Wapuuzi, nimekuja hapa wananitolea bastola eti rudi kwenye gari,
nimepigana kuiweka CCM madarakani anakuja mpuuzi eti usishuke kwenye
gari, mimi nape sina kinyongo na uamzi wa rais wangu, kama
sikumshawishikunichagua hivyo hata kuniacha ni sawa.
Nimejitahidikutimiza wajibu wangu, tusihangaike na Nape tuhangaike na
Tanzania inapokwenda nimekuwa mzalendo na muungwana, nimekuwa ninatimiza
wajibu wangu
Mimi ndo nlisimama kuiinua CCM, nitasemakweli daima na fitina kwangu
mwiko, kinachotukutanisha sio magwanda ya kijani, ni imani, nimefundisha
na mzee Nnauye kusema kweli na kusimamia ninachokiamini, mimi
nlishawahikufukuzwa CCM
Usipopita kwenye matatizoya kisiasa hutakomaa, Ili mbegu iote shuti
ioze, nimepandambegu ya kupigania haki, Tanzania ni yetu nchini yetu.
Mwalimu, Kawawa waliondoka na sisi tutaondoka.
Lengo la kuja hapa ni kumshukuru rais kwa alichokifanya, namshukuru kwa
kuniamini kwa mwaka mmoja, nampongeza Mwakyembe naye ni mwanahabari.
Nimefurahi kufanya kazi na nyie, muungeni mkono Mwakyembe na Rais Magufuli
Tudumishe amani na upendo wa nchi yetu, Nape ni mdogo kuliko nchi,
wakati wa aliyeniteua ameniondoa mimi nitaendelea kuwatumikia
Polisi wamezuia gari ya Nape isiondoke, ameshuka kwenye gari anamsikiliza kamanda wa polisi Kinondoni
Nape anawataka waandishi wa habari waondoke, anadai hakuna la kuwaambia tena
No comments:
Post a Comment