Viongozi wazee Duniani
viongozi wazee zaidi duniani walioko madarakani, Rais Robert
Gabriel Mugabe wa Zimbabwe, anaongoza orodha hiyo akiwa na umri wa miaka
93 na siku 12 leo, akiwa ameingia ikulu ya nchi hiyo akiwa waziri mkuu
hadi sasa akiwa rais.
A
naye shika nafasi ya pili ni Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza
aliyeshika wadhifa huo tangu mwaka 1952 hadi leo ambapo atafikisha umri
wa miaka 91 hapo Aprili 21, mwaka huu.
Beji Caid Essebsi, Rais wa Tunisia tangu mwaka 2014 hadi sasa, anashika
nafasi ya tatu atakapofikisha miaka 91 ifikapo Novemba 29, akifuatiwa
na Mwenyekiti Halmashauri Kuu ya Bunge la Umma la Korea ya Kaskazini,
Kim Yong-nam, mwenye miaka 90 na siku 25 ilipofika Februari 4, mwaka
huu.
Kwa viongozi wazee zaidi waliopo madarakani na wale waliostaafu lakini
wangali hai, Mugabe anashika nafasi ya 24, Elizabeth (53), Essebsi (62)
na Kim (78).
Viongozi wazee zaidi waliowahi kushika madaraka lakini wangali hai,
anayeongoza ni Do Muoi aliyekuwa waziri mkuu wa Vietnam tangu 1988 –hadi
1996, akawa pia Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunist tangu 1991 hadi
1997 akiwa na miaka 100 na siku 33 leo.
Huyo anafuatiwa na Babiker Awadall, Waziri Mkuu wa Sudan tangu 1969
aliyefikisha miaka 100 Alhamisi iliyopita (juzi) ambapo anayeshika
nafasi ya tatu ni Yasuhiro Nakasone aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan mwaka
1982 hadi 1987 atakayefikisha miaka 98 ifikapo Mei 27.
Kwa Afrika, Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyekuwa rais wa Tanzania tangu
1985 hadi 1995, anashika nafasi ya 42 duniani atakapokuwa na miaka 92
ifikapo Mei 8, mwaka huu ambapo aliyekuwa rais wa Zambia, Kenneth Kaunda
tangu 1964 hadi 1991, anashika nafasi ya 32 duniani ambaye atakuwa na
miaka 93 ifikapo Aprili 28, mwaka huu.
Rais Dawda Jawara wa Gambia aliyepinduliwa na Yahya Jammeh, anashika
nafasi ya 33 duniani. Jawara alikuwa waziri mkuu wa nchi hiyo mwaka 1962
hadi 1970 na rais tangu 1970 hadi 1994 alipopinduliwa na Jammeh. Jawara
atafikisha miaka 93 ifikapo Mei 16 akifuatiwa na aliyekuwa rais wa
Kenya, Daniel arap Moi, tangu 1978 hadi 2002 atakayekuwa na miaka 93
ifikapo Septemba 2, mwaka huu.
Viongozi wengine wazee Afrika waliopo na waliwahi kushika madaraka ni aliyekuwa Waziri Mkuu wa Libya, Mustafa
(1954-57) ana miaka 96 na siku 34 leo (Jumamosi) akishika nafasi ya 16.
Nafasi ya 17 inashikwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Katiba la
Algeria, Abdelmalek Benhabyles mwaka 1992 akiwa na miaka 96 ifikapo
Aprili 27.
Nafasi ya 41 duniani inashikiliwa na aliyekuwa rais wa Nigeria (1979-83)
Shehu Shagari mwenye miaka 92 na siku 7 ilipofika Februari 25, mwaka
huu akifuatiwa na Antoine Gizenga aliyekuwa Waziri Mkuu wa
Congo-Kinshasa (2006-08) atakayefikisha miaka 92 ifikapo Oktoba 5 mwaka
huu.
No comments:
Post a Comment