Wednesday 29 March 2017

Chelsea hawataki United wasiingie “top four”

Wanasema adui muombee njaa, Manchester United wako nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi ya Uingereza lakini vinara wa ligi Chelsea wanatamani Manchester United aishie hapo hapo asipande juu.
Unajua kwanini? Ipo hivi, Real Madrid wamepiga hodi katika klabu ya Chelsea wakitaka kuwanyakua nyota wao wawili muhimu Eden Hazard na Thibaut Courtois ambao ni wachezaji wao muhimu kabisa katika msimu huu.
Sasa achana na Hazard, Chelsea wanaona njia pekee kwa Madrid kuachana na Courtois ni kwa Manchester United kutoingia top four, United kama wasipoingia top four ina maana hawatacheza champions league tena katika msimu ujao.
United kuikosa champions league inamaanisha wachezaji wao baadhi akiwemo golikipa David De Gea wataanza kupata matamanio ya kushiriki champions league na njia pekee itakuwa kuhamia katika timu zinazoshiriki mashindano hayo.
Real Madrid kwa muda mrefu wamekuwa wakimtaka De Gea bila mafanikio, lakini sasa wanaamini United kukosa top four kunaweza kuwarahisishia kumchukua De Gea na kuachana na Courtois.

Lakini kama United wakicheza Champions league msimu ujao itakuwa ngumu kwa De Gea kuihama klabu hiyo kwani hakuna cha ziada ambacho atakifuata nje ya Old Traford.

No comments:

Post a Comment