Tuesday 28 March 2017

Mbwana Samatta kukosa Mechi ya leo dhidi ya Burundi

  Image result for mbwana samata
Nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Samatta ameondoka kurejea Ubelgiji na hatakuwepo kwenye kikosi kitakachomenyana na Burundi leo jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Samatta aliyefunga mabao yote katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Botswana Jumamosi, amelazimika kurejea ili kuwahi maandalizi ya klabu yake kwa mchezo wa Robo Fainali ya UEFA Europa League dhidi ya Celta de Vigo nchini Hispania Aprili 13. 
Kwa kumkosa Samatta, kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amemuanzisha Ibrahim Hajib kama mshambuliaji kiongozi akicheza na kiungo Farid Mussa, huku pembeni akiwatumia kiungo Muzamil Yassin kulia na winga Simon Msuva kushoto.
Kwa ujumla kikosi cha Stars leo kipo hivi; Deo Munishi ‘Dida’, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda, Salim Mbonde, Himid Mao, Muzamil Yassin, Salum Abubakr ‘Sure Boy’, Ibrahim Hajib, Farid Mussa na Simon Msuva.
Katika benchi watakuwapo Said Mohammed, Hassan Kessy, Gareiel Michael, Hassan Kabunda, Jonas Mkude, Mbarak Yussuf, Abdulrahman Juma, Shiza Kichuya na Frank Domayo.
1. Deo Munishi
2. Shomari Kapombe
3. Mohamed Hussein
4. Abdi Banda
5. Salim mbonde
6. Himid Mao


7. Simon Msuva
8. Mzamiru Yassin
9. Farid Mussa
10. Abubakary Salum
11. Ibrahim Ajib

No comments:

Post a Comment