstaafu wa Mahakama Kuu, Thomas Mihayo kuwa mwenyekiti wa kamati
maalum ya kumtafuta mzabuni ambaye atanunua hisa asilimia 50 za timu
hiyo kwa mujibu wa mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Afisa
Habari wa klabu hiyo, Hajji Manara imesema kuwa mbali ya Jaji Mstaafu
huyo, wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Wakili Damas Ndumbaro, Mbunge
wa Ilala, Azzan Zungu, mtaalam wa masuala ya manunuzi, Yussuf Majjid
Nassor na Abdulrazak Badru ambaye ni Mkurugenzi wa Bodi ua Mikopo ya
Elimu ya Juu Tanzania.
Manara alisema kuwa kamat hiyo
itakutana Septemba 7 (Alhamis) kuanza kazi ya kuwajadili wanachama
ambao watataka kuzinunua hisa hizo ambapo watafuata sheria za manunuzi
ya umma.
Sheria hiyo inawapa wanachama hao
kukaa siku 45 kabla ya kumtangaza mzabuni wa timu hiyo kwa mujibu wa
sheria. Klabu ya Simba imepyisha muunda mpya wa uendeshaji ambapo kwa
sasa itakuwa chini ya utaratibu wa hisa.
Klabu hiyo itamiliki hisa 50
ambazo ni sawa na Sh bilioni 20 na asilimia zilizobaki zitakuwa kwa
ajili ya wanachama au wabia ambao watagawana asilimia 50 (Sh bilioni
20).
“Nawaomba wanachama kuwa na
utulivu mkubwa kwa kipindi hiki ambacho ni muhimu kuifanya klabu kuwa
bora ndani na nje ya uwanja. Lengo ni kuwa katika mfumo wa kisasa ambao
utaifanya klabu yetu kuwa bora Tanzania na nje ya mipaka yake,” alisema
Manara.
No comments:
Post a Comment