Saturday 25 March 2017

Israel yashutumiwa kwa kupuuza azimio la UN



Nickolay Mladenov, ni balozi wa mataifa ya Mashariki ya kati katika Umoja wa Mataifa
Balozi wa mataifa ya mashariki ya kati katika Umoja wa Mataifa ameishutumu Israel kwa kupuuza maazimio ya Umoja huo yanayohusiana na agizo la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba isitishe ujenzi wa makaazi ya walowezi wa kiyahudi katika ardhi wanayoikalia kimabavu ya Wapalestina huko ukingo wa magharibi na Jerusalem mashariki.
Balozi huyo Bw Nickolay Mladenov ameyasema tangu baraza la usalama la UN lilipowasilisha ripoti yake Israeli mwishoni mwa mwaka jana, uliokemesha ujenzi wa makaazi hayo, unaokwenda kinyume na sheria za kimataifa, Israel umeendelea kupuuzia. .
Amesema si vyema kwamba kila Israel inavyokatazwa ndivyo inavyozidisha idadi ya ujenzi wa makaazi hayo jambo linaloongeza vizingiti kwa harakati za kutafuta suluhu la mzozo na uhasama wa miaka mingi kati ya Wapalestina na Waisrael.
Pia ameshutumu vikali tabia ya makundi ya Wapalestinian ya kurusha makombora kutoka ukanda wa Gaza wakiyaelekeza Israel inayochochea mzozo huo.
Kwa upande wake balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa Danny Danon ameipuuza ripoti hiyo akisema Umoja wa Mataifa unapaswa kuacha kuifutilia Israel.

Itakumbukwa ni hatua ya Marekani ya kutopiga kura wakati wa utawala wa rais Obama ndiyo iliochangia kupita kwa azimio hilo la mwezi Disemba dhidi ya Israel , azimio ambalo lilikuwa likishindwa kutokana na kura ya turufu ya Marekani.

No comments:

Post a Comment