Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kikao cha pamoja cha
Mawaziri wa Serikali za Tanzania na Uganda pamoja na wadau kuzungumzia
mradi wa ujenzi wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi kutoka Hoima
nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Mkutano huo, uliofanyika Ikulu,
Dar es salaam, Jumanne Machi 28, 2017, ulihudhuriwa na Mawaziri wa
Nishati na Madini pamoja na Mawaziri wa Ardhi wa nchi hizo mbili,
Wanasheria wa Serikali na kampuni washirika wa mradi huo Lake Albert
(CNOOC, TOTAL na TULLOW).
Pamoja na mambo mengine, Mawaziri,
Maafisa na Wataalam wa pande zote husika walikaa na kukubaliana kwamba
rasimu ya makubaliano rasmi ya kuanza kwa mradi yawe yamekamilika na
kuwa tayari katika kipindi cha wiki mbili ili kuwezesha Marais wa
Tanzania na Uganda kuweka jiwe la msingi kuashiria kuanza ujenzi wa
kihistoria wa mradi huo wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda
hadi Chongoleani mkoani Tanga, Tanzania.
PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment