Wednesday 22 March 2017

Serikali Ya Tanzania Na China Zasaini Program Ya Utekelezaji Wa Mkataba Wa Masuala Ya Utamaduni.

SAOBO
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Kushoto)  akizungumza na Ujumbe kutoka Jamuhuri ya watu wa China pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wizara yake (hawapo katika picha) wakati wa hafla  ya kusaini  Mkataba wa programu ya Utekelezaji wa masuala ya Utamaduni baina ya Tanzania na China wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 iliyofanyika  leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Utamaduni Jamhuri ya watu wa China Mhe. DONG WEI.
SAOBO 1
Naibu Waziri wa Utamaduni Jamhuri ya watu wa China Mhe. DONG WEI akitoa maelezo mafupi kwa  Ujumbe wa Serikali ya China pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Habari (hawapo katika picha) katika hafla  ya kusaini  Mkataba wa programu ya Utekelezaji wa masuala ya Utamaduni baina ya Tanzania na China wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 iliyofanyika  leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabariel.
SAOBO 2
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (aliyekaa kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China Mhe. DONG WEI (aliyekaa kulia) wakisaini Mkataba wa programu ya utekelezaji wa masuala ya Utamaduni baina ya Tanzania na China wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Katikati aliyesimama ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabariel.
SAOBO 3
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China Mhe. DONG WEI (kulia) wakikabidhiana Mkataba wa programu ya Utekelezaji wa masuala ya Utamaduni baina ya Tanzania na China wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
SAOBO 4
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Kushoto) akimkabidhi zawadi ya Kinyago Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Jamuhuri ya watu wa China Mhe. DONG WEI (kulia) mara baada ya kusaini Mkataba wa programu ya Utekelezaji wa masuala ya Utamaduni baina ya Tanzania na China wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM

Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye pamoja na Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Jamhuri ya  watu wa China Mhe. DONG WEI wamesaini programu ya utekelezaji wa Mkataba wa masuala ya Utamaduni wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri Nape ameeleza kuwa Mkataba huo unalengo la kuimarisha  na kuendeleza ushirikiano katika Sekta ya Utamaduni ambao umedumu kwa miaka mingi ulioasisiwa na Baba wa Taifa Mwl.Julius K. Nyerere.
“Tanzania na China tumekuwa na ushirikiano wa muda mrefu wa masuala mbalimbali ikiwemo hili la Utamaduni ambalo limetumika kukuza, kulinda na kuunganisha nchi zetu kuwa kitu kimoja”, Alisema Mhe. Waziri.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Utamaduni wa China Mhe. DONG WEI amesema kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na China uliokuwepo kwa muda mrefu  katika masuala  ya Utamaduni, Sanaa, Elimu,Ngoma na  Michezo yamesaidia kuimarisha ushirikiano uliopo na kuwezesha nchi hizi mbili kunufaisha katika maeneo hayo.
“Ushirikiano wetu wa muda mrefu katika  masuala ya Utamaduni umeleta mafanikio makubwa ambayo sote tunajivunia kila tunapokuwa pamoja”.Alisema Mhe. WEI.
Mkataba huo pamoja na mambo mengine una lengo la kuendeleza na kufanya mpango wa pamoja kwa siku za usoni, kufanya matokeo makubwa katika Sekta ya Utamaduni kati ya nchi hizo mbili, Kufanya mkutano maalum wa ushirikiano wakati muafaka, kuzidisha ushirikiano kwenye sekta ya viwanda katika bidhaa za Utamaduni na Kubadilishana wataalamu na mafunzo ya kiutamaduni.
 
Katika hatua nyingine Serikali hiyo ya China imeisaidia Wizara kiasi cha Yuan laki nne (400,000) kwa ajili ya kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya Wizara.

No comments:

Post a Comment