Manchester United imepania kuhakikisha inamsajili nyota wa Barcelona,
Neymar Jr kipindi cha kiangazi baada ya kuanzisha mazungumzo ya awali.
Hata hivyo, mchezaji huyo amekuwa akionyesha waziwazi mapenzi yake kwa
timu yake ya sasa ya Barcelona, jambo ambalo limewafanya Manchester
United kuingia mfukoni na kutangaza dau kubwa ambalo litamshawishi
Neymar.
Licha ya kwamba Mashetani hao wekundu wa London wametangaza kufanya
kufuru ya usajili wa dunia kwa kulipa fedha ya uhamisho wa Pauni 170 ili
kuipata huduma yake, lakini mchezaji huyo bado amekuwa akisisitiza
kwamba anafurahia maisha akiwa na miamba hiyo ya Hispania.
Hilo limetokana na Neymar kufurahia muunganiko wa Lionel Messi na Luis
Suarez wanapokutana wachezaji hao watatu na kuunda kikosi hatari maarufu
MSN ambacho kimekuwa tishio kwa mabao.
No comments:
Post a Comment