Thursday 30 March 2017

Kikao Cha Wadau Wa Afya Afrika Mashariki

Q
Picha ya pamoja ya mawaziri wa jumuiya ya umoja wa Afrika Mashariki Mara baada ya ufunguzi wa Kongamano LA kupanga jinsi ya kukabiliana na majanga.Kongamano hilo lilizinduliwa na Rais Pierre Nkurunzinza
Q 1
Mganga Mkuu wa Serikali toka Tanzania (wa kwanza kushoto)  Prof.Bakari Kambi akichangia mada katika mkutano huo uliokutanisha wadau wa afya kutoka Afrika mashariki.
Q 2
Baadhi ya wajumbe toka Kenya wakifuatilia mada zilizowasilisha kwenye mkutano huo.

Bujumbura,Burundi
Nchi wanachama wa Umoja wa Afika mashariki pamoja na sektarieti ya umoja huo(EAC) wamehimizwa kuharakisha mchakato wa kuhakikisha kada zingine za afya ikiwemo ya uuguzi na kada nyingine zenye sifa  na viwango vinavyofanana na madaktari kuajiriwa kwenye nchi yeyote ya Afrika Mashariki
Hayo yamesemwa jana na Waziri WA Afya,Maedeleo ya Jamiii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Kisekta la mawaziri wa Afya wa Afrika mashariki kwenye kikao cha 14 nchini hapa
Waziri ummy alisema amefurahishwa sana na hatua iliyofikiwa na  nchi wanachama wa Jumuiaya hiyo ambapo hivi sasas madaktari wanaotoka katika jumuiya hiyo kuajiriwa
Katika hatua nyingine kikao hivho kimejadili kuhusu kuimarishwa kwa mafunzo na usimamizi wa pamoja  wa waraalam wa afya,udhibiti wa magonjwa ya milipuko pamoja na magonjwa ya kuambukiza kama vile Ebola,Mafua makali ya ndege kifua kikuu(TB) na UKIMWI
Kuhusu kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto ,mawaziri wamekubaliana hao wamekubaliana kuongeza juhudi Zaidi ili kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto ndani ya Afrika Mashariki
“Bado Afrika Mashariki hatufanyi vizuri katika afya ya uzazi na mtoto na hivyo kusababisha kutofikia malengo ya kidunia ya Millenia yaliyowekwa,hivyo tuongeze jitihada katika hili”,alisema Waziri Ummy.
Aidha, Waziri Ummy ameelekeza Tume ya Utafiti wa masuala ya Afya ya  EAC ihamie mapema makao makuu yake mjini hapa kama ilivyokubaliwa kwenye vikao vya baraza la mawaziri  vilivyotangulia
Wakati huo huo Waziri Ummy akiwa nchini humo ameshiriki uzinduzi wa kongamano la Kimataifa la afya ya Sayansi lililofunguliwa na Rais wa Burundi Mhe.Piere Nkurunzinza ambalo limeandaliwa na Kamisheni ya Utafiti wa Masuala ya Afya ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
 
Kongamano hilo la siku tatu lina lengo la kujadili  na kujipanga katika kukabiliana na majanga ikiwemo ya magonjwa mapya yanayojitokeza(Emerging Diseases) na yale yanayojirudia (Re-emerging Diseases) na linawawashirikisha wataalam wa afya na watafiti kutoka nchi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment